Rais Karume Ajipanga Kujiongezea Muda Madarakani

Idimi
1. Chaguzi za visiwani zimejaa kila aina ya vituko, na vinasababishwa na uwiano wa idadi sawa kwa wanachama na washabiki wa vyama viwili vikubwa visiwani humo, hii usababisha kuwepo na kila mbinu ili kupatikana kwa ushindi kwa wahusika.

Hivyo basi sio sahihi kusema waliokimbia na mabox ya kura ni kutoka CCM, huku ikifahamika kuwa na CUF wana njia nyingi za kubadilisha matokeo ili Maalim Madevu ashinde!

Zaidi uchaguzi wa 2000, ilibidi urudiwe kutokana na mbinu chafu walizotumia CUF. CuF kuona hivyo wakasusia marudio ya uchaguzi na kumfanya Aman ashinde bila bobo.

2. Aman Karume hakuwa na nia dhahiri ya kutaka kujua ni nani aliyempigia kura na ni nani hakumpigia. Kwere hizi ziliandaliwa na UWT-Zenj kuwatia jamba jamba hasa watendaji wa juu wa SMZ, ikiwa ni matokeo ya baadhi ya watendaji wa juu kutompigia kura Komandoo Salmin mwaka 1995 na kuwa mstari mbele kutangaza ushindi wa Maalim Seif.

Aidha Aman kama kiongozi wa kisiasa alisema kuwa anawajua walimpigia kura, hii haikuwa na lengo lolote zaidi ya kupamba tu moja ya mahutubio yake kwenye mikutano ya hadhara ambayo uambatana na vijembe vya hapa na pale.

Aman Karume anajua nini maana ya uchaguzi na kamwe hawezi kupoteza muda kujua nani kampigia kura na nani hakumpigia na ukichukulia kuwa ameshashinda, na ana jukumu la kuwaongoza wote waliompigia na wale ambao hawakumpigia.
 
Malafyale unajipanga kuteuliwa kuwakilisha Jimbo la Ikulu?.

Kila la kheir
:D :D
Najaribu kuweka sawa baadhi ya hoja hapa. Zanzibar ina bahati mbaya sana kwenye siasa zake, kwani kila mtu uona anajua sana siasa za visiwa hivyo, kiasi cha kupotosha ukweli na hali halisi.
 
naam mambo ya pwani hayo

ila hili suala mbona limetoka kwa vyama ambavyo havina uhusiano wowote na karume?

sasa kujipanga huko kukoje wakati wasemaji hawajatumwa na mwenyewe
 
Idimi
1. Chaguzi za visiwani zimejaa kila aina ya vituko, na vinasababishwa na uwiano wa idadi sawa kwa wanachama na washabiki wa vyama viwili vikubwa visiwani humo, hii usababisha kuwepo na kila mbinu ili kupatikana kwa ushindi kwa wahusika.

Na hapa ndo hasa shida ilipo, uwiano wa wanachama unaolingana kati ya chama tawala na chama kikuu cha upinzani visiwani. Kwa hili nakuunga mkono, kwa asilimia 100%, lakini bado hoja inabaki pale pale.
Ni hatua gani madhubuti ambazo SMZ ilichukuwa kwa wachafuzi wale wa uchaguzi? Hatua hizi ndizo zingempa heshima kubwa raisi, kwamba anachukia madudu, tofauti na inavyoonekana sasa. Hali kadhalika hatua kali zingesaidia kupunguza hujuma ambazo tumeziona mwaka 2005 katika chaguzi za visiwani.

....Hivyo basi sio sahihi kusema waliokimbia na mabox ya kura ni kutoka CCM...

Aa wapi!
Hapa sijashawishika. Serikali (kwa muktadha huu namaanisha polisi na ZEC) ndio waliokuwa na jukumu la kuhakikisha kwamba masanduku ya kura yanakuwa salama muda wote. Viongozi wa ZEC wanachaguliwa na rais wa SMZ ambaye ni wa chama tawala. Na serikali kwa madai yao, ni ya sisiemu, sasa hapa wapinzani wanaingiaje?
Chama pinzani hawamiliki vyombo vya dola!

Zaidi uchaguzi wa 2000, ilibidi urudiwe kutokana na mbinu chafu walizotumia CUF. CuF kuona hivyo wakasusia marudio ya uchaguzi na kumfanya Aman ashinde bila bobo.

