Rafiki yangu alijiua kisa mapenzi

P Didy Wa Tanzania

JF-Expert Member
May 6, 2022
2,376
3,891
Mara nyingi sana huwa nikisikiliza nyimbo ya BUSHOKE na JULIANA KANYOMOZI " usiende mbali ". Huwa anamkumbuka rafiki yangu JAMES mapenzi tu ndo kilikuwa chanzo cha kifo chake.

Jamani tunatakiwa tujue maisha mafupi sana haya lakini kuna mtu anaweza akayafanya yakawa maisha mafupi zaidi kwako

Au unaweza ukaridhika na maisha yako au kipato unachokiingiza kwa siku ila kuna mtu akaja akakufanya ghafla tu usilizike na maisha yako.

Unaweza ukamuona mtu kaingia kwenye ujambazi au anakula unga ukasema aaaah yule nae usela mwingi kajitakia ila leo acha niwapange mambo yanayoendelea kwenye maisha yetu.

Mwana kitu mapenzi kitu kingine kabisa kuna mtu anaweza akaona upuuzi ila nataka niwakumbushe hapa duniani kama utakuwa mwanamke basi utachepuka weeee lakini kuna mwanaume moja utakuwa unamkubali balaa hata kama hana kitu na kwa wanaume hivyo hivyo.

Sasa twende kwenye mada kuu leo jamani nimemkumbuka marehemu rafiki yangu hapa nitatumia jina ambalo sio la kweli ili niwaelezee tu mwana kilimkuta nini ila yote ya yote acha mwana apumzike kwa amani na Mungu ampunguzie adhabu za kabuli uko alipo.

Kwangu mimi alikuwa ni zaidi ya mwana nilihisi ni ndugu kabisa maana alikuwa akipata tatizo mtu wa kwanza kunicheck alikuwa ni mimi.

Kama miaka 8 au 7 hivi iliyopita nyuma James alikuja maghetto ila si unajua mwanangu sana nikimcheck tu najua kabisa kama huyu hayupo sawa.

Nikamuuliza vipi baba upo sawa akaniambia yupo sawa ...aaah mimi nikampotezea nikachukulia ile style labda mwana hajaamka vizuri kumbe sasa mwana ana mawazo kama yote ila kauchuna kimya.

Mimi nilipata story baada ya tukio ambalo sikulitegemea kabisa kutokea kumbe bhana mwanangu James alikuwa na demu anaitwa Aisha mtoto wa chuo alikuwa anasoma pale IFM wakati huo James alikuwa kaishia form 4 tu.

Sasa baadae baada ya James kuuchuna sana akanichana salu eeeh nikamwambia niambie janangu akaniambia mwanangu acha mimi niingie mtaani.

Sema nikamtazama nikamchana James mwanangu leo haupo sawa ebu nichane tu kwanza mimi mwanao halafu hapa sisi wote wa kiume kimekukuta nini.

James akaniambia kama Aisha kazingua anasema kapata bwana mpya na huyu bwana wake mpya wanapendana sana na huyo mwana kashabadilisha mpaka dini kwa ajili ya Aisha.

Daaaah mwana haya mambo mengine tuyasikie tu tusiombe yatukite kabisa yani, nikamwambia sio kesi itakuwa Aisha labda kazingua tu kama vipi tutoke twende kwa kina huyo Aisha ...Aisha mimi si shemeji yangu nitamtuliza inawezekana kagombana na James Wakarushiana maneno si unawajua wanawake tena litakalo kaa mdomoni ndo ilo ilo unapewa ...

Kwahiyo nikatoka na James mpaka kwa kina Aisha ila Aisha alikuwa anakaa kwa Dada yake na sisi pale kwa Dada yake na Aisha tulikuwa tunajulikana kwahiyo haukuwa mlolongo mrefu kivile kumpata Aisha.

