Pugu Boys Secondary School a.k.a Pond boys

Vipi wakuu mnakumbuka yale maandamano tulifanya mwaka 1999 baada ya kifo cha Mwal.JK hai ukumbi wa Karimjee? mnakumbuka madikodiko tuliyokutana nayo pale Karimjee? ha!ha!ha sio mchezo!

Any plan for tomorrow......siku special ya ex Mwal. wa Pugu boys wakuu!
 
Vipi wakuu mnakumbuka yale maandamano tulifanya mwaka 1999 baada ya kifo cha Mwal.JK hai ukumbi wa Karimjee? mnakumbuka madikodiko tuliyokutana nayo pale Karimjee? ha!ha!ha sio mchezo!

Any plan for tomorrow......siku special ya ex Mwal. wa Pugu boys wakuu!

Gademu next level hii idea ungetupa mda mazee!!!!!

Mie sikuwepo kwenye maandamano maana niliondoka niaka ya mwanzo ya tisini lakini ni supa!!!

DOCEBIT VOS OMNIA

Kulikuwa na yule mwalimu sijui mmakua au mzaramo aliwahi kuwa naibu waziri mazee

Kituko!!
 
Mnawakumbuka TAASISI??

Ha!ha!ha!ha!ha!aaa...have got some of their pictures.....! Jamaa walikuwa wanajitolea kweli kuwasindikiza to mwisho wa Lami jioni wanapoondoka kupitia ''Bagdad''....ha!ha!ha!ha!haaa.......vile vibinti vilikuwa vipozeo vy fungus boys....sijui siku hizi bado wapo wale?
 
Mabagala alikuwa na kiduka karibu na Nyumba za walimu, siku moja watu wakaamua wamkasirishe kwa makusudi, bahati mbaya walifanya hivyo kwa kutumia kijana wa form one (sorry for him) ambaye alikuwa ni mgeni.

Walimpatia Sh 100, wakamwelekeza kiduka cha mabagala kilipo wakati huo mabagala mwenyewe alikuwa dukani, wakamwambia "We dogo nenda kwenye lile duka katununulie Mabagala tatu, mwambie muuzaji na chenji irudi.

Dogo kama alivyoelekezwa. "Shikamooo... Naomba Mabagala tatu na chenji irudi"

Jamaa alifunga duka, fikiria mwenyewe nini kilitokea.......

Sipati picha baada ya hapo kilichoendelea nini.....maake yule jamaa na mibangi ile atakuwa alienda kuitisha assembly .....then afanye identification parade....au huyo dogo alizaa naye.....ha!ha!ha!
 
Leo nimekumbuka sana Pugu seki na zile safari za kwenda Jangwani kwa Machagga na Tambaza kwa mama shija!!! wako wapi mama shija, machaga na yule mwalimu wa biology mwanamke wa pugu alifundisha PCB na charwe?
 
Just for records: Peformance ya vijana wa Pugu F4; 96 Zeros?????? .


S0147 PUGU SECONDARY SCHOOL <H3>DIV-I = 19 DIV-II = 34 DIV-III = 56 DIV-IV = 182 FLD = 96
 
Ha!ha!ha!ha! LG......True! true kabisa......kumbe na weye ni ex Pugu Boy? Safi mkubwa.....!

Mkuu hapo kny bold ....that challenge is there to live mkuu......mpaka leo hii ukienda pale Pugu, vijana bado wana matatizo ya maji, chakula na sasa uchakavu wa majengo.......sijui kwa nini serikali haifanyii kitu ile shule aisee!


Siku hizi mambo ya private tu mkuu....
 
Unawakumbuka walimu wafuatao?Mabagara,Wajimira,Nzoi,Msungu(marehemu),Secondmaster Swai(marehemu),Headmaster Mtera,Mama Mukuru,Mzee Mukuru,Makono(marehemu),Teti,Mkwiche,Grace Chuma,Mamiro,Mama Mtera,Mbulanya,Godfrey Wasiwasi,Kaunda(mwalimu wa michezo 1984-1988),Mzava,Chamuriro,Mugyabuso(marehemu),Bakari Mbonde(Ex-Rufiji Mp)n.k Orodha yao ni wengi sana,waliotangulia mbele ya haki Mungu awaweke mahari panapostaili, aaaammmmmmiiiiiiiiiinnnn.
Oh No! Nilisikia juu ya Msungu mkali wa Jiografia (aliyegoma kufuga kuku wakati analetewa ale mayai ya bure) - sijui kama alikujaongoka baadaye na kuoa. Kumbe na Mphizikia Mugyabuso kaishia? Really sorry japo hakuwahi kunifundisha, alikomalia PCM (streams B,C,D) tu. Na Swai mwenye sauti nyembamba na mpole pia? Du! Ama kweli thread hii imenikumbusha mbali sana. Thanks!

