Propaganda za uongo: Elimu bure, CHADEMA ikishinda

Ccm wanafanya reference kwa chadema kila wanachotaka kufanya.

Nchi ina vyama vya siasa 18 vyenye usajili wa kudumu lakini ccm macho yao wameyaelekeza chadema.

Mathalani cuf nao waliahidi elimu ya bure lakini hawasemwi, bila shaka ni sababu ya ndoa na ccm.

Mleta mada umejaa ushabiki wa kitoto na propaganda kwakuwa ni dhahiri unafahamu mfumo wa kupanga bajeti ya nchi yetu mikoa haipangi bajeti ya matumizi kwa kuzingatia kiasi walicho contribute kwenye pato la taifa. Serikali kuu ndiyo inapanga itumieje kodi zetu, lakini umeamua kupotosha watu.
 
alieniambia atagombea tena ni yeye mwenyewe kwa kauliyake aliitoa ktk mkutano wa hadhara pale viwanja vya sahara,ila kwa sasa hata wazo la kugombea atakua hanatena maana watu wa ilemela wameshamwambia uso na macho au wazungu wanasema live kuwa hata uchaguzi ufanyike kesho bora wachague ng'ombe kuliko kumchagua mtu muongo anaewatukana wapigakurawake.
Wacha chuki zako binafsi wewe. Gombea wewe unayedhani watu wa Ilemela wanakuona jembe.
 
Usemayo ni kweli na sikweli. Kuwa huko Zaire mikataba ilivunjwa ni kweli lakini unachoshindwa kuelewa ni kuwa wakati unafanya hivyo uko mgongoni kwa nani. Kwa mfano Libya leo mikataba yote inaweza kuvunjwa kwa masaa tu. Kwa sababu nia ya vita vyenyewe ilikuwa ni kugeuza mikataba toka kundi 'A' kwenda kundi 'B'. Unajua kesi ya fisi........

Lakini kwa suala la Tanzania ni gumu kwa vile mwenye mikataba ndiye mwenye Mahakama ya kimataifa....... Uganda iliwalipa wahindi wote mali yao... Wakati watu kibao duniani wamedhurumiwa ardhi zao na mali zao hutasikia wanalipwa.

Hii dunia imekaa kivyake vyake ndugu yangu, wala haina haki. Hayo ninayokwambia ndio majibu JK aliyopewa na Uingereza, Canada na Marekani. Sasa wewe sisi mizi utafanya nini.

Tukiendelea na uongozi wa CCM/Mafisadi, itakuwa vigumu kweli kuvunja mikataba. Hao hao ndio wanaotudanganya kuwa mikataba ni siri kati ya serikali na mwekezaji wakisahau kuwa bunge, ambalo ni mhimili mwingine wa utawala, pia wanalo jukumu kuidhinisha mikataba. Sasa hivi hao hao viongozi wa CCM wamo mbioni kugawa maeneo yetu ya ardhi (Pinda) kusaini mikataba ya harakaharaka (Malima) kana kwamba there is no tomorrow. Na mikataba yote wanayosaini ni ile inayompa maslahi "mwekezaji." Ndio maana nimesema tunahitaji regime change. Sata amefanikiwa Zambia. Na sisi tunaweza. Na kuhusu Uganda, si kweli kwamba Wahindi wote walilipwa mali zao. Alichofanya Museveni ni kuwakaribisha wale waliotaka kurudi warudi, lakini hawakupewa fidia. Tunachohitaji Tanzania ni nia tu na kwa sababu mingi ya mikataba hii imeandikwa na wawekezaji na mawaziri wetu kuhongwa kitu kidogo tu na kusaini away urithi wetu tunachotakiwa kufanya, baada ya kuiondoa CCM mamlakani, ni kuwaita hao wawekezaji na kuwaambia huku tukiwaangalia usoni, tunajua mchezo mliotuchezea sasa ngoma ya mdundiko imekwisha. Wataufyata!
 
Usidhani watu wa Mwanza ni limbukeni kama wewe, na hii inaonyesha jinsi gani hujui hata kazi za mbunge nini, pili mbunge sio sultani kwamba kila kipindi lazima achaguliwe yeye tu, hizo ni fikra duni za wachovu kama wewe. Wananchi wana haki ya kubadirisha uongozi kadri wanavyotaka. Aliye kuambia mbunge aliyepo sasa lazima agombee tena ninani?

