Project funding sources

Heshima mbele wana JF,

Nimekuwa nahangaikia kupata habari au msaada wa mawazo kutoka sehemu mbalimbali nafikiri na hapa jamvini lazima kuna msaada mkubwa wa mchango naweza kupata kwani naamini hapa ni kitovu cha taaluma na ujuzi wa mambo.

Kwa muda mrefu sana nimekuwa nikifikiria na kutafuta njia mablimbali za kuweza kufanya sisi kama vijana wa kitanzania katika mambo ya kiuchumi (nikimaanisha kuwa na biashara kubwa) tunazoweza kuanzisha vijana na kutufanya kuondokana na mawazo ya kuajiriwa hasa kwa vijana wenye elimu ya chuo kikuu. Lakini ninasikitika sana kuona watanzania wengi tunagombea nafasi za kuajiriwa tu na serikali yetu haina msaada wowote wa kuwezesha kuleta mafanikio. Serikali yetu inatafafsiri ujasiriamali ni kumwezesha mtu kupata rizki, mi naamini bila viwanda vidogo vya kati huo ujasiriamali hautakuwa na manufaa yoyote, wazalishaji wanatakiwa wajue soko na processing ikifanyika thamani ya mazao yao inaongezeka kwenye masoko ya kimataifa.

Kwa mtazamo wangu nimekuwa nikiamini watu wenye elimu ya chuo kikuu wanatakiwa kuwa na mtazamo wa kuanzisha ajira kwani wao wamepevuka upeo tofauti na waliokosa elimu hiyo.

Kwa wanaJF wanaojua jinsi ya kupata resources jamani ninaomba msaada wa mawazo.

Nimefanya feasibility study kwa miaka kadhaa sasa na hatimaye nimeaandaa business plan ya kufanya processing ya cassava (mihogo) kutengeneza starch. Mali ghafi hakuna asiyejua inapatikana nchi kwetu popote pale unahitaji kuwahakikishia wakulima soko tu na watakufanyia mambo ya kutosha. Hii itainua uchumi wa wakulima wadogo sana na hasa kwenye maeneo ambayo kilimo cha pamba kimeanguka na mikoa kame kama ya kati isiyo na zao la biashara kwani popote inastawi

Soko lipo juu sana na lengo ku export tayari kuna watu wanahitaji sana kuimport kutoka Tanzania nimejaribu kutangaza na kupata response nzuri sana. Kuna soko kubwa sana nchini (yote inaagizwa toka nje esp SA) kuna soko kubwa sana pale TBL na viwanda vingine vinavyotengeneza madawa, nguo, bia, tambi, biscuits, noodles, almost viwanda vyote vinavyotengeneza vyakula (canned na bottled) vinahitaji starch.

Tatizo kubwa nililonalo ni kwamba natafuta source ya funds kuanzisha kamradi haka ambacho profit margin yake ipo juu sana. Nipo tayari kwa mazungumzo specific ya jinsi ya kufanya ili mradi niweze kutimiza hii ndoto. Mradi huu unaweza kuwa expanded katika muda wa miaka 2 au 3 ukawa na plant nyingine ya kuzalisha ethanol kwa kutumia waste materials baada ya kuprocess cassava na tayari nimeanza kudraft plan yake. Nimejaribu kupita Tanzania investment bank na kuongea nao wakawa na interest ya kusaidia ila nikawa sina colateral wala mdhamini mwenye assets nzuri (mimi mtoto wa mkulima tu hata elimu yangu ni ya kuungaunga tu) ninaweza kuraise kidogo tu. Nimepita na NBC ikawa vilevile tu na mradi unakubalika na tatizo siaminiki tu kwa vile sina historia ya kushika pesa kubwa.

Ninaweza kusimamia hii kazi na ikawa juu kiasi cha kuridhisha na kushindana na biashara kubwa tu hata kuanzisha zingine safi zaidi.

Haya wadau naomba reference kwenye source au tujiunege na kuona nini cha kufanya. Nipo kwa wazi nasikiliza mawazo yenu na ushauri! unaweza kuchangia au kuniPM vyovyote utakavyoona

Ahsanteni sana

Mzuzu,
Hilo ni wazo zuri sana.... nadhani umefika wakati sasa wa kuanzisha kitu kama THINK CLUB, ambapo watu wenye mitazamo inayofanana wanakutana at least twice a week kuwa na concerted thinking... akina Ford, Edson, etc walikuwa na kitu kinaitwa Master Mind na ndiyo maana walifanikiwa.... unfortunately huku kwenye forum tunaona majina ya ajabu ajabu tu labda ningelipendekeza kwa Administrator kukawa na facility ya kuwaunganisha members through e-mails... mfano kukawa na option ya kum e-mail mtu ambaye umekutana naye kwenye Forum na ukawa interested na line of thinking..
 
