Rais amteua Bi Amina Said Mrisho kuwa Kamishna wa Sensa ya Mwaka 2012

Huyu mama kwa kweli ni mtaalamu wa mambo ya takwimu. Na pia ana uzoefu sn wa masuala ya ICT. Mimi naona anafaa sn ktk nafasi hii!
 
Taarifa ya ikilu inasema, Mh. rais amamteua bi Amina Said Mrisho kuwa kamishna wa sensa mwaka 2012, ambae kabla ya hapo alikuwa mkuu wa mkoa wa pwani. uteuzi huu unaanza mara moja. Vile vile amemteua bibi Seraphia R. Mghembe kuwa mratibu wa mpango wa kurasimisha rasilimali na biashara za wanyonge Tanzania (MKURABITA), kabla ya uteuzi huu alikuwa mkurugenzi wa fedha na utawala wa MKURABITA. uteuzi huu unaanza mara moja.
 
Taarifa ya ikilu inasema, Mh. rais amamteua bi Amina Said Mrisho kuwa kamishna wa sensa mwaka 2012, ambae kabla ya hapo alikuwa mkuu wa mkoa wa pwani. uteuzi huu unaanza mara moja. Vile vile amemteua bibi Seraphia R. Mghembe kuwa mratibu wa mpango wa kurasimisha rasilimali na biashara za wanyonge Tanzania (MKURABITA), kabla ya uteuzi huu alikuwa mkurugenzi wa fedha na utawala wa MKURABITA. uteuzi huu unaanza mara moja.

Jamani naomba kusaidiwa nini maana halisi ya wanyonge na hao wanyonge walifanya lini biashara wakapata rasilimali ambazo sasa zinarasimishwa. Hizo mali zina thamani gani. Kwa anaejua tafadhari. kwa sababu utitili wa hizi taasisi za serikali unanichanganya
 
huyu mama iringa si ilimshinda mpaka wakati fulani kukawa na ziara ya JK , akaugua kwa kuogopa kuumbuliwa?
 
nawapongeza wote.wanastahili, bora mzee salema kastaafu ana visa tangu akiwa TASAF alipoondoka walishangalia na kufanya sherehe wkt mkapa alipomteuwa kwenda Mkurabita.
kwa huo mradi sijaona bado umuhimu wake zaidi ya kula hela na kusafiri,kukaa vikao kila mara,bora hata Bi amina na kitengo chake

Wewe hujui lolote kuhusiana na MKURABITA nenda kwenye website yake upate taarifa ya nini walichokifanya.
 
Inaonekana kama ukamishina unahitaji umri mkubwa au? Sijui kigezo gani kimetumika kuwateua hawa maana yake taarifa haisemi kuhusu hilo? Anyway hii ndo Tz kila kitu ndivyosivyo. Licha ya hayo ahsante kwa kutujuza.

Mkuu huyo mama ni mtaalamu kinoma kwenye mambo ya takwimu. Kuhusu undugu na ******, kwa kweli hawana. Huyu mama kwao ni kiteto, ni mguu huyo mama, ukifika pale kibaya ndo ukoo wake ulipo. Kaka yake ni mwenyekiti wa ccm wilaya ya kiteto na ni kiongozi wa chama cha ushirika pale wilayani kinachoitwa Kaloleni!
 
Kuna mzee mmoja yupo pale NBS (Ofisi ya Takwimu Taifa) alinisimulia kuwa huyu mama ana Shahada ya kwanza ya TAKWIMU then Masters in IT, amefanya kazi NBS muda mrefu na ana uzoefu wa kutosha. Pia alishawahi fanya kazi BoT kisha akaingia kwenye siasa.
Zaidi ya hayo alitoa mchango mkubwa katika kuandaa/kutengeneza(design) Database ya Sensa ya 2002, hivyo uteuzi wake naamini ni sahihi ukizingatia uzoefu alionao.
KAMA KUNA (ANA) MENGINE NYUMA YA PAZIA, NASHAURI AACHE badala yake atekeleze jukumu la Sensa kwa ufanisi.
Nawasilisha.

Mimi sina tatizo kabisa na uwezo na qualification za mama Amina Mrisho. Tatizo langu ni madaraka makubwa ya RAIS kuteuwa hata Wakurugenzi wa sensa? Huyu RAIS ni Mungu? Leo hii kama hiyo post ingetangazwa na watu waka apply kwa qulification zao wakawa interviwed tusingeongea haya yote.

Jamani tuangalie sana kwenye katiba mpya, haya madaraka ya RAIS is too much. Siku ikatokea tukampata dictator tutakwisha. BTW, JK sio dictator, a weak leader is different with a dictator.
 