Kamuulize Mh Slaa aliyewapiga Biti akina ZITTO hata kuchukua fomu za kugombea urais wasahau mpaka yeye atapokufa.
 
kama mimi mbwiga basi wewe *****,umepitiwa naule usemi usemao ukipenda ukiona chongo utaita kengeza,huyo mbunge aliedanganya watu wa ilemela wakampa kura hata akimaliza huo mudawake wamiaka5 hawezi hata kurudi kugombea tena amelikoroga na atalinywa,na ushahidi upo wa mikanda yavideo alivyowatukana watu waliomfata kumuuliza kuhusu ahadi ya elimu bure,pia kuna ushahidi wa cd wakati wa uchaguzi alivyowadanganya watu mambo mengisana hata aliahidi kuwapelekea maji wale waliokua hawana leo hata kupita jimboni anaona aibu,akipata tena kura ilemela hata masha atakua tena mbunge wa nyamagana,nazani huwajui watu wa mwanza unawasikia tu.

Wabunge kama hawa Toka CHADEMA ni wengi sana, na 2015 wote hawarudi hata wakibadili sura zao na kuweka maboya mengine toka chama hicho hatutawachagua. Hawa wamezoea na ndio maana wakereketwa wao wana hasira na JAZBA kali hapa JF kwa sababu za mwizi ni 40. Na arobaini zake ni 2015, msijihangaishe kutoa fedha zenu kwani fedha zitaliwa na ubunge hamtapata.

Mtachofanya ni kwenda kuandamana tu.
 
Mkuu Zawadi Ngoda naona unaogelea katika utaratibu ule ule unaofanywa na wanaCCM wenzanko, japo wewe najua uko CCM kimaslahi . , Mmegundua kwamba CCM haiwezi kuonekana nzuri au kukubalika mbele ya jamii. Ni chama kilichochoka, kimepoteza dira, hakijiamini na support base yake haieleweki na haiaminiki. Hivyo mmeona namna pekee ya kujinusuru ni kuwaaambia wananchi ni jinsi gani CHADEMA ilivyo mbaya. Bahati nzuri mwenendo huu kama historia inavyotuonyesha ndiyo huwa mwisho mwisho wa tawala dhalimu zote look at Libya, KANU enzi zile, Utawala wa makaburu, MMD kule Zambia, The ever rigging party ZANU PF etc. Wote hawa walipita hatua hii mnayopita wakati kamba za mwisho mwisho za tawala zao zinakatika hivyo haitushangazi na wala si hatari. Ni maandalizi mazuri ya kutoka kutawala na kuwa wapinzani.

Ushauri naokupa na ni vema ukauzingatia ni kwamba hata siku CCM haitakuwa nzuri eti kwa sababu ya ubaya wa CHADEMA au CUF au TLP. Kwa wapenda mabadiliko hawatavutiwa na CCM eti tu kwa sababu CCM inawaambia CHADEMA haifai. CCM haitakiwi iongee kwa sasa inatakiwa kuonyesha vitendo, success stories na mwelekeo wa Taifa kiujumla. Haiwasaiidii kuwapaka matope CHADEMA kwa habari za kutunga wakati CCM ndiyo tunawasikia mkikwaruzana kila siku, kastori kenu ka kuvua gamba mmeona hakatekelezeki basi mnaona sasa ni kuiandama CHADEMA tu hahahahahahaha! Kuporomoka kwa CCM hakujaanza mwaka jana wala juzi ni zaidi ya miongo miwili na mnachoona sasa ndiyo hatua za mwisho kwa ufalme ulioparanganyika.

Ongeza jitihada though maana hiyo kazi uliyonayo si ya mkataba, ukiisha itabidi urudi tena kwa JK hahahahahaha ahahahaha!!!!!!!!!!!!! What a life???????????
 
Hapana, sitakataa ukinieleza mipango yenu. Namba hazidanganyi hata siku moja. Ukinieleza kuwa utakusanya jumla ya sh 100 hapa na pale, na utatumia sh 90 hapo sina ubishi, na haya ndio mahesabu ninayoyaomba hapa JF. Lakini ukasema kuwa utakusanya sh 100 na utatumia sh 110, hapo tutahitilafiana. Ninachohitaji ni kujua jinsi CHADEMA walivyojipanga kupata mapato na matumizi yake katika mahesabu ya karibu ya mwananchi.

Ukisema tutapunguza mishahara ya wabunge na viongozi wa serikali, ok. Lakini ninachohitaji kujua mimi ni NAMBA kuwa katika mapunguzo hayo utakusanya sh ngapi. Ninachotaka kuepuka ni kuzungumzia kuserve sh mil 100 wakati matumizi tunayoyazungumzia ni sh mil 200.

