Nicholas
JF-Expert Member
- Mar 7, 2006
- 25,260
- 7,195
wait a minute.......mwalimu alitoa elimu bure , alipigana vita ya kagera, alitoa msaada wa mali na hali kukomboa nchi nyingine na baba wa hawa mafisadi wa leo wa ccm wakamhujumu na kuuwa kila kiwanda.Mwalimu NYerere alitoa elimu bure, matokeo yake baada ya miaka 20 nchi ilitembelea magoti. CHADEMA (Mh Slaa) japo ya kujua hilo bado ilisisitiza kutoa Elimu bure kwa watanzania wote ili ishinde uchaguzi 2010, lakini ikaanguka. Hii ni kutokana na ueleo mkubwa wa watanzania na kuelewa kuwa hizo ni PROPAGANDA ZA UONGO.
Suala la uelewa wananchi na sera ya Dr. Slaa-tunahitaji maelezo.Kwani vilivyofanyika kwa vitendo na CCM ni vibaya sana,sasa sijui kwanini waamini kitu walichokiona ubaya halafu wasiamini walichoahidiwa na mtu asiye shemu ya ubaya?
Umechemsha Kilimanjaro si Ngome ya CDM.Ila kuna maeneo CDM ina nguvu .Na unahitaji kuthibitisha hili.Wiki iliyopita nilipoandika Thread "CHADEMA NI CHAMA CHA PROPAGANDA" wengi walidai nilete ushahidi au vyanzo vya taarifa hizo. Sikufanya hivyo kwa kuogopa Mod kuifuta habari hiyo. Leo nimeamua kuandika ushahidi wa Propaganda hizo za uongo tukianzia kwenye kipengele cha ELIMU BURE KWA WATANZANIA WOTE.
Ili twende hatua kwa hatua naona vyema tuanzie na mkoa wa Kilimanjaro ambako ndio Ngome ya CHADEMA ilikojikita. Naomba waziri kivuli wa fedha wa CHADEMA aeleze kinaga ubaga ni vipi kwa kutumia kodi ya mkoa wa Kilimanjaro itamudu kutoa elimu bure kwa wananchi wa mkoa huo kabla hatujazungumzia Tanzania nzima.
Naona umeamua weka link ya Kigoma sijui ndio hila hizo ama?Mkoa wa Kilimanjaro unaongoza Tanzania nzima kwa kuwa na shule za Sekondari nyingi kuliko mikoa yote ya Tanzania. Una sekondari 288 wakati hata Dar es salaam ina sekondari 252 tu (Chanzo: www.moe.go.tz/NectaResuls). Wakazi wa kilimanjaro ni 1441000 ukilinganisha na Dar es salaam ambao ni takriban 2,809,000 (Chanzo: Tanzania: Regions, Major Cities & Urban Localities - Statistics & Maps on City Population). Pato la kodi la mkoa wa Kilimanjaro (Rombo, Hai, Mwanga, Same, Mosho mjini na Moshi vijijini) ni 14,236.4 Milioni (Tzsh) wakati lile la Dar es salaam ni 441,000.5 Milioni (Tzsh) (Chanzo: Tanzania Revenue Authority - Kigoma).
Kwa taarifa yako Kilimanjaro Vipindi vya Mkapa na hata mwanzoni Kikwete akiingia Kilimanjaro ilikuwa inacheza kuanzia no.1 hadi 5.Vyanzo vikubwa vikiwa border ya Holili, utalii ,misitu ya west, na mazao kama viazi,vitunguu, nyanya, carrots etc..
Usisahau pia kuwa Sukari ya TPC ,Gypsum ichimbwayo upare na dhahabu, pamoj ana madin mengine ambayo serikali ya ccm haijua hata kama yanachimbwa ni maeneo CDM wanaweza rudisha hivyo vyanzo kataka njia sahihi na maisha yakenda vizuri.
