mwana wa africa
JF-Expert Member
- Apr 17, 2011
- 548
- 128
maamuzi magumu yaliyochukuliwa na cc ya cdm kuwavua uanachama madiwani watano wakaidi ni kielelezo cha dhamira ya kweli ya chama makini kusimamia sheria na taratibu sahihi katika kuiongoza jamii. aidha uamuzi kama huu unaweza kuchukuliwa na baadhi ya watu kama mtaji wa kisiasa kuwatumia madiwani hao wakaidi katika ajenda zao za kutaka kukibomoa au kukiyumbisha chama. kutokana na hali hiyo ni vyema busara zaidi ikatumika kuwapa wananchi hasa wa arusha taarifa sahihi kwa kutumia vikao na mikutano ya hadhara katika kueleza kwa ufasaha na dhamira iliyopelekea maamuzi haya kufikiwa . zaidi sana viongozi, . aidha kwa viangozi wakuu wa cdm (mbowe na timu yake kwa kushirikiana na ofisi ya waziri mkuu kutumia wakati huu kusukuma kwa nguvu zaidi jitihada za kutaka kuleta utengamano wa kisiasa katika jiji hilo ili kumaliza suala hili.