Rais amteua Bi Amina Said Mrisho kuwa Kamishna wa Sensa ya Mwaka 2012

Invisible

Robot
Feb 11, 2006
9,075
7,878
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bibi Amina Saidi Mrisho kuwa Kamishna wa Sensa ya Mwaka 2012.

Aidha, Rais Kikwete amemteua Bibi Seraphia R. Mgembe kuwa Mratibu wa Mpango wa Kurasimisha Raslimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA).

Taarifa iliyotolewa na kutiwa saini Dar es Salaam leo, Jumanne, Februari 21, 2012, na Kaimu Katibu Kiongozi, Bwana Peniel Lyimo imesema kuwa uteuzi huo umeanza jana, Februari 20, mwaka huu, 2012.

Taarifa ya Bwana Lyimo imesema kuwa kabla ya uteuzi wake, Bibi Amina Mrisho alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani.

Katika taarifa tofauti iliyotolewa na kutiwa saini pia mjini Dar es Salaam leo, Jumanne, Februari 21, 2012, na Katibu Mkuu Ikulu, Bwana Peter Ilomo, imesema kuwa uteuzi huo wa Bibi Mgembe umeanza pia jana, Jumatatu, Februari 20, 2012.

Bwana Ilomo amesema katika taarifa yake kuwa kabla ya uteuzi wake Bibi Mgembe alikuwa Mkurugenzi wa Utawala na Fedha wa MKURABITA.

Bibi Mgembe anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bwana Ladislaus Salema ambaye amestaafu kwa mujibu wa sheria.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
21 Februari, 2012
 
Kwenye siasa watu hawatupani. Mama ametoka ukuu wa mkoa akapumzika kidogo na sasa amepangiwa kazi nyingine!

Bi. Mgembe hongera sana, kaza buti mama. Nakumbuka ile kazi yako ya consultancy naona ilikujenga. Jitahidi uturasimishie mali zetu sisi wanyonge wenzako; usitusahau.
 
Mama Amina ni jembe la ukweli; alitemeshwa ukuu wa mkoa na mafisadi, alisimama kidete na wezi wa fedha za madaraja zilizoibiwa halmashauri ya Bagamoyo, mama hakujua kuwa fedha hizo zilipigwa na watu wazito (Ridhiwani, Celina Kombani)... JK amempa hicho cheo kumnyamazisha lakini mama mzalendo wa ukweli
 
Hongera mama,ni wakati wako sasa kuonyesha kuwa kweli mnaweza kama mkiwezeshwa,namtakia Mh Rais safari njema UK arudi salama usalimini
 
Inaonekana kama ukamishina unahitaji umri mkubwa au? Sijui kigezo gani kimetumika kuwateua hawa maana yake taarifa haisemi kuhusu hilo? Anyway hii ndo Tz kila kitu ndivyosivyo. Licha ya hayo ahsante kwa kutujuza.
 
CV yake kwa kipindi kifupi ni hii
1.DC bukoba
2.RC Tabora
3.RC Pwani
4.Kamisha wa Tume
 
Kuna mtu kanidokeza kuwa Amina ni mtaalam aliyebobea wa Takwimu na kwa vipindi tofauti amekuwa akishirikishwa katika hatua muhimu za Census. Sasa amepata shavu rasmi.
 
Hii nchi ni ya ajabu sana,yaani hata kitengo kama hiko kinapata bosi wake kwa kuteuliwa tena na raisi.Haya madaraka ya raisi kufanya kila kitu sidhani kama yatatufikisha.Yaani tuna haja ya kufanya mabadiliko makubwa sana kwenye katiba mpya,huu ****** wa kusubiri raisi ateue mpaka mfagizi wa ikulu sijui kama tutafika.Nilitegemea kitengo kama hiki kipate msomi fulani wa population...may be huyu mama nae ni msomi huko,ila sina uhakika kabisa.
 
