Mwendabure
JF-Expert Member
- Mar 10, 2011
- 2,138
- 1,040
Wakuu Nawasalimu!
Kuna hii Radio Tumaini inayopatikana ktk masafa ya 105.9FM (kwa Dar) ambayo hupiga rekodi za kizamani (zilipendwa) kwa muda mwingi. Binafsi ni mpenzi wa nyimbo za zamani zile za hapa nyumbani na hata nje na nimefarijika kwa kuwepo kwa kituo hiki cha Radio inazopiga nyimbo za enzi hizo. Pia naamini sipo peke yangu ktk hili. Lakini nashangazwa na mtindo wa kurudia nyimbo zilezile kila siku kiasi unaweza kujua wimbo gani utafuata baada ya ule uliopo hewani. Pia huwa inatokea kutoweka hewani kwa muda mwingi hata zaidi ya majuma mawili bila taarifa kwa wasikilizaji. Hali hii imenifanya nijiulize maswali mengi kuhusu lengo na dhumuni hasa la kuanzishwa kwake. Pai naamini kuwa rekodi zipo nyingi mno za kizamani kiasi cha kutolazimika kurudiarudia nyimbo hata zaidi ya mara nne kwa wimbo mmoja kwa siku.
Naomba kuwauliza wadau wa kituo hiki (najua mpo humu) kulikoni? Kama suala ni ukosefu wa nyimbo za kutosha kwanini msitoe ombi kwa wadau ili tujitolee kuwapatia hizo nyimbo?
Ukweli kituo hiki kimekuwa kimbilio la wale wenzangu na mimi ambao tunachoshwa na hivi vituo vingine ambavyo vinapiga nyimbo za kisasa na vimejaa matangazo lukuki tena ya mara kwa mara. Jirekebisheni hima!
Nawasilisha!