Sawa!
Kimsingi sishabikii kususia uchaguzi! Sipendi watu wa jamii ya akina Tsvangirai.
Walicholalamikia CUF miaka ile ni kwamba mazingira yaliyosababisha uchaguzi uvurugike yalikuwa hayajarekebishwa na wanaostahili kurekebisha, ndio sababu wakasusia. Hata bara, mazingira haya hayajarekebishwa mpaka sasa.

....Aidha Aman kama kiongozi wa kisiasa alisema kuwa anawajua walimpigia kura, hii haikuwa na lengo lolote zaidi ya kupamba tu moja ya mahutubio yake kwenye mikutano ya hadhara ambayo uambatana na vijembe vya hapa na pale......

Asante kwa utetezi huo, kama kweli lengo halikuwa ku-deal na wabaya wake basi utakuwa umemuondolea wasiwasi mGombea mwenzake amBaye walichukua fomu za uraisi pamoja miaka ile, ambaye ndiye alituhumiwa kwamba alimnyima kura mwanachama mwenzake.

....Aman Karume anajua nini maana ya uchaguzi na kamwe hawezi kupoteza muda kujua nani kampigia kura na nani hakumpigia na ukichukulia kuwa ameshashinda, na ana jukumu la kuwaongoza wote waliompigia na wale ambao hawakumpigia.

Hio bold ndio jukumu haswa la raisi ambaye kaomba ridhaa ya kuwaongoza wananchi bila kujali rangi, itikadi, mrengo ama maeneo wanayotoka wananchi hao. Kwa tunayoyaona na kusikia kuhusu Pemba yana-reflect hiyo bold hapo juu?

Nakushukuru kwa elimu uliyonipa!
 
Asante kwa utetezi huo, kama kweli lengo halikuwa ku-deal na wabaya wake basi utakuwa umemuondolea wasiwasi mGombea mwenzake amBaye walichukua fomu za uraisi pamoja miaka ile, ambaye ndiye alituhumiwa kwamba alimnyima kura mwanachama mwenzake.
Sasa huyo ndie king'ang'anizi wa madaraka! Well, bado ana nafasi ya kutupa tena karata yake...
 
...Sasa huyo ndie king'ang'anizi wa madaraka! ...

Kwi kwi kwi!
Huenda anataka kutimiza ndoto yake ya kuwa raisi wa visiwa vya marashi! (joke). Lakini hii haimfanyi kuitwa king'ang'anizi, ni haki yake ya kikatiba! Ni haki hii hii anayoing'ang'ania Karume wa nje ya nchi! Je naye tumpe jina hilo hapo juu?

.... Well, bado ana nafasi ya kutupa tena karata yake...

Yeeeees!
Katiba ya Jamhuri inamruhusu kufanya hivyo, provided anakidhi vigezo vya kuwa raisi. Ni haki hii pia ambayo inampa Maalim nafasi ya kugombea tena na tena bila kukata tamaa, hadi ukamilifu wa dahari!
 
Kwi kwi kwi!
Huenda anataka kutimiza ndoto yake ya kuwa raisi wa visiwa vya marashi! (joke). Lakini hii haimfanyi kuitwa king'ang'anizi, ni haki yake ya kikatiba! Ni haki hii hii anayoing'ang'ania Karume wa nje ya nchi! Je naye tumpe jina hilo hapo juu?
Kitendo chake cha kutompigia kura Karume, kinaonyesha wazi kuwa na gundu na matamaa, mbaya zaidi kwamba hakuridhika na maamuzi ya chama chake. Hivyo ni sahihi kusema ni king'ang'anizi, ilhali Ali Karume alikubali kushindwa katika mchujo na kuamua kujipanga upya kuwania nafasi ya uprezi safari hii huko visiwani.

Kinachoonekana GB ni hali ya kutaka, sitaki. Hii ni mbaya kwa wanasiasa... ni vema akawa wazi kuonyesha nia yake binafsi ya kuwa prez kule, pasipo kusubiri kufanyiwa kazi hiyo na wapambe. Hii itamjengea amani ya moyo hata pale atakaposhindwa na hatakuwa na lawama kwa kundi lolote kwa kushawishiwa kushiriki uchaguzi.

i14_k.jpg
 
Hawa washenzi. Huyu Karume ni mwizi, hatuwezi kumuachia nchi. Aonndoke harakakaaaaaa
 
huko ni kuchekesha watu wamezaliwa katika maeneo hayo wame kulia hapo leo mnawadai vitambulisho ili waandikishwe kwannini hamkuanza kutoa hivyo vitambulisho au kufanya tu sensa ndogo ya kujua nani ana cheti cha kuzaliwa na nani hana ili itakapofika katika zoezi hili iwe rahisi.leo mnawasumbua wananchi mpaka wanaonekana kama wakimbizikatika nchi yao.hivi ni lini serekali zetu zita acha kufanya mambo kwa kukurupuka.hii mipango ya muda mfupi,mipango ya kati na mipango ya muda mrefu wenzetu mna ifuata ipi hatuwaelewi.
 
