Taarifa ya ikilu inasema, Mh. rais amamteua bi Amina Said Mrisho kuwa kamishna wa sensa mwaka 2012, ambae kabla ya hapo alikuwa mkuu wa mkoa wa pwani. uteuzi huu unaanza mara moja. Vile vile amemteua bibi Seraphia R. Mghembe kuwa mratibu wa mpango wa kurasimisha rasilimali na biashara za wanyonge Tanzania (MKURABITA), kabla ya uteuzi huu alikuwa mkurugenzi wa fedha na utawala wa MKURABITA. uteuzi huu unaanza mara moja.
nawapongeza wote.wanastahili, bora mzee salema kastaafu ana visa tangu akiwa TASAF alipoondoka walishangalia na kufanya sherehe wkt mkapa alipomteuwa kwenda Mkurabita.
kwa huo mradi sijaona bado umuhimu wake zaidi ya kula hela na kusafiri,kukaa vikao kila mara,bora hata Bi amina na kitengo chake
Inaonekana kama ukamishina unahitaji umri mkubwa au? Sijui kigezo gani kimetumika kuwateua hawa maana yake taarifa haisemi kuhusu hilo? Anyway hii ndo Tz kila kitu ndivyosivyo. Licha ya hayo ahsante kwa kutujuza.
Kuna mzee mmoja yupo pale NBS (Ofisi ya Takwimu Taifa) alinisimulia kuwa huyu mama ana Shahada ya kwanza ya TAKWIMU then Masters in IT, amefanya kazi NBS muda mrefu na ana uzoefu wa kutosha. Pia alishawahi fanya kazi BoT kisha akaingia kwenye siasa.
Zaidi ya hayo alitoa mchango mkubwa katika kuandaa/kutengeneza(design) Database ya Sensa ya 2002, hivyo uteuzi wake naamini ni sahihi ukizingatia uzoefu alionao.
KAMA KUNA (ANA) MENGINE NYUMA YA PAZIA, NASHAURI AACHE badala yake atekeleze jukumu la Sensa kwa ufanisi.
Nawasilisha.
Nikisema JK ni mdini nitakuwa nimekosea?
huyu mama iringa si ilimshinda mpaka wakati fulani kukawa na ziara ya JK , akaugua kwa kuogopa kuumbuliwa?
Kabla ya huyu mama kuwa mkuu wa mkoa Iringa alikuwepo mama mwingine Halima Kasungu yeye ameishia wapi siku hizi? Alikuwa jasiri sana na alichapa sana kazi alipokuwa D.C. Njombe.
Hii nafasi ingetangazwa watu waombe,na kwa jambo nyeti kama sensa kunatakiwa kuwe na kamisheni ya wataalamu ambao wangeomba hiyo kazi ,matokea ya kupeana kazi kwa kujuana mwisho wake ndio tunasikia mkoa wa Lindi una watu wengi kuliko Shinyanga,Hii nchi ni ya ajabu sana,yaani hata kitengo kama hiko kinapata bosi wake kwa kuteuliwa tena na raisi.Haya madaraka ya raisi kufanya kila kitu sidhani kama yatatufikisha.Yaani tuna haja ya kufanya mabadiliko makubwa sana kwenye katiba mpya,huu ****** wa kusubiri raisi ateue mpaka mfagizi wa ikulu sijui kama tutafika.Nilitegemea kitengo kama hiki kipate msomi fulani wa population...may be huyu mama nae ni msomi huko,ila sina uhakika kabisa.
waKuna mtu kanidokeza kuwa Amina ni mtaalam aliyebobea wa Takwimu na kwa vipindi tofauti amekuwa akishirikishwa katika hatua muhimu za Census. Sasa amepata shavu rasmi.
Poa kabisa huyu mama Mrisho hana uhusiano wa kidugu na JK na wala hakuteuliwa kimbumbumbu. Kabla ya kuingia kwenye siasa za ukuu wa wilaya na mkoa alikuwa kwenye kitengo hichi (sina uhakika kama mkurugenzi kamili au msaidizi)
Yeye ni statistician na ni muelewa sana wa fani hiyo.