Q-NET Company "biashara mtandao" ni utapeli unaoenea kwa kasi Tanzania. Serikali mko wapi?

Kwanza niseme hii QNET nshaenda hadi training zao kwa kiasi flani niseme sio utapeli bali wanachembe chembe za uongo mwingi sana tena sana.
Ofisi zao Dar es Salaam Sinza Makaburini,Ubungo Mawasiliano,Kinondoni Studio(Stereo Bar karibu na kwa TID) na mpya ya juzi ipo Mikocheni B.
Mtu wako wa karibu ana kupick anakukaribisha ooh njoo on time sehem flan,ukifika vaap unapigwa kitraining pale ukiona zile hesabu za hela hautamani kuondoka sawa eeh uende mchana asubuhi jioni salamu yao ni good morning(wierd)
Kesho yake wanakuonyesha hayo mapackage yao ya millions and millions Holiday,Education & saa etc.
afu ujiunge uingee training ila wao wanakuaminisha usijali sisi tutakusapoti hao watu wawil wa kuwaweka usijali,ila kwangu ilikuwa ndivyo sivyo mm ni mwajiriwa ambae asilimia kubwa ya kazi yang ni safiri nakosa nafasi za kupeleka watu ilinipa shida kila siku wananipigia simu leta watu leta watu nilikuwa kama chizi.
Shida aliyenipeleka ni ndugu nkashindwa kumwambia umenipeleka choo gani,ila yy bado anashabikia sana kuna faida,kwahiyo nililiwa hela yangu yote na nashindwa hata namna ya kufanya.(88BB,na paradigm shif zao na welcome proffesional zao zote nnazo)
USHAURI:
Kama unataka kujiunga jua haya:
1.Utatakiwa kudedicate all of your free time kwenda hapo ofisini.
2.Kwa wiki hakikisha unapeleka watu tano zikapigwe somo
3.ujifunze kuedify na show products.

Well there is no easy money,
ILA QNET KUWENI WA KWELI UNAJUA MTU MUAJIRIWA NA MSAFIRI SANA UKISHACHUKUA HELA NDO UNAANZA KUMNANGA OOH AJIRA INAKUPA HELA NDOGO SANA NJOO QNET.
KINGINE SAA YA KUCHUKUA HELA HATA UWAAMBIE UPO KIMBIJI WANAKUJA SUMBUANENI SASA NJOO OFISI NJOO KWA UPLINE NJOO KWENYE MEETING NJOO LEADERSHIP CAMP.
KWELI QNET NI YA KUANGALIA KWA JICHO LA TATU.
 
Hii kampuni ni ya kitapeli ila uzuri ni ww mwenyewe hulazimishwi niliwai kupelekwa huko na jamaa mmoja nikagundua fasta ni wasanii alafu wameweka madada wengi kwa ajili ya kuhadaa watu ela haijawai kuwa rahisi rahisi vile eti uweke m 4 afu kila mwezi uanze kula m ngapi sijui
 
Wakuu na mimi leo nimepata mwaliko wa hii qnet....kiukweli kabla ya hapo sikuwa nimeisikia hii kitu....Nashukuru wadau wote kwa maoni mazuri mliyotoa.
Nina jamaa yangu yupo forever, rifaro sasahivi yuko na AIGM
Binafsi sijawahi kuzikubali MLM companies nimewahi kuhudhuria semina moja ya forever baada ya hapo nikawapotezea sikujiunga.
Nimejifunza mengi kupitia wadau wangu wa karibu waliopo Forever,GNLD,ORGANO,Rifaro,D9, Leo nimekutana na QNET
Bila kusahau 2014 Telex free walitrend sana kuna jamaa yangu aliliwa mkwanja wake.
 
Kuna kampuni moja inaitwa Qnet ni kampuni tanzu ya Qi company,ni biashara ya mtandao makao yake makuu yapo Hong kong,wana deal na kuuza saa,vifaa tiba n.k.

ni hivi wanashawishi watu wakope na wanunue bidhaa mtandaoni km saa n.k kwa bei kubwa km milioni 5 then automatically unakua umeshakua member then unaambiwa utafute watu kadhaa nao wanunue bidhaa ili upate kamisheni cha ajabu ni kua hta km huna hela watatumia mbinu zote za kiulaghai kwamba utapata zaidi ya milioni 10 as a kamisheni kila mwezi na maisha yko yatakua mazuri ndani ya muda mfupi sasa na njaa zetu hizi ukipiga picha m10 kila mwezi unaweza kuingia mkenge .