Nikisema JK ni mdini nitakuwa nimekosea?

Kama huna la kuchangia soma hata comments walizoandika wenzako badala ya kuropoka,udini maana yake nini..au akichaguliwa au kuteuliwa muislam kushika nafasi ndio udini,.! Unaposema udini maana yake nini? Au ndio kuleta uchochezi usiokuwa na tija hapa! Yaani watu wengine sijui waliumbwa kwa nuru ya moto!
 
Kumekuwa na wimbi kubwa sana la mauaji ya raia hapa Songea hasa watoto, ambapo hadi sasa zaidi ya watu 12 wameripotiwa kufa.
RPC akiulizwa kuhusu hali hiyuo anasema nimambo ya Mapenzi bt hadi watoto, na hata kama nimapenzi kwanini wasichukue hatua?
Imefikia hatua wananchi wameandamana kwenda kwenye kituo kikuu cha Polisi Songea kushinikiza serikali ichukue hatua lakini hakuna kinachoendelea zaidi ya kuambulia mabomu.
Je Polisi wanahusika katika mauaji hayo?
 
huyu mama iringa si ilimshinda mpaka wakati fulani kukawa na ziara ya JK , akaugua kwa kuogopa kuumbuliwa?

Kabla ya huyu mama kuwa mkuu wa mkoa Iringa alikuwepo mama mwingine Halima Kasungu yeye ameishia wapi siku hizi? Alikuwa jasiri sana na alichapa sana kazi alipokuwa D.C. Njombe.
 
Kabla ya huyu mama kuwa mkuu wa mkoa Iringa alikuwepo mama mwingine Halima Kasungu yeye ameishia wapi siku hizi? Alikuwa jasiri sana na alichapa sana kazi alipokuwa D.C. Njombe.

Kama sijakosea mama Halima Kasungu kabla ya kuwa mkuu wa mkoa ,aliwahi kuwa kwenye tume ya Warioba iliyokuwa inahusika na uzuiwaji wa rushwa enzi ya Rais Mkapa; utendaji wake sidhani kama angeendana na hii serikali iliyopo sasa kwani alikuwa ni muadilifu sana hivyo ilibidi apumzike!!!.
 
Hii nchi ni ya ajabu sana,yaani hata kitengo kama hiko kinapata bosi wake kwa kuteuliwa tena na raisi.Haya madaraka ya raisi kufanya kila kitu sidhani kama yatatufikisha.Yaani tuna haja ya kufanya mabadiliko makubwa sana kwenye katiba mpya,huu ****** wa kusubiri raisi ateue mpaka mfagizi wa ikulu sijui kama tutafika.Nilitegemea kitengo kama hiki kipate msomi fulani wa population...may be huyu mama nae ni msomi huko,ila sina uhakika kabisa.
Hii nafasi ingetangazwa watu waombe,na kwa jambo nyeti kama sensa kunatakiwa kuwe na kamisheni ya wataalamu ambao wangeomba hiyo kazi ,matokea ya kupeana kazi kwa kujuana mwisho wake ndio tunasikia mkoa wa Lindi una watu wengi kuliko Shinyanga,
 
Kuna mtu kanidokeza kuwa Amina ni mtaalam aliyebobea wa Takwimu na kwa vipindi tofauti amekuwa akishirikishwa katika hatua muhimu za Census. Sasa amepata shavu rasmi.
wa

Kwa hili nakuunga mkono kwani mama huyu mimi namfahamu vyema!! Watu watasema mengi ila kwa kazi hii hakuna anaemshinda Bi Amina. Mi Mtakwimu, Mtaalamu wa Komputa na mwana hisabati. sasa mtamkamatia wapi? Hii ni sensa yake ya tatu kushiriki katika uchambuzi. Muwe mnatafuta CV za watu sahihi na ni bora mkawahoji wenyewe.
 
Poa kabisa huyu mama Mrisho hana uhusiano wa kidugu na JK na wala hakuteuliwa kimbumbumbu. Kabla ya kuingia kwenye siasa za ukuu wa wilaya na mkoa alikuwa kwenye kitengo hichi (sina uhakika kama mkurugenzi kamili au msaidizi)

Yeye ni statistician na ni muelewa sana wa fani hiyo.


Hana habari huyo anaamua kuropoka tuu kwa kutokujua. Habari ndio hiyo na mwenzio ameshaula!
 
Pinda anahusika na akaamua kumuweka mtu wake aitwaye Paul Kimiti ili wale vizuri na JK akaiona hiyo akamtosa ila bado hajakubali sijui itakuwaje. Tusubiri tuone!
 
Back
Top Bottom