Rais Kagame aishutumu Tanzania

Here he comes again. Ajaribu kuitikisa Tanzania atakiona kilichomnyoa Khanga mayonya. Sasa hivi watu wanatafuta kitu cha ku-divert attention na yeye anataka kuwapa excuse. ................
Usijidanganye Bongolander, Tanzania ya hivyo haipo sasa hivi. Mungu aepushie mbali nchi hii ilivyosambaratika na maufisadi, uzembe,kununua silaha fake na kukosa uzalendo kuingia vitani. Kama vita vya ndani kupigana na ufisadi na rushwa viongozi wanafanya usanii vya risasi tutaweza?
 
Nadhani huyu bwana ya kwake yamemshinda anaamua kutafuta visingizio. Anapaswa kukumbuka kuwa RPF iliingia madarakani kwa mdomo wa bunduki so hilo litazidi kumwandama katika utawala wake na amani itakuwa ngumu kupatikana kwake ilizingatiwa kuwa wanaoshitakiwa kwa mauaji ni Wahutu tu na hii inatufanya tujiulize kuwa je ni wahutu tu ndo walishiriki mauaji ya halaiki? na watutsi hawakuhusika hata kidogo? kwa mwendo huu EAC ni yaleyale ya enzi za kina Amin haitaweza kusimama!
 
Tukumbuke kuwa 85% ya watu wa Rwanda ni Wahutu!Kagame ni mtusi,na hawa wamedestabilise Congo,hata Uganda ya sasa(Mkumbuke na ye Mu7 anasili ya huko).
One man one vote,Kagame hawezi kushinda kihalali.

Hizi ni facts tuzijue!
inachekesha eti alishinda ule uchaguzi kwa 97%
icon10.gif
 
This guy is just a fool, don waste your time discussing him.
He eliminates everyone who thinks with brain amebakiza ndio bwana. Huyu Kayumba was an excellent general but look.
As for threatening Tanzania, he did not refer to the country specifically, he said govts in the region. In any case licha ya ufusadi wetu, hawezi kutuingia. Na ujue bandari anaitegemea mfuta ya kuendesha vifaru yatapita wapi. It was just kutapatapa kwa lunatic huyu.
 
inachekesha eti alishinda ule uchaguzi kwa 97%
icon10.gif
Babu ni kweli lakini kulikuwepo na vitisho chinichini kwa wananchi ndo maana wengine hawakwenda kupiga kura na hata walopiga kura walikuwa wanaogopa sana. Yote tisa, kumi huyu jamaa ni kiboko kwa viongozi wazembe nchini kwake manake wengi anawalazimisha kujiuzuru wakileta uzembe!
 
Hata kama tuna matatizo yetu ya Ndani,nitaweka itikana za vyama pembeni

Huyu asituletee udikteta wake,we are not going to buy his political insanity!

Mbona yeye aliingilia huko DRC,anadhani yeye ni nani?Damn!
 
Babu ni kweli lakini kulikuwepo na vitisho chinichini kwa wananchi ndo maana wengine hawakwenda kupiga kura na hata walopiga kura walikuwa wanaogopa sana. Yote tisa, kumi huyu jamaa ni kiboko kwa viongozi wazembe nchini kwake manake wengi anawalazimisha kujiuzuru wakileta uzembe!
yaah hapo umesema,swala la rushwa na utendaji huyu bwana kakomesha,yaani hapo lazima tumsifu,ufisadi hamna kule.
 
5th March 10

Rais Kagame aishutumu Tanzania

Mwandishi Wetu

Rais Paul Kagame wa Rwanda ameituhumu Tanzania kwamba inaruhusu watu wanaoipinga Serikali yake kuendeleza harakati za kuhujumu nchi hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Kigali juzi na taarifa zake kutangazwa na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC), Kagame alisema atawasiliana na Tanzania ili watu hao wanaoendesha harakati hizo wakamatwe.

Mbali na Tanzania, Kagame pia aliitaja Kenya na Uganda kwamba kuna watu kama hao wanaoendesha harakati dhidi ya serikali yake, lakini akaapa kwamba kamwe hawataweza kuiangusha serikali yake.