Mimi nikamuita Aisha nikaongea nae lakini wapi Aisha hataki kuelewa kabisa James nae akamfuata kuongea na Aisha kama ugomvi wao uishe ebu vuta picha mwanaume mrefu ana mbembeleza mwanamke mfupi halafu mwanaume analia daaaah yani kama dharau fulani hivi....

Aisha akakaza...Mimi na James tukaona sio kesi tukasepa zetu nikampanga vya utamu vimezaliwa vingi kama vipi ampotezee mwana akaniitikia sawa kumbe wanangu ndio sawa kalichukua neno sawa kaliingiza sikio la kulia kalitolea kushoto mazima.

Halafu jamani acha tu hakuta kitu kigumu kama kuachana na mtu ambae unamuona kila siku iko kitu kigumu sana. yani James ilikuwa haipiti siku 3 kwa 2 asikutane na Aisha...

Sema Aisha alikuwa anapendeza ajabu yani mpaka mimi mwenyewe nikawa najiuliza huyu Aisha anapendeza sana pesa za nguo anapata wapi na maisha ya kwa dada yako mbona ya kawaida tu lakini Aisha anavaa vitu ambavyo vinaendana na muda uo usika.

Mara tukasikia Aisha anarudishwa na gari aina ya PRADO time za usiku halafu anakuwa na mifuko imejazia ile mbaya ...yani inaonesha huyo anayemshushaga basi pesa kwake sio tatizo.

Mara kuna mwana akanisanua kama Aisha anatoka na jamaa fulani hivi ana miliki Mabasi ya kampuni fulani hivi ( Jina la Kampuni naiifadhi ).

Kwamba huyo mwana ndo anatunza kwa Aisha na jamaa akanitajia mpaka jina ila sasa jina alilonitajia mbona la kikristo kwahiyo inawezakana Aisha alitufunga kamba kama bahasha wake mpya kabadili dini kwa ajili yake.

Nikapiga hesabu zangu nikaona Aisha kwahiyo tamaa zimemzidi halafu yani acha sijui ndo umasikini sijui kitu gani mwanamke wa uswahilini akijiunga na chuo tu anabadilika wengi wao wanataka kuonekana wao wa kishua waenda na wakati dakika ya mwisho wanapata maradhi.

Acha niwaambie kitu wakina dada NB ; Ogopa sana mwanaume wenye biashara zake, mwenye nyumba yake , mwenye pesa zake halafu anakwambia yupo single ogopa sana wanaume tumeubwa na matamanio ...tunatanguliza matamanio kwao halafu ndo tunapenda.

Mimi nikampanga yule mwana kama uchune kimya ahakikishe yale aliyoniambia James asiyajue ....mwana akanijibu haina shida hawambii James

Aaaah kumbe bhana mimi ndo nilijiona wa kwanza kumbe mimi ndo wa mwisho na zamani sana kumbe yule jamaa kashamwambia James kama demu wake anatoka na mwana anamiliki mabasi ya mkoani...

Siku hiyo nimekaa kama mida ya saa 10 hivi sijamuona James wakati sio kawaida yetu kabisa hata kama James atakuwa yupo bize sana lazima anipigie simu anipange kama yupo bize hawezi kuja maghetto kwangu.

Nikajaribu kumpigia James kama mara 10 hivi simu inaita haipokelewi aaaah nikaona james vipi tena ...

Ikabidi niende maghetoni kwake ili kufika maghetoni kwake kama mida ya saa 12 jioni hivi kumbuka mwana mara ya mwisho kuonana kama siku 5 hivi nyuma ila ukimya wake ndani ya siku hizo ulinishitua kidogo.

Kufika maghetoni kwake nikakuta mlango umefungwa halafu ubaya wa kitu kingine mlangoni kulikuwa na kitasa kwahiyo ikawa ngumu pia kujua kama James yupo au katoka nikawauliza mdada wa pale vipi mmemuona huyu mtu siku ya leo wakanijibu hawajamuona kabisa itakuwa labda katoka asubuhi sana maana kuna mtu alipishana nae wakati anaenda kuoga James ndo alikuwa anatoka kuoga.

