Jenerali Ulimwengu: Wakosoaji hawamtendei haki Paul Kagame

chiembe

JF-Expert Member
May 16, 2015
12,009
20,684
Jenerali Ulimwengu alitoa kauli hiyo wakati akihojiwa na chombo Cha habari kinachofahamika kwa jina "chanzo". Jenerali Ulimwengu aliunga mkono ukandamizaji demokrasia unaofanyika Rwanda kwa kisingizio Cha mauaji ya kimbati, ambayo hata hivyo yametokea miaka karibu thelasini Sasa.

Kagame amejaza maelfu ya wanasiasa na wanaharakati wa haki za binadamu katika magereza ya Rwanda, na mara kadhaa amejiongezea muda wa urais, Jenerali Ulimwengu aliunga mkono Kagame kuongezea mihula ya Urais.

Hapa watanzania tuna mambo ya kujiuliza, si huyu Jenerali juzijuzi tu alimpinga JPM kwa udikteta? Leo upande wa pili anauunga mkono unapofanywa na Kagame!

Ni huyuhuyu Jenerali Ulimwengu alimpinga JPM kuongeza muda wa urais, Leo anaunga mkono Kagame kujiongezea muda wa urais.

Ni huyu Jenerali Ulimwengu aliyepinga JPM kufungia shughuli za kisiasa kwa sababu za maendeleo, Leo anaunga mkono Rwanda kuminya demokrasia kwa sababu PAKA analeta maendeleo.

Ni huyu huyu Jenerali aliyepinga kelele kutwa kucha wakati JPM amepunguza Uhuru wa demokrasia, na kuweka watu magereza. Leo anaunga mkono wanadamu, hata kama ni wanyarwanda, wa asili ya wahutu(sijui kwa nini anaona ni sawa Kagame akawafunga) kuwekwa gerezani.

Ni moja kati ya mahojiano ambayo Jenerali Ulimwengu alikuwa anajibu maswali akionekana anakwepa kamera, hakuwa comfortable, hasa alipokiri kwamba Kagame ni rafiki yake mkubwa sana, na muda wote akimuhitaji anaongea naye. Katika mada zake kuhusu Tanzania, Jenerali Ulimwengu amekuwa akiikashifu Tanzania na kuitusi, na hajafanya hivyo kwa nchi yake ya asili. Katika mahojiano, mara zote aliisifia.

Jenerali Ulimwengu anapokuwa katika vikao vya chama chake Cha Chadema, huwa anawaeleza kwamba anapinga udikteta, na kwamba yeye ni mnazi wa demokrasia.

Wakati wa Mkapa, vyombo vya dola vilifumua taarifa kwamba Jenerali ni mnyarwanda, hivyo si raia, na alipata kashkash nyingi sana.

Ni vyema watanzania tukawa makini, tuilinde sana nchi yetu. Kuna watu Wana pa kwenda. Baadhi watoto wao Wana uraia wa U.S.A, na nchi mbalimbali, na wanalindwa na taasisi za kiinteljensia za nchi hizo. Wengine wanapewa mitaji kufungua magazeti kuyumbisha nchi.
Screenshot_20230804-154552.jpg
 
Kisingizio cha mauaji ya kimbari alichotoa Ulimwengu kina mantiki au hakina? na hata kama hayo mauaji yalitokea miaka thelathini iliyopita, je, hayawezi kutokea tena kama Rwanda wakichezea amani waliyonayo?

Wewe ni mjinga, mwenye fikra na upeo finyu, uliyezoea kushangilia ujinga wanaofanya CCM na serikali yao kila siku, ujinga ambao unaweza kuwa chanzo cha kuvuruga amani tuliyonayo kwa sasa, kwako sio rahisi kuelewa mantiki ya alichomaanisha Jenerali Ulimwengu.

Upuuzi kama ule wa kutoa bandari zetu zote kwa mwarabu milele, unaweza kuwa chanzo kikuu cha kuvuruga amani yetu, hasa pale watanganyika watakapoamua kutumia njia tofauti kudai haki ya kurejeshewa bandari zao walizoporwa na kiongozi msaliti aliyepo kwa sasa.
 
Kama ikitokea, chanzo kitakuwa ujinga wa mtawala kutoa bure bandari zetu kwa wajomba zake milele.
Sio kwa waTanzania Hawa!! Watu wako busy na Simba day kuliko hata masuala serious. Si juzi tu hapa mlikua mnatoka povu kuhusu ripoti ya CAG leo hii hakuna anayefuatilia lolote sio wananchi sio jamii forums. Hii ndio Tanzania ya wajinga hata hili litapita na maisha yataendelea..
 
Sio kwa waTanzania Hawa!! Watu wako busy na Simba day kuliko hata masuala serious. Si juzi tu hapa mlikua mnatoka povu kuhusu ripoti ya CAG leo hii hakuna anayefuatilia lolote sio wananchi sio jamii forums. Hii ndio Tanzania ya wajinga hata hili litapita na maisha yataendelea..
Kesi iko mahakamani na movement nyingine zinaendelea kisha unasema litapita!, au ndio unaomba lipite kwasababu hujawahi kusema chochote kuhusu unyama waliofanyiwa watanganyika?

Usiishi kwa kukariri, jana sio leo, na leo haitakuwa kesho. Wewe endelea kuvizia tu na siasa zako, nini na wapi useme, pengine unaacha, sisi wengine tunasema pote penye kero za watanganyika.
 
na hao ndiyo waliopora kibabe bandari zetu na siyo sijui mwarabu gani wa Dubai mnadanganywa tu, Bandari imeenda Rwanda …
 
Kama kweli unawapenda Wanyarwanda, basi lazima umwombee Paul Kagame aendelee kuwa na Afya njema ili aendelee kuwaongoza hata kwa miaka 20 hivi mbele!
 
Kesi iko mahakamani
Kesi ya CAG ipo mahakamani? Si mlisema kitanuka unless waliotajwa kwenye ripoti watakamatwa ghafla imekuja issue ya DP world mmepoa, soon mtasikia Feisal kahamia Simba mnasahau Dp world. Hao ndio waTanzania hayupo serious ni mihemko tu.
sisi wengine tunasema pote penye kero za watanganyika.
Hahahaha acha utani mkuu, hivi issue ya loliondo mliishia wapi? Hivi Kuna anayekumbuka kweli? Mind you watu wamesahau mambo ya Tozo na kelele za bando!! Hao hao wamesahau ripoti ya CAG

Niamini mimi kufikia December Hawa waTanganyika wapenda ngono na simbaYanga watakua busy na kufuatilia Bongo movie sio issue ya DP world.

Tuwe serious tuache mihemko otherwise CCM itaendelea kutuburuza
 
Inanikumbusha msemo "Success has many fathers , failure has none"

Namuelewa Ulimwengu lakni jamaa ni mnafiki..mbona namba 5 alikuwa anamsema Sana...ili sisi waAfrika ndio tulivyo we like results but not really invested in the journey toward the results
 
Back
Top Bottom