Mukuru yuko wapi jamani? Ingawa yeye hakuwa mwalimu wa Kiswahili ila mkewe, jamaa kila siku alikuja na msamiati wa kiswahili, maneno magumu ya kutuvunja mbavu huku akivutavuta suruali yake kwa elbow joint (kipepsi). Nilimfaidi sana kwenye assembly na misemo yake. Charles mkali wa Physics yupo Wizara ya Elimu sasa, kipenzi cha Mungu (Mlokole) pamoja na mkuu wake Godfrey Mosha (?) na mkewe mwalimu pia.

Mwanzoni mwa 1980s kulikuwa na gwaride kwa kila form five na form one ili kuwaandaa wageni kumudu maisha ya Pugu. Fikiria form two na form three wanapowaviringisha chini mavumbini form five wapya na kuwapiga mabuti. Ole wako ukatae na G. Mosha apate habari, shule huna hapo. Du! Jamaa mmoja Amidu alikuwa mkuu wa majeshi ya Shuleni hapo, wakati huo huo akawa mkuu wa jikoni lakini mlokole aliyekubuhu. Tulilazimika kupanda lori kwenda kutafuta kuni misitu ya Kisarawe ili tule mchana tunatolewa darasani. Siku moja tuligoma tukiwa form six kwenda kutafuta kuni, wacha tuchapwe mboko!

Nakumbuka Charles Philemon aliandikwa ubaoni na mwanafunzi mtundu mmoja, kwamba "Mwalimu Philemon Alaaniwe" Alipotaka kuanza kufundisha fizikia mwalimu, akaona ubaoni maneno hayo, wacha! akaacha kufundisha tangu siku hiyo na walimu wote wakagoma ati tumeitukana mpaka serikali na Rais. Tukasusiwa darasa kufundishwa, kila mmoja akajitetea kukwepa Division zero. Kweli watano wakatoka stream yetu na division zero. Lakini Mungu sio athumani, wapo madaktari na wakurugenzi kutoka darasa lile leo hii.

Asante kwa kunirudisha Pugu.
 
Ha!ha!ha!ha!ha!aaa...have got some of their pictures.....! Jamaa walikuwa wanajitolea kweli kuwasindikiza to mwisho wa Lami jioni wanapoondoka kupitia ''Bagdad''....ha!ha!ha!ha!haaa.......vile vibinti vilikuwa vipozeo vy fungus boys....sijui siku hizi bado wapo wale?

ebana eeeh...umenikumbusha kitu yangu! Sijui imepotelea wapi?
 
Mkuu mbona kipindi hicho hii shule ilikuwa imeshafanyiwa ukarabati wa nguvu na DANIDA na ilikuwa inaonekana ni bomba?? Wewe ulizia miaka ya nyuma ktk ya miaka ya 1980 hv jinsi ilivyokuwa imechoka.

Mkuu,

Kwa hili ulikuwa sawa. Nimechanganya Pugu na Minaki. Niliongea na Dogo akasema kuwa alikuwa Minaki na si PUGU. Kwa sababu mama yake alikuwa akiishi Gongolamboto, alikuwa akiona wanafunzi wa Pugu wakija kuchota maji. Kwa hiyo akakataa kwenda pale kwa shida hiyo na akaomba aende Minaki.

Ile shule niliyoiona ni Minaki. Ilikuwa imechoka sana. Sijui kwa sasa ikoje.
 
hahaha nimekumbuka mabli sana hasa lile bango lililoko pale mbele ya jengo la utawala pale tulipokuwa tunasimama kila asubuhi na jioni kwa rollcall lile bango linasema "Docebit vos omnia" ni kilatini inamaana "Teach them everything" namkumbuka sana marehemu mwal. Msungu alilipenda sana hili neno. Hivi mkuu wakati uko pale mwal Juma wasiwasi ulikuwepo, aaaa huyu jamaa wa Tangakunani ni mwisho wa maneno mnoko huyo! Fungus! Pond du nimekumbuka long sana mi nakumbuka tulikuwa tukienda kusoma tution pale tambaza wakati wa likizo, jamaa walikuwa wanatuita Mitambo ya Fungus! Long live Pugu/St. francis!
 
Kila asubuhi mkondo mmoja lazima kuchota maji ya kupikia kila mwanafunzi ndoo sita kutoka Pondi,na jioni darasa lingine nalo huchukua nafasi.Kweli tunahaki ya kupata maisha tuliyonayo,Pugu wee acha tuuuuu.


Amosam ulipo kuja KIBAHA SEC.ilkua kama peponi,mimi tofauti kidogo nimepiga madaras yote ya sec. KIBAHA,nilipojoin UDSM ndio maisha nikaona magumu sana.
 
Mzazi acha kabisa, Pugu nomaaaaaaaaaa, mi nilisoma hapo 1993/95.Kaka unamjua mzee wa shamba wewe kwa mihogo yake? unakumbuka beto nyuma ya azimo zile zisizo na milango ambazo lazima uweke bendera kuashiria uwepo wako? unakumbuka scrambo ya msosi kuwe dinning? unamkumbuka marehemu Mabagala na bakora zake za kuamsha student asubuhi? unakumbuka mkwara wa kobra akikukuta unadrop? unakumbuka bagdad kwa wauza mafuta na ukibaka wao? unakumbuka chai maharage za enzi zile tulikuwa tuanapandia pale DDC? unmkumbuka marehemu Msungu wa kula kuku na mayai yake? unakumbuka enzi zile kabla ya kuja mademu wa taasisi akipita mtoto wa kike mwalimu watu wanaenda bafu kupiga mambo yetu yaleeeeeee? Kaka kama ulimaliza juzi juzi hayo yalikuwa historia kwako ila hapo zamani Pugu ni sawa na JKT.Life ile imenipa ujasili wa maisha na najiamani kama nini.I MISS U PUGU HIGH SCHOOL.
 