Katika mkutano huo, Kagame pia alimshambulia mshirika wake wa zamani wakati wa mapambano ya kuikomboa Rwanda, Luteni Jenerali Kayumba Nyamwasa ambaye alikuwa balozi wa nchi hiyo nchini India kwamba ni miongoni mwa watu wanaoendesha chokochoko dhidi ya serikali yake.

Alisema Kayumba ambaye alivuliwa ubalozi hivi karibuni na sasa amekimbilia Afrika Kusini kuomba ukimbizi wa kisiasa, kuwa wamekuwa na mawasiliano na aliyekuwa mkuu wa mambo ya usalama Luteni Jenerali Patrick Kalegeya katika mipango yao ya kuhujumu Rwanda.

Majenerali hao wote walikuwa washirika wa Kagame lakini sasa wamekimbia nchi kutokana na kutofautiana na Rais huyo huku wakimtuhumu kwa kuendesha nchi kidikteta.

Alimtaja Kayumba kwamba alihusika na mashambulizi ya maroketi jijini Kigali hivi karibuni na kwamba ataiomba Afrika Kusini kumrejesha nyumbani kwa ajili ya kujibu tuhuma zinazomkabili.

Akijibu tuhuma dhidi yake, Jenerali Kayumba alisema kwamba Rwanda inazidi kuzama katika utawala wa kidikteta na kumtaja Rais Kagame kama mtu asiyetaka kukosolewa na yeyote.

Jenerali Kayumba ambaye amekwisha kupata hifadhi ya ukimbizi wa kisiasa Afrika Kusini, alisema Rais huyu anataka watu wa kumlamba miguu kumzunguka lakini si watu wanaoweza kutoa mawazo yao.

“Madaraka yasiyokuwa na mipaka huporomoka vivyo hivyo, nchi haiwezi kuendeshwa na mawazo ya mtu mmoja tu huku akipingana na wale wenye mawazo tofauti,” alisema Jenerali Kayumba.

Kadhalika, Jenerali Kayumba alikanusha vikali kuhusika na mashambulizi ya Kigali ya hivi karibuni na kusema yalipangwa na serikali ya Kagame mwenyewe kwa nia ya kuwapakazia watu asiowataka.

Rais Kagame alisema Mwendesha Mshitaka Mkuu wa Serikali, Martin Ngoga, hivi karibuni aliwataja Jenerali Kayumba na Jenerali Karegeya kuwa ndio waliopanga mashambulizi hayo.

Wakati Wanyarwanda wakilumbana kuhusu mashambulizi ya Kigali ya hivi karibuni, Nipashe iliwasiliana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, juu ya Tanzania kutuhumiwa na Rwanda, lakini alisema yuko safarini Cairo, Misri.

Hata hivyo, alisema kwamba bado serikali hajaipata taarifa rasmi za malalamiko ya Rais Kagame ili iyatazame na kuyatolea tamko.

Hata hivyo, Membe alisema Tanzania wakati wote imesema wazi kwamba haifanyi wala kuunga mkono kitendo chochote cha kuhujumu nchi jirani katika ardhi yake.

Membe alisema Tanzania ilikwisha kutoa msimamo wake wakati taarifa za kuhujumiwa kwa Rwanda zilipotolewa na maofisa wa Umoja wa Mataifa na kuitaja serikali kusaidia waasi wa Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), kwa kusisitiza kwamba imejitolea kwa nguvu zake kuhakikisha kwamba amani inarejea katika ukanda wa Maziwa Makuu.

“Ni jambo lisiloingia akilini kusema kwamba Serikali ya Tanzania inaweza kupanga mkakati au kutoa msaada kwa kikundi chochote kinachokusudia kuvuruga amani katika ukanda huu,” alisema Membe ambaye aliahidi kutoa taarifa zaidi akishawasiliana na ofisi yake.

NIPASHE
alivyokuwa **** huyu dikteta hachelewi kusema ni JF inampinga.
 