Hii kampuni ilishapigwa marufuku kwa "fraud" nchi kibao kama India,australia n.k.hivi sasa hapa bongo ndo imeshika kasi na ofisi zao zipo hpa kinondoni Studio. serikali mko wapi?

kwa jinsi walivyo wajanja hpa walipoweka ofisi yao huwezi jua kinachoendelea humo ndani utaona tu watu wanaingia na kutoka ukiuliza kuna nini humo ndani huwezi ambiwa,nimejaribu kunyapia nyapia mpaka nimefanikiwa kuingia na kufanyiwa semina ndo nikagundua hawa ni matapeli.

Maisha magumu yasitufanye tuwe wepesi wa kuamini visivyo aminika.
Studio sehemu gani mkuu?nakumbuka juzi wamefanya launching ya ofisi yao pale Mbuyuni,Namanga.
 
Studio sehemu gani mkuu?nakumbuka juzi wamefanya launching ya ofisi yao pale Mbuyuni,Namanga.
Studio karibu na studio bar kwa kina TID,wana ofisi nyingi hiyo ni moja wapo,ingine ipo sinza makaburini,kinondoni mwananyamala,mikocheni B.
 
Studio karibu na studio bar kwa kina TID,wana ofisi nyingi hiyo ni moja wapo,ingine ipo sinza makaburini,kinondoni mwananyamala,mikocheni B.
afu ofisi zao mara nyingi hua wanakodi guest house nzima wana nyingne nyuma ya makumbusho barabara ya kuelekea mwananyamala upande wa kulia kuna hotel ndefu kabla hujafika kuna barabara ya vumbi mkono wa kulia unaenda hadi mwisho utakutana na barabara nyingne tena ya vumbi unavuka upande wa pili maeneo hayo wengi walio mule ni wanavunzi waliomaliza vyuo au bado wapo vyuoni mafanikio yao wanawaza magari tu wakiwa wanakupiga sound utasikia wanakwambia huwez kununua gari kwa mshahara jiunge qnet soon utakua billionea washakua kama machizi nilibahatika kuingia kuwachunguza ukiwaambia huna hzo million 4 wanakupa mbinu za kudanganya uzipate
 
Me nimejoin and i am getting paid each week ikifa nshapata pesa yangu nlowekesha.. if you want to join make sure your awere that your taking risk anything might happen
Michezo hii ya pyramid ndivyo ilivyo. Walioanza kuingia hupata malipo na kuwavutia wanaojiunga baadae. Hao wa baadae ndo hasa hupatwa na masaibu ya kupokwa hata kile kidogo walichonacho.
 
Kama hujui kitu bora kukaa kimya unawezapost kitu cha uongo ukaonekana jinsi gani ubongo wako hauna kitu.pia yawezapelekea watu kukuona ni jinsi gani hujui dunia inapo elekea dunia yote inaondoka off line na kwenda online wazo lako hilo kuhusu qnet ni potofu na naomba uweke namba yako ya simu tukuelimisha usiwe unasoma udaku pekeyake soma magazeti yaliyokwenda shule utajifunza mengi.
 
Nenda facebook na type qnet india utaikuta.type qnet tanzania utaikuta type qnet kenya utaikuta.type qnet dubai utaikuta.type qnet kenya utaikuta nenda kigali kuna ofisi huyo hajui dunia inakoelekea.
 
"...usipotumia akili yako sawasawa, mwerevu atatumia ujinga wako...."

Ukiona mambo ambayo watanzania wengi wanafanya ili tu wawe na hela (sitaki kuita utajiri) utashangaa sana.
Watu hawafikiri, hawachunguzi, wala hawakumbuki yaliyotokea huko nyuma.
Nimalize kwa kusema
"...there is no difference if you choose a ugly or a good looking slaughter..."
 
Networking mkuu, unatoa pesa, unaalika watu unapiga pesa zaidi, though sio rahisi kama inavyosound...
 
Naomba kama kuna mtanzania aliefaidika na qnet ajitokeze,naona wengi wanapelekwa tu huko bila kujua!Kama kuna kunufaika au hasara...
 
Back
Top Bottom