Rais Dkt. Mwinyi akutana na Balozi wa Saudia Arabia - Tanzania

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Sep 6, 2020
741
479
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi ameipongeza Serikali ya Saudi Arabia kwa jitihada kubwa wanayoitoa Tanzania kuungamkono miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo sekta ya Afya, maji, miundombinu ya barabara na kusaidia uzalishaji umeme.

Rais Dk. Mwinyi amesema hayo alipozungumza na Balozi wa Saudia Arabia nchini Tanzania Mhe.Yahya Ahmed Okeish na ujumbe wake Ikulu Zanzibar tarehe 8 Desemba, 2023

Aidha Rais Dk. Mwinyi aliikaribisha Serikali ya Saudia Arabia kuwekeza kwenye shamba la Makurunge, Bagamoyo linalomilikiwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, ambalo linafaa kwa uwekezaji wa kilimo,uvuvi na utalii.

Kwa upande mwingine Rais Dk. Mwinyi aliipongeza timu ya Madaktari 21 kutoka Saudia Arabia waliojitolea kuweka kambi ya matibabu na upasuaji jimbo la Gando, Mkoa wa Kaskazini Pemba.
IMG-20231208-WA0016.jpg
IMG-20231208-WA0013.jpg
IMG-20231208-WA0014.jpg
IMG-20231208-WA0015.jpg
IMG-20231208-WA0012.jpg
 
Back
Top Bottom