Aaah nikajaribu kuipiga simu huku nikiwa dirishani kwa James vipi kama mwana atakuwa yupo ndani simu si itaita itatoa mlio tu lakini round hii simu yake ikawa haipatikani kabisa nikajua mwana atakuwa kashaizima simu kabisa itakuwa labda kanimaindi mpaka mimi. Basi nikarudi zangu mtaani. Sema kabla sijarudi nikasema acha niende kwa kina Aisha.

Nilivyoenda kwa kina Aisha bahati nzuri sijui mbaya Aisha Sikumkuta alikuwepo dada yake na Aisha tukapiga piga story akanisanua sasa ila ubaya wa mambo pia dada yake Aisha alikuwepo upande wa mdogo wake ila nikajua tu lazima awepo upande wa mdogo wake si na yeye anakula neema.

Akasema James na Aisha wamegombana eti James ana akili eti kwanini anamfokea Aisha kwani kuna ulazima gani wa kupokea simu ya mtu na kuna ulazima gani wa kujibiwa meseji kila siku Kwanza Aisha anasoma yupo bize na masomo.

Ila nikaunga dots nikapata jibu kama ukiwa hauna pesa na mume mwenzako anazo pesa na umeshitukia mchezo jaribu kuwa mpole maana demu anaishi na wewe kwa kukuonea huruma tu...

Nilichukia yale majibu ya Dada yake Aisha yani anamsemaje mwanangu sana kama hivi wakati ni makosa ya mdogo wake.

Nikaona mambo yasiwe mengi sana nikamuaga huyo nikasepa zangu. maghetto nikaa kama siku tatu hivi aaaah

Kumbe bhana James alikuwa yupo yupo mule mule magheto kwake na alikuwa kashakufa zamani ila kawaida ya binadamu baada ya siku 3 anapasuka tumbo anatoa harufu kali...

Sasa ile harufu ya kunuka kwa mwili wa James ulianza kuoza na kutoa wadudu daaaah.

Yani hata sijui niseme nini ila haya mambo jamani hayafai kabisa yani ...ila yote ya yote mwana alijiua alimeza vidonge kama 30 hivi kwa pamoja akanywa na bia kwahiyo mwana alijiua kwa style hiyo baada ya kupewa hiyo taarifa kama Aisha kamuacha kisa kapata mwanaume mwengine ana pesa na anamiliki mabasi kipindi iko James ana kazi nipo nae mtaani tu tunapiga piga day waka, ikitokea kazi hii tunafanya ikitokea ile tunafanya...

Mwanangu siamini mpaka leo hii yani alikuwaje akajiua yani pia ilikuwaje mpaka Aisha akamkataa mwana kisa Pesa tu.

Uchunguzi wa polisi ukapita kesi ikaishia juu juu kama mwana kajiua mwenyewe maiti akaletwa tukazika hivyo hivyo yani unajua wakristo wana ibada ya kuaga maiti ili maiti ilivyokuwa imealibika hiyo ibada ya kumuaga haikuwepo...

Sema Aisha na Dada yake pia walikuja msibani ila Aisha alilia sana na nilitamani kama niende nimpige makofi hivi maana mimi na yule mwana ndo tulikuwa tunaelewa mchezo mzima..

Yani kilio cha Aisha nilikiona cha kinafiki sana, baada ya maziko ilinibidi nihame mtaa kabisa maana daaaah nahisi na mimi ningefanya tukio kwa Aisha maana James alikuwa kwangu ni kama ndugu yangu hivi kwangu alikuwa zaidi ya rafiki.

Rest in Peace Mwanangu uko ulipo...

Mwanao bado napambana japo life bado gumu ila nikapata muda huwa nakuombea sana.

Mungu akupumzishe peponi James.
 
Mara nyingi sana uwa nikisikiliza nyimbo ya BUSHOKE na JULIANA KANYOMOZI " usiende mbali ". uwa anamkumbuka rafiki yangu JAMES mapenzi tu ndo kilikuwa chanzo cha kifo chake.