Mategemeo yangu ni kwamba mjadala ungekuwa wa kiuchumi zaidi kuliko wa kisiasa, pamoja na kuwa maamuzi ya kisiasa ndio yataongoza mfumo husika.

Kifupi bado sijapata kile nilichokitegemea huenda baadae kidogo.
Shukran sana nimekuelewa vizuri sana lakini hapa JF sii mahala pake kwa sababu haiwezekani kupata namba sahihi, hata mimi siwezi kupata jibu kwa nini Elimu bure haiwezekani kwa mahesabu ya CCM. Na hata kama nitauliza hapa sidhani kama nitalipata jibu sahihi, isipokuwa mara zote swali kama hili hutolewa wakati wa uchaguzi na namba zikatolewa kulingana na makusudio ya chama ktk kukusanya fedha hizo na matumizi yake..

Hivyo kama kweli wewe ni mwelewaji ktk vitu nilivyokupa hapo nyuma, nikikupa namba yoyote utaweza vipi kuhakikisha kama kweli ndicho kiwango kitakacho kusanywa?.. tuwe wakweli maanake Chadema wanaweza kusema kwamba watategemea kukusanya nusu Trilioni tokana na makato ya matumizi ya serikali! Kwa mfano ktk misamaha wa kodi tunapoteza billioni 700, wewe na mimi tutaweza vipi kuhakikisha ukweli huu.. Hivi tulipo, hatufahamu rais wetu analipwa na kutumia kiasi gani, mawaziri wetu, wabunge wetu na kadhalika maanake haya yote ni maswala nyeti wao wakidai "Confidential" hatupaswi kujua pamoja na mikataba yake.

Leo tunakwenda walipa Dowans mabilioni, hizi fedha zinatoka wapi? Mlitwambia au nisema CCM walituambia huu ndio mwisho wa mahotel kubadilisha majina ili walipe kodi stahiki, lakini ndio kwanza Kilimanjaro na Sheraton zinazidi kubadilisha majina wakitumia Francise names ili tusipate kuwajua viongozi wanaomiliki hotel hizi tukiendelea kufikiria sijui za Mwarabu au Msomali alowekwa kupumbaza watu...

Kifupi mkuu wangu Elimu haichukui sehemu kubwa ya bajeti ya serikali hata Canada ambako Elimu ni bure utaona ni asimia ndogo sana ya bajeti yao inatumika ukilinganisha na matumizi ya wizara nyinginezo kwa sababu nyumba (madarasa) na vitabu ni vitu ambavyo vinadumu na elimu haiozi. Ukisha weka msingi bora matumizi yake makubwa yapo ktk mishahara na vifaa vya kufundishia.

Swala la majimbo ambalo wengi wanalizungumzia hapa, naweza kukubaliana nao ktk maswala mengine lakini sio Elimu kwa sababu jimbo moja linakuwa na mikoa zaidi ya minne hivyo pato la Jimbo moja linaweza kabisa kuwa kubwa kiasi cha kuweza kutosheleza Elimu pamoja na marekebisho makubwa ya ukusanyaji kodi...hili halina ubishi kabisa yaani ni aibu iliyoje kwa nchi kama Tanzania wanaolipa kodi hawafiki millioni 3 wakati hesabu ya watu waliojiandikisha tu kupiga kura ni millioni 19!. Eeeeh! yaani siasa ni muhimu zaidi ya kusisitiza ulipaji kodi, sasa tunategemea vipi kuendelea kiuchumi ikiwa siasa ndio zinatawala Uchumi..

Halafu pia tukumbuke Chadema hawajatueleza mpango huo utaanza rasmi lini? Hata wangeshinda uchaguzi ulopita wasingeweza kubadilisha kila kitu ikiwa ni pamoja na kuondoa sheria ya Mawaziri kuwa wabunge, kufuta kazi za wakuu wa mikoa, wilaya na kadhalika - both nature and the legal system must be moving gradually.

Kitu kimoja muhimu ambacho nakuomba tuwe pamoja.. Tanzania fedha ipo, isipokuwa tumekuwa na kiburi cha umaskini hata tukikopeshwa fedha tunataka tusipangiwe jinsi ya kuzitumia kwa sababu tunamiadi nje ya maendeleo ya nchi yetu. Miaka ya Nyerere na tulipewa mikopo ya maendeleo kwa jina la Tanzania, tukajenga reli ya Tazara, tukaanzisha shirika la ndege, tukajenga viwanda vya Ufi, Pamba, Kahawa, Korosho n.k na hata baiskeli zilitengenezwa Tanzania..Leo hii hawa wachawi wanatuambia - Hatuwezi kupata mikopo isipokuwa kwa kupitia mashirika ya nje. Tazama mikataba ya leo ikiwa ni pamoja na huu wa Mchuchuma..tunashindwa kupewa mkopo sisi kwa sababu hatuaminiki!..tunaficha nini ukweli huu, tumeuza uhuru wetu kwa sababu tumeharibu wenyewe jina la nchi yetu kwa matumizi mabaya ya mikopo! Nchi kibao zimetukatia na pengine hata WB nao hawatuamini tena isipokuwa kwa masharti yao..