.....mbaya zaidi kwamba hakuridhika na maamuzi ya chama chake. ....

Kibunango,
Kama ni maamuzi ya pale Dodoma yameumiza wengi sana katika chama tawala, si GB pekee. Kinachomfanya GB aendelee kukomaa na haya maamuzi ya chama chake ni ile "Demokrasia" ya chama chake kwamba asiyeridhika na maamuzi ya chini basi akate "rufaa", ndio sababu akaitwa na CC na "Wazee wa Busara" kwamba asioneshe kutoridhika kwake na maamuzi ya chama waziwazi kiasi kile, atakigawa chama. Ila alichokifanya ni halali yake, chama kinaruhusu, ila "mazoea" ya chama tawala hayaruhusu, kama ambavyo tumezoe kumpa mgommea uraisi wa Jamhuri kutoka chama tawala mihula miwili.

Najua unakumbuka vema kwamba mwaka 2005 GB alichukua fomu za kugombea uraisi, wale "Wazee wa Busara" wakamlazimisha kuondoa jina lake ili amwachie Karume amalize vipindi viwili. Ni mazoea haya ya chama tawala ambayo yanaua demokrasia kwa chama hiki na yanayoumiza wengi. Hii hakubaliki! Mbona raisi wa Jamhuri naye amechukua fomu mwaka 1995 na 2005 na mwakani mnamwachia awe mgombea pekee? Je naye ni king'ang'anizi?

..... Ali Karume alikubali kushindwa katika mchujo na kuamua kujipanga upya kuwania nafasi ya uprezi safari hii huko visiwani.....

Sawa. Hivi nguvu ya ushawishi ya Ali na GB kwa visiwa vya marashi inafanana kisiasa? Nani yuko juu? Nielimishe

...Kinachoonekana GB ni hali ya kutaka, sitaki. Hii ni mbaya kwa wanasiasa... ni vema akawa wazi kuonyesha nia yake binafsi ya kuwa prez kule, pasipo kusubiri kufanyiwa kazi hiyo na wapambe. Hii itamjengea amani ya moyo hata pale atakaposhindwa na hatakuwa na lawama kwa kundi lolote kwa kushawishiwa kushiriki uchaguzi.

Duh!
Fomu anachukuliwa na kujaziwa na nani?
Kila mgombea ana wapambe nyuma yake na hawakwepeki. Ndio wapangaji wa kampeni. Ndio watoa pesa za kuchukulia fomu na kupigia kampeni. Ndio viongozi wasaidizi watarajiwa. Je Karume hana wapambe?
Na JK na mtandao wake je?
Jamani chama tawala kubalini kubadilika kuendana na wakati. Acheni demokrasia ya mazoea.

Hawa washenzi. Huyu Karume ni mwizi, hatuwezi kumuachia nchi. Aonndoke harakakaaaaaa

Braza matusi ya nini? We lete hoja tuchambue na tuelimishane!
Tuhuma zako za wizi wa Karume ziletee ushahidi hapa. Hatuna cha kuficha, tutamhukumu kutokana na ushahidi wako.
 
Kibunango,

Sawa. Hivi nguvu ya ushawishi ya Ali na GB kwa visiwa vya marashi inafanana kisiasa? Nani yuko juu? Nielimishe
Ali na GB wana kitu kimoja in common, kwamba wote kwa muda mrefu wamekuwa nje ya siasa za visiwa hivyo.

Nguvu ya ushawishi baina yao, umejengeka kwa tofauti kubwa ambapo unatokana na jinsi walivyokulia ndani ya visiwa hivyo.

Ali ana ushawishi mkubwa kwa watu wenye za kati wengi wao wakiwa ni wakaazi wa mjini. Kujiamini kwake ni sehemu kubwa katika nguvu yake na ameweza kuitumia vema katika kueleza nia yake wazi ya kuwania uprez. Zaidi alijiongezea umaarufu pale alipoweka wazi azma yake ya kuwa na serikali ya mseto. Sio siri kwamba kila Wazanzibari wengi wamehusiana, kati ya Pemba na Unguja, na ni siasa za wakati huu tu ambazo zinajaribu kuwatenganisha. Kwa wengi wa siasa za kati wanaona Ali anaweza kupunguza joto la sasa la utengano kama si kuliondoa kabisa.