Jamani tunatakiwa tujue maisha mafupi sana aya lakini kuna mtu anaweza akayafanya yakawa maisha mafupi zaidi kwako

Au unaweza ukalidhika na maisha yako au kipato unachokiingiza kwa siku ila kuna mtu akaja akakufanya ghafla tu usilizike na maisha yako.

Unaweza ukamuona mtu kaingia kwenye ujambazi au ana kula unga ukasema aaaah yule nae usela mwingi kajitakia ila leo acha niwapange mambo yanayoendelea kwenye maisha yetu....

Mwana kitu mapenzi kitu kingine kabisa kuna mtu anaweza akaona upuuzi ila nataka niwakumbushe hapa duniani .kama utakuwa mwanamke basi utachepuka weeee lakini kuna mwanaume moja utakuwa unamkubali balaa hata kama hana kitu na kwa wanaume hivyo hivyo.

Sasa twende kwenye mada kuu leo jamani nimemkumbuka marehemu rafiki yangu hapa nitatumia jina ambalo sio la kweli ili niwaelezee tu mwana kilimkuta nini ila yote ya yote acha mwana apumzike kwa amani na mungu ampunguzie adhabu za kabuli uko alipo.

Kwangu mimi alikuwa ni zaidi ya mwana niliisi ni ndugu kabisa maana alikuwa akipata tatizo mtu wa kwanza kunicheck alikuwa ni mimi...

Kama miaka 8 au 7 hivi iliyopita nyuma james alikuja maghetto ila si unajua mwanangu sana nikimcheck tu najua kabisa kama huyu hayupo sawa...

Nikamuuliza vipi baba upo sawa akaniambia yupo sawa ...aaah mimi nikampotezea nikachukulia ile style labda mwana hajaamka vizuri kumbe sasa mwana ana mawazo kama yote ila kauchuna kimya.

Mimi nilipata story baada ya tukio ambalo sikulitegemea kabisa kutokea kumbe bhana mwanangu james alikuwa na demu anaitwa Aisha mtoto wa chuo alikuwa anasoma pale IFM wakati uo James alikuwa kaishia form 4 tu....

Sasa baadae baada ya James kuuchuna sana akanichana salu eeeh nikamwambia niambie janangu akaniambia mwanangu acha mimi niingie mtaani.

Sema nikamtazama nikamchana james mwanangu leo haupo sawa ebu nichane tu kwanza mimi mwanao alafu hapa sisi wote wa kiume kimekukuta nini...

James akaniambia kama Aisha kazingua anasema kapata bwana mpya na huyu bwana wake mpya wanapendana sana na huyo mwana kashabadilisha mpaka dini kwa ajili ya Aisha....

Daaaah mwana aya mambo mengine tuyasikie tu tusiombe yatukite kabisa yani...nikamwambia sio kesi itakuwa aisha labda kazingua tu kama vipi tutoke twende kwa kina huyo aisha ...Aisha mimi si shemeji yangu nitamtuliza inawezekana kagombana na james ...Wakarushiana maneno si unawajua wanawake tena litakalo kaa mdomoni ndo ilo ilo unapewa ...

Kwahiyo nikatoka na James mpaka kwa kina Aisha ila Aisha alikuwa anakaa kwa Dada yake na sisi pale kwa Dada yake na Aisha tulikuwa tunajulikana kwahiyo aukuwa mlolongo mrefu kivile kumpata Aisha...

mimi nikamuita Aisha nikaongea nae lakini wapi Aisha hataki kuelewa kabisa James nae akamfata kuongea na Aisha kama ugomvi wao uishe ebu vuta picha mwanaume mrefu ana mbembeleza mwanamke mfupi alafu mwanaume analia daaaah yani kama dharau flani hivi....

