Rafiki kutambulishwa kwa mke/mume/mchumba? IS IT REASONABLE?

Asprin

JF-Expert Member
Mar 8, 2008
68,012
95,358
Eti Jamani:
Kwa wale wenye mahusiano ya dhati ya kimapenzi. Wenye ndoa zao na wachumba ambao wanatarajia kuingia kwenye ndoa. Au basi ma-boy/girl friends wenye mahusiano ya kingono.

Inawezekana mtu ukawa na rafiki wa jinsia tofauti. Urafiki kwa maana ya urafiki usiohusiana na mambo ya ngono. Mnapiga stori, mnabadilishana mawazo, mnashauriana mambo mengi, mnasaidiana kwa mambo mbalimbali na vitu kama hivyo (Carmel unalielewa hili, japokuwa urafiki wako ulivuka mipaka ukaibua ndoa.)

Je ni sahihi rafiki kama huyu kumtambulisha kwa mumeo/mkeo/mchumba? Yaani Carmel amtambulishe Geoff kwa mume wake kuwa huyu ni rafiki yangu. Au Fidel80 amtambulishe nyamayao kwa mkewe kuwa huyu ni rafiki yangu?

Nina rafiki yangu wa kike nataka nimtambulishe kwa wife, nahofia nisije nikazua msala.

CAN YOU? IS IT REASONABLE?
 
Mkuu achana na hiyo habari. Unless huyo wife wako kweli una uhakika si mtu zogo. Kwetu waswahili wengi hawaamini kama kunaweza kuwepo urafiki kama urafiki kati ya mwanamke na mwanaume so be careful unaweza kujilaumu baadae.
 
inategemea wewe na mwenzio mnaishi namna gani
kama mnaaminiana kumtambulisha rafiki sioni kama kuna tatizo mana urafiki sio lazima iwe jinsia moja tu
lakini kama trust ni kitendawili katika mahusiano thubutu yake
 
Sasa siku moja akitukuta tuko mkahawani tunapata chai na sambusa, wife si atajua nimekamata nyumba ndogo? Ipi hatari zaidi?
 
Mkuu inawezekana ila tatizo linakuja pale utapozidisha ukaribu yaani namaana kuwa wewe unaweza kua nyumbani na mkeo na mimi nikakupigia simu kua asee tukutane hapa zero pub nnamazungumzo....mkeo atakuruhusu....ila inapokuja opposite sex inakua ngumu sana kuamini ni urafiki tu wa kawaida!! hata mimi mamsapo kila siku anambia nipo na Xpini lazima niweke doubt hapo!!
 
inategemea wewe na mwenzio mnaishi namna gani
kama mnaaminiana kumtambulisha rafiki sioni kama kuna tatizo mana urafiki sio lazima iwe jinsia moja tu
lakini kama trust ni kitendawili katika mahusiano thubutu yake

Kama trust ni kitendawili, itakuwaje akinikuta naye zero pub napata naye mvinyo huku tukibadilishana mawazo. Si atajua tumetokea gesti kabisa? Si heri niokoe jahazi mapema kwa kumtambulisha no matter what?
 
ndo nakwambia kama hakuna kuaminiana katika mahusiano yenu yote hayo yanaweza kutokea ..
wengine vicheche
 
Mkuu inawezekana ila tatizo linakuja pale utapozidisha ukaribu yaani namaana kuwa wewe unaweza kua nyumbani na mkeo na mimi nikakupigia simu kua asee tukutane hapa zero pub nnamazungumzo....mkeo atakuruhusu....ila inapokuja opposite sex inakua ngumu sana kuamini ni urafiki tu wa kawaida!! hata mimi mamsapo kila siku anambia nipo na Xpini lazima niweke doubt hapo!!

Hahaha! Hapo mkuu umenivunja mbavu. Lakini mimi ni mwaminifu kwa mashemeji. Labda kama angekuwa Fidel. Sasa asipokuambia afu siku ukamkuta na fidel chawote bar wanakunywa mvinyo then akakuintrodyuzi huyu ni rafiki yangu itakuwaje. Si heri angekuambia mapema ujue moja?
 
Mkuu achana na hiyo habari. Unless huyo wife wako kweli una uhakika si mtu zogo. Kwetu waswahili wengi hawaamini kama kunaweza kuwepo urafiki kama urafiki kati ya mwanamke na mwanaume so be careful unaweza kujilaumu baadae.

Jamani kwa uzoefu wangu mdogo, hakuna urafiki wa kawaida wa watu wa jinsia 2 wa jinsi hii,hasa kwa wenye ndoa.Ni hatari na hakuna mwanamke au mwanaume yeyote anayeweza kuamini hili.Ni wachache saaaaaaaaaana kama sio sifuri.
 
Back
Top Bottom