Halafu hawa viongozi wanakuja bila aibu na ujasiri wa kutuambia mkataba huu ni mzuri sana hali sii mkataba wetu sisi na Bank wakopeshaji kisha hao wawekezaji wakawa contracted, bali ni mkataba wa wawekezaji na bank ambao wanatumia mali yetu kama dhamana yao na wanachukua asilimia kubwa ya pato!..Upuuzi kama huu hata siku moja siwezi kukubaliana nao hata kidogo pamoja na kwamba tunahitaji umeme!

Asikudanganye mtu, hakuna kitu kisichowezekana maadam tutaweka nia kinawezekana kabisa.
 
Anyway, Zawadi uliwahi kujiuliza kwa mwaka ni pesa kiasi gani zinazopotea kwenye mikono ya mafisadi wachache wa nchi hii?
Hizo pesa hazitoshi kuwasomesha vijana wetu?
Unajua TRA inapoteza Trilioni ngapi kwa mwaka kwa wakwepa kodi na watumishi wasio waadilifu?
Hizo pesa hazitoshi kusomesha vijana wetu?
Atleast basi ungeuliza yale maisha bora kwa kila Mtanzania yaliyoahidiwa na Jk 2005 yamefikia wapi?
 
CAMARADERIE acha Jazba. Kwanza hizo data za kodi ni za Kilimanjaro- ila nilipokopi chanzo nilikuwa nimepele kambele ukurasa. pato la Kigoma ni dogo zaidi.

Shule za kata, walimu hulipwa mishahara na nani? Tafadhali jibu swali hili ni muhimu sana katka kuendeleza mjadala

Bajeti ya taifa hutokana na kodi zikusanywazo mikoani na sio kuwa zinatoka mbinguni. Hivyo unapopiga bajeti yako (japo ni centralised) lakini ili kuwa mhalisia ni vyema uangalie kuwa umeingiza ngapi na umetumia ngapi. Ni lazima ujue na lazima uzingatie sana kuwa hizi pesa zinatoka kwanza mikoani kwenda makao makuu. Hivyo kama wewe ni mchumi mzuri ni vyema kuelewa kuwa ulipopewa pesa toka makao makuu umepata zaidi ya ulichoingiza au chini ya ulichoingiza. Pili, matumizi yako ni zaidi ya ulichoingiza au ni chini ya ulichoingiza. Hivyo ndivyo uchumi unavyokwenda.

Samahani hoja yako ya mwisho sijaielewa mantiki yake hivyo sitaijibu.

Mimi situmiagi jazba kujadili na watu....hata wawe wa aina ipi........nimejaribu kukuuliza nawe umeshindwa kunijibu......asante lakini kwa kujaribu nakupa 18% kama mwalimu wako
 
akili ya mtoa mada ni ndogo hata kuliko mbegu ya haradani! hujui elimu bure ni kitu cha kawaida kinachowezekana hapa tanzania???umesoma nini au kata product at work???misamaha ya kodi tena kwenye madini tukiamua tupunguze from 2.5% to 1.5% ni shiling ngapi tunapata???tayari ada ya mwaka kwa wanafunzi wote wa from primary to high school!wewe unapost vitu huna upeo navyo vizuri??ungeuliza ''chadema watafanyaje kutoa elimu bure'' then solution ungeziona hapa jammvini!hii nchi ni tajiri kuliko maelezo sema magamba ni wabovu kuliko maelezo'' itis very pocibo
 
I am very sorry for you Topical, because now I come to believe that you are an islam activist against other religions, especially christianity! I'm telling you my dear citizen, Israel will never fail against islamic terrorist and Palestine! It has been written in the Holly Bible and we all see it in reality!

Forget about fighting for your fellow islam rights that will never come true in this world or in the Paradise!