Leo nimekumbuka sana Pugu seki na zile safari za kwenda Jangwani kwa Machagga na Tambaza kwa mama shija!!! wako wapi mama shija, machaga na yule mwalimu wa biology mwanamke wa pugu alifundisha PCB na charwe?

Mkuuu zile safari za Jangwani na Azania kwa Mchagga na Mkandawile zilikuwa soo, unakumbuka ukishuka uhuru na kuanza kutumbea hadi Jangwani, ukifika unastink mbaya mpaka wale warembo wanakutenga.Nakumbuka nilikuwa na perfume yangu inaitwa AYU naipuliza nikikaribia pale jangwani mateso yale we acha tu.Mwinshehe yuko wizara miataala na Charwe alikuwa headmaster pale shemshanga sec korogwe ila kavuta tayari.Mi nilikuwa katibu wa shule 1994/95 namshukuru Mungu nilikuwa nakula top layer.Anyway ni mambo mengi ya kuikumbuka Pugu, labda tuarrange kongamano la waliosoma Pugu kisha tuchangie fedha ili tusaidie mambo kadha wa kadha.
 
Leo nimekumbuka sana Pugu seki na zile safari za kwenda Jangwani kwa Machagga na Tambaza kwa mama shija!!! wako wapi mama shija, machaga na yule mwalimu wa biology mwanamke wa pugu alifundisha PCB na charwe?

Mkuuu zile safari za Jangwani na Azania kwa Mchagga na Mkandawile zilikuwa soo, unakumbuka ukishuka uhuru na kuanza kutumbea hadi Jangwani, ukifika unastink mbaya mpaka wale warembo wanakutenga.Nakumbuka nilikuwa na perfume yangu inaitwa AYU naipuliza nikikaribia pale jangwani mateso yale we acha tu.Mwinshehe yuko wizara miataala na Charwe alikuwa headmaster pale shemshanga sec korogwe ila kavuta tayari.Mi nilikuwa katibu wa shule 1994/95 namshukuru Mungu nilikuwa nakula top layer.Anyway ni mambo mengi ya kuikumbuka Pugu, labda tuarrange kongamano la waliosoma Pugu kisha tuchangie fedha ili tusaidie mambo kadha wa kadha.
 
Pugu boys, mnamkumbuka Cobra na Swai? Mnakumbuka mgomo wa 1994 wa msosi mpaka Swai akasema 'kama sambusa mtakul mmhhhh'.Beto wakuu, lazima uwe na special jezi otherwize ukienda na uniform class watu hawakai.Je mnakumbuka toilet paper za Pugu miaka ya tisini ni gazeti lililofinyangwa likawa lainiiiiiii.Mtoto wa mama Pugu hasomi walahi.
 
HHHaaaaaaaaaahhh, pond boys.......... Nakumbuka mbali sana miaka kumi sasa tangu nitoke pale mahala, Nakumbuka baba wa taifa ameiaga dunia tukiwa pale, ililazimika tutembee kwa miguu toka pugu hadi karim jee mjini ili kumuenzi baba wa taifa ili lenye ufisadi mkubwa. Tuliondoka na mabango kibao mkuu wa msafara huo akiwa Juma Wasiwasi.

Kuna ticha mmoja anaitwa mkandawile alikua anakuja kutuzingua na ma'chemia yake ya kukalili akawa anafundisha tuition. Ticha flani anaitwa Ngolu alikua anafundisha physics sasa hivi yupo pale Mbeya anafundisha Iyunga Secondary.

washkaji walikua wanaponea MADEMU WA TAASISI, Fangus noma...... Mabagala nae anafanyia mazoezi kwa kukimbiza wanafunzi, zamu za kuosha madishi ya misosi kama kawa kama huoshi hauli. BAGDHAD wanamwaga KONDOM barabari:target:
 
WAPI HIYO MAZEE... MUZEE WA SHAMBA, CHARWE, MBARAKA, MSUNGU (rip), CHAVILA, MUGYABUSO (rip), NZOWI, MKANDAWIRE, WASIWASI, AMANDA (HEHEHEEEE), PITA SHIJA, WAZEE WA AZIMIO,

I MISS OLD GOOD DAYS, LEO NAJISKIA KUPITA PALE PUGU NIANGALIE ZILE PIT LATRINE KAMA WAMEBADILISHA, MAANA ILIKUA LAZMA UENDE NA CHUP! TU LA SIVYO NZI WANAHAMIA KWAKO

DOCEBIT VOS OMNIA
 
Back
Top Bottom