Radio za FM hazina mipaka?

The Boss

JF-Expert Member
Aug 18, 2009
49,110
115,899
Jana mchana radio times fm
watangazaji sijui walianzia wapi
but wakati naanza kusikiliza nikasikia
wanashindana kutaja majina ya bangi......
I mean watangazaji kama wanne na baadhi ya
wasikilizaji wanatuma sms halafu majina yanasomwa....

Kuna siku nasikiliza kipindi cha michezo cha clouds fm
mtangazaji wao milad ayo akawa anatangaza mambo
ambayo ni ya kipuuzi mno.....
Sijui obama kamualika jlo kwenye kutazama supebowl ikulu,
mara muigizaji gani sijui wa hollywood kaachana na mke wake...

Sasa hata maana ya kipindi cha michezo hakuna....

Najiuliza hili swali hivi radio za fm hazina chombo kinachotoa muongozo????????na mipaka ya nini kitangazwe??????????
 
Nchi yetu watendaji wetu wamelala ktk kila kitu. Kila mtu anaamua kufanya anavyotaka.
 
Ndiyo maana ya market economy hiyo, kama wewe hupendi kuna watu wanapenda. Mimi binafsi sifagilii redio kama Clouds FM, lakini kama hawajavunja sheria, hata kama sikubaliani na wanachosema, nakubaliana na kanuni ya kuwapa uhuru wa kujieleza.

Ukiwashutumu hivyo na sie wengine tusiopenda dini tutasema hatutaki kusikia vipindi vya dini redioni. Na wasiopenda bongoflava watasema hawataki kusikia bongoflava, wasiopenda taarab nao hivyo hivyo, mwisho tutafunga redio tu.

Inabidi uonyeshe kuna sheria gani imevunjwa kwa kutaja majina ya bangi, ama sivyo usiwasikilize.
 
Back
Top Bottom