Naona kuna haja raisi akaishia kuteua baraza la mawaziri tuu!Hii ikiwekwa kwa katiba mpya itakuwa njema
 
Hii nchi ni ya ajabu sana,yaani hata kitengo kama hiko kinapata bosi wake kwa kuteuliwa tena na raisi.Haya madaraka ya raisi kufanya kila kitu sidhani kama yatatufikisha.Yaani tuna haja ya kufanya mabadiliko makubwa sana kwenye katiba mpya,huu ****** wa kusubiri raisi ateue mpaka mfagizi wa ikulu sijui kama tutafika.Nilitegemea kitengo kama hiki kipate msomi fulani wa population...may be huyu mama nae ni msomi huko,ila sina uhakika kabisa.

Poa kabisa huyu mama Mrisho hana uhusiano wa kidugu na JK na wala hakuteuliwa kimbumbumbu. Kabla ya kuingia kwenye siasa za ukuu wa wilaya na mkoa alikuwa kwenye kitengo hichi (sina uhakika kama mkurugenzi kamili au msaidizi)

Yeye ni statistician na ni muelewa sana wa fani hiyo.
 
Mama Amina ni jembe la ukweli; alitemeshwa ukuu wa mkoa na mafisadi, alisimama kidete na wezi wa fedha za madaraja zilizoibiwa halmashauri ya Bagamoyo, mama hakujua kuwa fedha hizo zilipigwa na watu wazito (Ridhiwani, Celina Kombani)... JK amempa hicho cheo kumnyamazisha lakini mama mzalendo wa ukweli

sijaelewa..kama hela kala Rizone si alitumwa na babake au?hivi rizone ni waziri au ana cheo gani serikalini? nauliza tu
 
Amina Mrisho, hajawahi kuwa RC Tabora, bali Iringa. Fani yake ni IT na amefanyakazi miaka mingi Takwimu/(census) kabla ya kuingia benki kwa miaka kadhaa na kurudi tena Takwimu, hivyo karudi kwenye utaalamu wake! Hawana ukoo na Mh Rais!
 
Tatizo sio uislamu mbona wapo waislamu majembe mwanzo mwisho hao hawapewi shavu ila wale maamuma ndio wanaojikomba kuvaa mishungi na makanzu wajizungusha kutafuta vyeo na wengi jamaa anao wapa shavu ni vichwa panzi hata kutoka hawawezi
 
kwa nini kila kitu rais,nafasi kama hii si muhimu rais kumteuwa mtu,libidi hii nafasi itangwazwe watu wafanye application,si kila kitu rais tu
 
Mama Amina ni jembe la ukweli; alitemeshwa ukuu wa mkoa na mafisadi, alisimama kidete na wezi wa fedha za madaraja zilizoibiwa halmashauri ya Bagamoyo, mama hakujua kuwa fedha hizo zilipigwa na watu wazito (Ridhiwani, Celina Kombani)... JK amempa hicho cheo kumnyamazisha lakini mama mzalendo wa ukweli

Mkuu hapa utakuwa umechanganya madawa,
Aliyemtemesha kibarua cha ukuu wa mkoa Bi Amina Mrisho ni Raisi Kikwete na aliyemteua kuwa kamishana wa sensa ni huyo huyo Risi Kikwete.
Hao mafisadi waliomtemesha kibarua wameshindwaje kumzuia Kikwete asimteue kamishna wa sensa.
 
mkuu maranya hapo juu,ukuu wa mkoa ni zaidi ya hicho cheo cha sasa,rc ni sawa na rais mkoani,.alikataa kusurrender kwenye ishu ya bagamoyo,alionekana threat,amina alitnfautiana na tamisemi sababu wao walikuwa wanasisitiza hakukuwa na wizi bagamoyo,pinda anahusika na kutemeshwa ukuu wa mkoa..
 
Mama Amina ni jembe la ukweli; alitemeshwa ukuu wa mkoa na mafisadi, alisimama kidete na wezi wa fedha za madaraja zilizoibiwa halmashauri ya Bagamoyo, mama hakujua kuwa fedha hizo zilipigwa na watu wazito (Ridhiwani, Celina Kombani)... JK amempa hicho cheo kumnyamazisha lakini mama mzalendo wa ukweli
Ipo siku atakuja mzalendo wa real Tz ambaye hadanganywi kwa chochote zaidi ya utaratibu na sheria[wasiochakachuliwa]
 
Back
Top Bottom