Tutsi's are damn intelligent, nimesoma nao undergraudate, wapo so bright na focused, (the likes of Waisrael) kwa nchi yao. So far so gud, Kagame has done great kwa nchi yake although ana makosa ya hapa na pale kama binadamu. My take is that, kwa nchi kama Rwanda ambayo ime-progress frm myriads of coup de tat na genocide, absolutely democracy cant be the best way forward, mda fulani unahitaji a kind of u-dictator ili kuwa-push watu.
Although namuona Kgm anajichimbia kaburi lake taaratibuu, hawa ma-Generals wengi kwenda exile, he should nt take it for granted, one day watarudi, na yale ya '94 yatakuwa madogo. Ajitahidi hata kuwafanyia toppling/indirect obstraction, mfano; awape hata Ukuu wa mikoa kule kwao, au lah, unsound wizara's.....Binadamu ni kama maji, huwezi kuyazuia, yatachimba tu!

BTW; At least ths time Membe kajibu vzuri tuhuma hizo, Lol!!, manake bingwa wa kukurupuka na majibu yake yule Chinga Lol!
 
the next time revenge itakuwa mbaya sana mkuu,kuanzia hao mageneral waliokimbia na wahutu ndio wana hasira na jamaa na kabila yake yote,na safari hii wameapa kutoacha mtusi yeyote suvival,na yote inatokana na kagame,jamaa amewafanya watu wake wachukiwe zaidi.
 
Wakati wa Kagame kuachia ngazi umefika. Akiendelea kukaa madarakani atavuruga mafanikio yote aliyoiletea Rwanda. Kinachomsumbua ni paranoiya inayotokana na mikono yake kujaa damu nyingi tokea alipoitungua ile ndege ya Habyarimana.

Yeye bado ni kijana akitaka azeeke vizuri na kwa usalama, basi inabidi ajitahidi aachie ngazi wakati mambo ni mazuri. Akichelewa yakaharibika sio ajabu akawindwa kama wengine ili na yeye ajibu mashitaka ya mauaji aliyoamrisha.
 
thubutuu,aachie ngazi geneva court inamsubiri,usijeshangaa akakaa madarakani maisha,maana anajua akichomoka tu wanaye.
 
..ikianzishwa Mahakama ya Mauaji ya Congo sidhani kama Kagame na washirika wake watasalimika.

..halafu Kagame amemhifadhi Jenerali Nkunda muasi wa Congo halafu analalamika kwamba kuna nchi majirani zinahifadhi waasi wa Rwanda.

..ili eneo hili la maziwa makuu litulie inabidi Rwanda iongozwe na Raisi asiyekuwa na historia ya kijeshi-jeshi.

..Kagame anapaswa kung'atuka akajibu kesi za DRC genocide.
 
Kwa hiyo sisi tusupport hayo madudu, ili wachapane af warudi tena hapa maelfu as refugees? Atoe boriti kwenye jicho lake kwanza kabla ya kuonyesha vibanzi kwenye macho ya wengine
 
doubt kama kagame au Kikwete wanafikiria mnavyofikiria nyie,yaani mnajidai mnaelewa kumbe utumbo mtupu!
 
Jamani haya mambo wakati mwingine ni magumu siyo rahisi rahisi...
Unaweza ukute kuna kikundi cha watu nadani ya serikali yetu kinalipwa kifisadi na watu fulani wenye maslahi yao kwa Kagame japo siyo rasmi, kwa Kagame yeye ataona ni Tanzania tu kwa ujumla. Msisahau kashfa ya Tz kuwapitishia silaha waasi wa DRC?

Sure. Let's not just jump into the bandwagon of full denial without having full info. Bado hatuwezi kujua kama aliyosema Kagame si ya kweli au ni ya kweli.
Serikali yetu, tena hii ya sasa ya watu wa RA siyo malaika ambao hawawezi kufanya mambo fulanifulani.

Kumbukeni kashfa ya kusafirisha silaha kwenda DR Congo na uhusiano wake na Mapanki ya Ziwa Victoria. Kikwete alitoa hotuba ya kukanusha kuwa masuala hayo yapo, na mwandishi aliyefuatana na mzungu aliyepiga picha za documentary hiyo alisumbuliwa sana na vyombo vya dola kuwa wamezusha mambo hayo ya silaha na mapanki.

Ila hatimaye penye ukweli uongo ulijitenga. Hatimaye ikafahamika kuwa yaliyoelezwa kwenye documentary ni ya kweli na kuwa JK alikanusha kitu cha ukweli.

Serikali hii mhhh... lolote linawezekana... ala Silvio Berlusconi...
 
Back
Top Bottom