Aisha akakaza...Mimi na James tukaona sio kesi tukasepa zetu nikampanga vya utamu vimezaliwa vingi kama vipi hampotezee mwana akaniitikia sawa kumbe wanangu ndio sawa kalichukua neno sawa kaliingiza sikio la kulia kalitolea kushoto mazima.

Halafu jamani acha tu hakuta kitu kigumu kama kuachana na mtu ambae unamuona kila siku iko kitu kigumu sana. yani James ilikuwa haipiti siku 3 kwa 2 asikutane na Aisha...

Sema Aisha alikuwa anapendeza ajabu yani mpaka mimi mwenyewe nikawa najiuliza huyu Aisha anapendeza sana pesa za nguo anapata wapi na maisha ya kwa dada yako mbona ya kawaida tu lakini Aisha anavaa vitu ambavyo vinaendana na mda uo usika....

Mara tukasikia Aisha anarudishwa na gari aina ya PRADO time za usiku alafu anakuwa na mifuko imejazia ile mbaya ...yani inaonesha huyo anae mshushaga basi pesa kwake sio tatizo.

Mara kuna mwana akanisanua kama Aisha anatoka na jamaa fulani hivi ana miliki Mabasi ya kampuni fulani hivi ( Jina la Kampuni naiifadhi ).

kwamba huyo mwana ndo anatunza kwa Aisha na jamaa akanitajia mpaka jina ila sasa jina alilonitajia mbona la kikristo kwahiyo inawezakana Aisha alitufunga kamba kama bahasha wake mpya kabadili dini kwa ajili yake.

Nikapiga hesabu zangu nikaona Aisha kwahiyo tamaa zimemzidi alafu yani acha sijui ndo umasikini sijui kitu gani mwanamke wa uswahilini akijiunga na chuo tu anabadilika wengi wao wanataka kuonekana wao wa kishua waenda na wakati dakika ya mwisho wanapata maradhi...

Acha niwaambie kitu wakina dada NB ; Ogopa sana mwanaume wenye biashara zake, mwenye nyumba yake , mwenye pesa zake alafu anakwambia yupo single ogopa sanaaaaa wanaume tumeubwa na matamanio ...tunatanguliza matamanio kwao alafu ndo tunapenda.

Mimi nikampanga yule mwana kama uchune kimya hahakikishe yale aliyoniambia James asiyajue ....mwana akanijibu haina shida hawambii James

Aaaah kumbe bhana mimi ndo nilijiona wa kwanza kumbe mimi ndo wa mwisho na zamani sana kumbe yule jamaa kashamwambia James kama demu wake anatoka na mwana ana miliki mabasi ya mkoani...

Siku hiyo nimekaa kama mida ya saa 10 hivi sijamuona james wakati sio kawaida yetu kabisa hata kama James atakuwa yupo bize sana lazima anipigie simu anipange kama yupo bize hawezi kuja maghetto kwangu...

Nikajaribu kumpigia James kama mara 10 hivi simu inaita haipokelewi aaaah nikaona james vipi tena ...

Ikabidi niende maghetoni kwake ili kufika maghetoni kwake kama mida ya saa 12 jioni hivi kumbuka mwana mara ya mwisho kuonana kama siku 5 hivi nyuma....ila ukimya wake ndani ya siku hizo ulinishitua kidogo.

Kufika maghetoni kwake nikakuta mlango umefungwa alafu ubaya wa kitu kingine mlangoni kulikuwa na kitasa ...kwahiyo ikawa ngumu pia kujua kama James yupo au katoka nikawauliza mdada wa pale vipi mumemuona huyu mtu siku ya leo wakanijibu hawajamuona kabisa itakuwa labda katoka asubuhi sana maana kuna mtu alipishana nae wakati anaenda kuoga James ndo alikuwa anatoka kuoga....

Aaah nikajaribu kuipiga simu uku nikiwa dirishani kwa james vipi kama mwana atakuwa yupo ndani simu si itaita itatoa mlio tu...lakini round hii simu yake ikawa haipatikani kabisa nikajua mwana atakuwa kashaizima simu kabisa itakuwa labda kanimaindi mpaka mimi...basi nikarudi zangu mtaani. sema kabla sijarudi nikasema acha niende kwa kina Aisha ....