Data TRA walizoweka ni selective sana na ni za miaka ya nyuma.
http://www.tra.go.tz/index.php?option=com_content&task=view&id=282&Itemid=64
Kwanza mkoa mdogo na uliopigwa vita kama kilimanjaro kuwa na shule zote hizo ukilinganisha na idadi ya watu inaonysha jinsi gani wakitumi shule zao vizuri.Muda si mrefu wanabadili mkoa kuwa Macau.
Kwanza ujue kuwa Sera ya majimbo inapinga dhana potofu yako.Kuwa watatumia hela za mikoa mingine kuendeleza mingine.majimbo yanakuwa na gavana anayekuwa na utawala unaojitegemea kabisa bila kupingana na serikali kuu.Majukumu ya jimbo yanajulikana kam aleo watu wajuavyo ya mikoa na ya serikali kuu pia hujulikana pakiwa na tofauti ya umiliki hela.Kabla sijaandika zaidi naomba huyu waziri kivuli wa fedha wa CHADEMA akisaidiana na wapambe wake hapa JF wanieleze ni vipi watazigawanya hizo 14,236.4 milioni Tzsh katika huduma za matibabu (hospitali, zahanati na elimu ya afya), Polisi, utawala mkoa na wilayani, pembejeo, na Elimu (mishahara ya walimu, ukarabati na stationaries).
Mkishindwa kufanya hivyo maana yake ELIMU BURE KWA WATANZANIA WOTE NI PROPAGANDA YA UONGO. Vinginevyo mlitaka kutumia pesa ya walipa kodi wa mikoa mingine kuendeleza mkoa wenu maana kiuchumi haiwezekani Kilimanjaro yenye wakazi 1441000 iwe na shule kupita Dar es salaam yenye wakazi 2,809,000.
Nasubiri majibu yenu kabla sijaendelea na sekta nyingine.
CDM wana insist kuwa watacontrol mapato ambayo leo CCM wanapeleka kuficha nje na kuwaachia wawekezaji, wataongeza kipato pia kwa kutumia vitu vilivyolazwa na kukosa ubunifu kwa CCM.
Hiyo figure (14,236.4 milioni) ya zamani ambayo imekuja kutokana na wizi wa CCM, vita ya kuuangusha huu mkoa ktk kila nyanja.Hiii si figure iliyopaswa iangaliwe kama vile matokeo mengi ya kura yasivyo asilia.Ila nakupa majibu.
Na suala la deficit ni kawaida kwa nchi nyingi duniani ndio maana hata Nyerere na hata Kikwete leo anakopa.Jimbo linalopungukiwa na hela linaweza kopa serikali kuu na kuhitajika lipa baadaye.Hofu ni kwa mikoa ya wavivu,wataishi sana kwa federal governement rescue packages.hawa ndio watakula vya wenzao.
Mwisho nakuambia kuwa hiyo figure ya TRA ni kodi TRA waliyopata na si vinginevyo.Hakuna makusanyo ya Manispaa,vijiji na kata.Nahdani umeanza ona ni wapi kichwa yako haikuwa sawasawa kama si makini sana.Idara ya misitu inakusanya mapato toka katika misitu,KINAPA wanakusanya toka kataka mlima na mbuga iliyopo chini ya mlima.Hata ni mapato ambayo sio kodi ya kwenda TRA.Tanesco,Posta, national House etc.Hawa wote wanapokea mapato kwa niaba ya serikali na haya yote si kodi ya kwenda TRA,kwani katika risit zao utaona VAT na kodi nyingine vikiwa zimevunjwa.Ila mwisho wa siku hela zinakwenda hazina.
Manispaa na taasisi nyingine ndizo zimeweka Lami mji mzima.Ndio wanaomikili shule,zahanati, ma hospital, na hata za makanisa kodi za kipuuzi zikipunguzwa au kuondolewa watachaji kiasi kidogo cha ada ambacho serikali ya ngazi husika itaweza lipia.
Kuthibitisha kuwa CCM ni vimeo, kuna mikoa imekuwa ikitoa dhahabu, alamsi na makaa ya mawe, na sasa gesi ila hadi leo miji yao vumbi kama vile barabara za maporini.Tatizo hapa si kipato,ila misuse na misallocation.