Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,485
- 40,014
Ndugu MM,
Hii note ya mpenda TZ imeeleza na kupitiliza... Hata kwenu unapoona jirani adui anaunguliwa na nyumba halafu ukasimama na kuanza kunyooshea vidole badala ya kukimbilia mchanga na maji kuzima moto ni dhahiri tafsiri yake unatamani nyumba iteketee tena bila mtu mwingine kujua asijeuzima moto!.
MMM nimesoma maelezo yako kwa ufasaha yamekaa kinafiki sana! wewe kama mpiganaji kwanini unanyoosha vidole tu cdm??? kwanini usiibuke kama mwanaume ukawapa ushauri na mawazo kama ulivyowapa Tanzania Police force???? ni dhahiri kabisa unataka mabadiliko sikatai lakini kwa kutumia nguvu nyingi hivi kukosoa tuuuu bila kutoa wazo la kuokoa pale panapokwenda mrama inatafsirika kwamba wewe unahamu kuona nyumba ya jirani yako (cdm) ikiteketea!!!
Naona umeweka mpaka biography yako ya namna umefanya makubwa na mengine yamechukuliwa instantly na kuwekwa kwenye operations na labda zikaleta maendeleo, ni hatua kubwa sana hii!!! tena wewe basi uko popular kimantiki na kimaarifa kwahiyo ukiwaambia cdm sasa hivi wafanye nini naamini instantly watayabeba mawazo na michango yako nakuanza kuyapanga kwenye operation zao na nikuhakikishie cdm wanahamu yakusikia mapungufu yao na wanaham zaidi yakusikia na solutions za mapungufu hayo pia!!!
Lakini Mzee ukinyoosha vidole tuuu kama unavyofanya hapa basi wewe ni piper tu ambae nyuma yake kuna the payer anae determine the tune!!!
japo unasema umesoma kwa makini ni wazi hujasoma vizuri. Kwa sababu kama ungekuwa umesoma kwa makini ungeona kuwa tayari nimeshatoa msaada wa kutosha kwa CDM na ninaendelea kutoa zaidi ya mnavyofikiria. Kufanya hivyo hakunikatazi kuwa critical. Yawezekana wengine ambao wanajionesha kuwa wanaipenda sana CDM na kuikubali hawajafanya lolote kuisaidia ishinde zaidi ya kuisifia tu. Hivyo soma taratibu unaweza ukaibuka na vitu viwili au vitatu badala ya kuita watu majina ukifikiria umesema jambo la maana.