Nilivyoenda kwa kina Aisha bahati nzuri sijui mbaya Aisha Sikumkuta alikuwepo dada yake na Aisha tukapiga piga story akanisanua sasa ila ubaya wa mambo pia dada yake Aisha alikuwepo upande wa mdogo wake ila nikajua tu lazima awepo upande wa mdogo wake si na yeye anakula neema....

Akasema James na Aisha wamegombana eti James ana akili eti kwanini anamfokea Aisha kwani kuna ulazima gani wa kupokea simu ya mtu na kuna ulazima gani wa kujibiwa meseji kila siku Kwanza Aisha anasoma yupo bize na masomo....

Ila nikaunga dots nikapata jibu kama ukiwa hauna pesa na mume mwenzako anazo pesa na umeshitukia mchezo jaribu kuwa mpole maana demu anaishi na wewe kwa kukuonea huruma tu...

Nilichukia yale majibu ya Dada yake Aisha yani anamsemaje mwanangu sana kama hivi wakati ni makosa ya mdogo wake.

Nikaona mambo yasiwe mengi sana nikamuaga huyo nikasepa zangu. maghetto nikaa kama siku tatu hivi aaaah

Kumbe bhana James alikuwa yupo yupo mule mule magheto kwake na alikuwa kashakufa zamani ila kawaida ya binadamu baada ya siku 3 anapasuka tumbo anatoa harufu kali...

Sasa ile harufu ya kunuka kwa mwili wa James ulianza kuoza na kutoa wadudu daaaah ....

Yani hata sijui niseme nini ila aya mambo jamani hayafai kabisa yani ...ila yote ya yote mwana alijiua alimeza vidonge kama 30 hivi kwa pamoja akanywa na bia kwahiyo mwana alijiua kwa style hiyo baada ya kupewa hiyo taarifa kama Aisha kamuacha kisa kapata mwanaume mwengine ana pesa na ana miliki mabasi kipindi iko James ana kazi nipo nae mtaani tu tunapiga piga day waka...ikitokea kazi hii tunafanya ikitokea ile tunafanya...

Mwanangu siamini mpaka leo hii yani alikuwaje akajiua yani pia ilikuwaje mpaka Aisha akamkataa mwana kisa Pesa tu...

Uchunguzi wa polisi ukapita kesi ikaishia juu juu kama mwana kajiua mwenyewe maiti akaletwa tukazika hivyo hivyo yani unajua wakristo wana ibada ya kuaga maiti ili maiti ilivyokuwa imealibika hiyo ibada ya kumuaga haikuwepo...

Sema Aisha na Dada yake pia walikuja msibani ila Aisha alilia sana na nilitamani kama niende nimpige makofi hivi maana mimi na yule mwana ndo tulikuwa tunaelewa mchezo mzima..

Yani kilio cha Aisha nilikiona cha kinafiki sana...baada ya maziko ilinibidi niame mtaa kabisa maana daaaah nahis na mimi ningefanya tukio kwa Aisha maana James alikuwa kwangu ni kama ndugu yangu hivi kwangu alikuwa zaidi ya rafiki....

Rest in Peace Mwanangu uko ulipo...

Mwanao bado napamban japo life bado gumu ila nikapata mda uwa nakuombea sana mungu akupumzishe peponi James.
Ilikua lini?,kifo kilitokea mwaka gani?
 
🙂🙂
 
mimi hakuna mbwa itakuja itokee initese kisa mapenz...
ila nyie mjue tumeumbwa tofaut kuhimili hisia na maumiv, kuna wengine hawawez kupambana na hisia zao wanaishia kuua au kujiua...
All in all ukiona mtu anateseka sana na mapenz mfariji mtie moyo muepushe na mawazo hasi...
 
Back
Top Bottom