Believe in Jesus you will be Free! Jesus bless you!

wangeanza wale waliokamatwa na unga kuwa free kwani bado wanasota ndani
 
Wapendwa wadau wa JF wapenda maendeleo ya nchi yetu ya Tanzania natumaini ni wazima!!!
Tukikumbuka kwenye kampeini za uraisi 2010 Mheshimiwa Katibu MKuu Wa chama cha CHADEMA aliahidi kuwa akichaguliwa kuwa Raisi wa nchi ya Tanzania, serikali yake ITATOA ELIMU BURE kwa wanafunzi ngazi zote za elimu!!!! Watu wa CCM walipinga saana pamoja na wagombea wote vyama mbali mbali hasa ngombea wa CCM ambaye ni Raisi wetu kwa sasa!!!!! Lakini kwa kuangalia kwa uhalisi wa nchi yetu kulingana na mapato ya serikali jambo hili linawezekana kabisa!!!! Kwa tathimini za haraka tukiweza kuziba mianya ya kuvuja kwa mapato ya serikali jambo hili sio ndoto ni halisi:-
1. Tuanzie muundo wa serikali ni wa gharama kubwa saana kuendesha nchi tunayodai ni masikini. Kuna Mkuu wa Mkoa na maofisa lukuki kwenye ofisi za mkuu wa mkoa, ambao kazi zao zinaweza kuunganishwa ili kubana matumizi kama tunayo nia haswa ya kujikomboa kwenye umasikini. Mkoani kuna ofisi za Wizara mbali mbali, kwa nini kazi zao zisifanywe na maofisa wa mkuu wa mkoa.
2. Kuna Munispal Council kazi nyingi za Municipal zinaweza kuunganishwa ili Mji uweze kuwa uongozi mmoja (centralized leadership) hiyo itabana matumizi. Kwa nini uwe na meya na mkuu wa mkoa????
3. Utaratibu huo ukifuatwa hadi kwenye wilaya ni fedha nyingi zitaokolewa na kutumika kwenye miradi mingi ya maendeleo!!! Team kubwa za watendaji wakubwa wote wana mashangingi ya gharama kubwa ma v-8 na v-6, yanahitaji mafuta na maintenance ya hali ya juu. Hii ni kuanzia Mikoa, Wilaya, Municipal vitengo mbali mbali !!!!Kwa nini watumishi wasiendeshe Vitara au Escudo kubana matumizi ya mafuta na maintanance???
4. Vikao kwenye mikoa, wilaya na municipals watu hawafanyi kazi kwenye ofisi zao bali wanafanya kazi kwa vikao tuu, yote hiyo ni gharama kubwa kulipa allowances kila kikao!!
5. Kupunguza baraza la mawaziri wasio na tija kwa taifa, ukiondoa kuchagua watu kisiasa bali kitaaluma na kiuwajibikaji!!! At least ten ministries could be okay!!!
Gharama za kuendesha baraza la mawaziri ni kubwa mno!! Wakubwa wanaishi maisha ya ukwasi sana huku wakidai nchi ni masikini!!! Huo ni unafiki!!
Hapo hatujakusanya kodi kwenye migodi ya madini, viwanda, TANAPA, kwenye vyanzo na sehemu mbali mbali.
Tukifuta pia mikataba mibovu inayo tugharimu fedha nyingi k.m.SYMBION capacity charges Tshs 156,000,000/= kwa siku.IPTL and so on!!!!Inahitaji kujipanga kukomboa taifa hili toka mikononi mwa wachumia tumbo!!!!
Yako mambo mengi ambayo tukiyaacha na matumizi ya luxuriant huku tukijidai kuwa nchi yetu ni masikini kiunafiki, bila shaka lolote unaweza kulipia elimu kuanzia msingi hadi university bila shida yoyote na nchi ikaendelea kiuchumi!!!! Wakuu nawasilisha!!!
 
Linawezekana lakini kwa CCM ukisema hili watakwambia kuapanga ni kuchagua
 
inawezekana kutoa elimu bure angalia fedha ngapi zinapotea kwa ufisadi je hizi zisingetoa elimu bure?
 
Nimeshindwa kusoma thread yako maana lengo lako ni kutuharibu macho na hiyo milangi yako. kwani ukitumia maandishi ya kawaida ujumbe wako haufiki?
 
Naamini ilo linawezekana. Kwa taarifa yako tu, fedha zinazotumika kuwatibia viongozi wetu wakuu wanapoenda kubadilisha damu ulaya, ingetosha kabisa kuwasomesha vijana wetu.
 
very possible, mbona nchi zingine zinafanya hivyo? Shida ni wakuu wetu waangalia tu matumbo yao yasipungue...lakiini yatapungua tu siku moja....
 
Back
Top Bottom