GB, aliandaliwa kuwa rais, hakuwahi kuonyesha nia ya kuwa rais wa visiwa hivyo. Kupitia kuandaliwa huko aliweza kupata ushawishi mkubwa kwa wengi waliopendelea kuendeleza yale yote ya awamu ya Tano.

Hii inamfanya kutokuwa na mvuto na ushawishi kwa wengi wa mjini na maeneo mengine ambayo kwa waliona kutengwa kwa wazi kwa wakati wote wa Awamu ya Tano.

Fani yake ya kitaaluma, imezusha maswali mengi kwa wananchi kama kweli anaziweza siasa za hapo. Na inazidi kuchangiwa na tabia yake ya ukimya ambayo sio tabia maarufu katika siasa za visiwani humo.
 
kwneye siasa kuna mbinu nyingi sana ...hilo nalo neno na ni mbinu kali kweli............
''usawa hauopatikani kwa mzani kuwa sawa ....inategemea na mpimaji mweneywe'
 
1995 mbona alikubali kumwachia Komandoo! GB atulize game kwani 2000-10 ni zamu ya watu wa mjini...
Jamaa namuona hivi anataka kumgeukia GB awali ilikubaliwa siku ile ya "mapinduzi daima" kule Dodoma kuwa GB amwachie karume amalize, maana urais hauna formula kwa CCM, hata mtu akivurunda temu moja atapewa na nyengine ya kuvuruga kabisa, sasa nashangaa anamsukuma sukuma Nahodha(maana hizi futari za huku Dar ndo kwanza nizione mara hii kwa Nahodha) wakati huo huo anapima pumzi za ndugu yake Ali Karume, hatujuwi anataka kuelekea wapi, kibunango naona chama chako kinaelekea kushoto, wagombea wote naona weupeeee(hawawezi kusimama na Hamadi) labda Bilali anaweza akaambulia kura mbili tatu.
 
Duh! GB akisimamishwa na Maalim, atatolewa nishai vibaya sana, sema huko Zenj watu hawachagui mtu bali wanachagua chama. Nahodha katika miaka hii mitano ya mwisho amekuwa akijiweka sawa kuchukua uprezi, ingawa naona bado hafai kuongoza visiwa hivyo, kwani maamuzi mengi ya kwake yanatokana na ushauri wa kwenye maskani!

Aman Karume alishamtosa Ali tokea wakati ule Ali alipotaka kugombea Uprez wa JMT. Hivyo anaweza kuweka nguvu zake kwa Nahodha. Na akifanya hivyo atakuwa amechemsha big time.

CUF wanamuofia zaidi Ali, na wanatumia njia mbalimbali za kumpaka matope ili asichaguliwe kugombea, kwani ndie atakayeweza kusimama kiushindi dhidi ya Maalim. Ali akisimamishwa uwezekano wa CCM kupata majimbo kadhaa kule Pemba ni mkubwa sana, aidha CUF hawataambulia jimbo lolote pale Unguja.
 
Mkimchagua mtu asiyekuwa GB mjuwe Maalim atashinda kwa kishindo kikubwa sana, hakutakuwa na kufungana wala vp, GB ndo peke yake atakaye kubali kushindwa na Maalim waliobaki naona mgongo wa "kidodoma dodoma" tu ndo wanaoutegemea, wengine wameamua hata kutafuta wachuchu huko huko "idodomya", kina Nahodha nao watu wao wanakufa njaa huko Mwera na Makunduchi wamepiga kambi Dar wanawalisha wenye shibe zao. Hawawi kama GB yeye cool tu bongo na hategemei saaaaana mgongo wa "kidodoma" anajuwa ndo wachawi wake nguvu yake kubwa ipo zanzibar na na huko bara UWT na kinara wao Asha Bakari Makame wameshafunika kila kitu, umoja wa vijana anajipendekeza "Msakatonge" kuna Masauni kule zanzibar ambaye kesha vutwa "kidombo" kwa komandoo kupewa sera, huwenda akaukwaa uwaziri katika serikali ya GB, Vuai usisema yy mtu wa Salimini kwa hiyo kura yake na domo lake linajuulikana litapayukiya wapi.
Kibunango upo!
Usione GB kanyamaza muda huu ukafikiri hakutokoti, noooooo jamaa keshajenga ngome tokea siku ile aliyoambiwa "Mapinduziiiiiiiiiii.........."
 
Back
Top Bottom