Wazo lako ni zuri sana,
Tayari mimi na baadhi ya wanajf tumeanza,matokeo yamekuwa mazuri. Kwa njia ya e-mail tulialikana,tukajulishana ukumbi na gharama,tukapeana muda wa jukwaa na tukakutana. Tunaweza.
 
Basi mimi nitajibanza mkuranga na naanza mwaka huu kwa kulima ekari 10 mihigo,wakati nawasubiri ngoja niwe natengeneza Crisps na mingine niwauzie kina mama wa Dar wanochoma na kukaanga mihogo.
Mkuranga would be more ideal if u plan to export ,ni karibu zaidi na bandari na pia barabara safi haina foleni ,pia TRL and TAZARA bado hawajajipanga still suffering from ufisadi and kubinafsisha crisiss

Nakubaliana na wewe mkuu, hatutaweza kuundoa unyonge wetu kwa kusema tu, tuende mbele kwa kuchukua hatua za kusonga zaidi. Tumesema sana sasa tutumie hizo potentials tunazoziongelea miaka yote jamani. Nipo tayari kukaa na kuangalia nini cha kufanya pamoja, tungeanza zamani haya mambo sidhani kama tusingeweza ku-run viwanda vyetu vilivyouzwa bei chee. siku zote nasema tufikirie mbali zaidi ya familia zetu, tuangalie mambo makubwa ya kubadilisha maisha ya watu na sio kufikiria kununua hiace na kujenga tu
 
Pamoja sana mkuu.
Kaza buti kaka. Kila taarifa unayokujanayo inatia moyo.
Naamini wakati ndio huu, hakuna kulala. Mpaka kieleweke.
 
Ndugu yangu huko kote nimepita na hakuna support yoyote ya maana unayoweza kupata kwa vyombo vyetu hivi zaidi ya kuvitumia kwa maslahi yao ya kisiasa tu. Unafikiri TIC ingekuwa inafanya kazi inayotakiwa wahisani wangekata hio fungu la misaada? Wawekezaji wanaoitwa wote wanalalamika rasimu uliopo kwa system ya utawala wa serikali yetu. Wanaofanikiwa haraka ni wale wanaotoa au kuahidi kitu kwa watendaji hivyo nakomaa tu kuangalia sources nyingine, na nashukukuru tayari nimempata mbia yupo tayari tufanye naye kazi tumeshaweka local Manager na tumesajiliwa as a company mambo yanasonga sasa

Siku moja nilitia timu pale TIC kwa matamanio kwamba kwa vile ni kijana basi nitapata support kubwa,kushangaa jamaa wakanigeuza dili. Baada ya kugundua kuwa wamenigeuza dili sijakanyaga tena,na kila wakinipigia nawaambia niko mkoani.
 
Hamna kitu pale ni siasa chafu, usanii na rushwa tupu! Usitegemee support ya serikali hii labda nyingine
 
Tatizo kubwa nililonalo ni kwamba natafuta source ya funds kuanzisha kamradi haka ambacho profit margin yake ipo juu sana. Nipo tayari kwa mazungumzo specific ya jinsi ya kufanya ili mradi niweze kutimiza hii ndoto. Mradi huu unaweza kuwa expanded katika muda wa miaka 2 au 3 ukawa na plant nyingine ya kuzalisha ethanol kwa kutumia waste materials baada ya kuprocess cassava na tayari nimeanza kudraft plan yake. Nimejaribu kupita Tanzania investment bank na kuongea nao wakawa na interest ya kusaidia ila nikawa sina colateral wala mdhamini mwenye assets nzuri (mimi mtoto wa mkulima tu hata elimu yangu ni ya kuungaunga tu) ninaweza kuraise kidogo tu. Nimepita na NBC ikawa vilevile tu na mradi unakubalika na tatizo siaminiki tu kwa vile sina historia ya kushika pesa kubwa.

Ninaweza kusimamia hii kazi na ikawa juu kiasi cha kuridhisha na kushindana na biashara kubwa tu hata kuanzisha zingine safi zaidi.

Haya wadau naomba reference kwenye source au tujiunege na kuona nini cha kufanya. Nipo kwa wazi nasikiliza mawazo yenu na ushauri! unaweza kuchangia au kuniPM vyovyote utakavyoona

Mzuzu,

Fund zipo nyingi za kutosha, zinakosa wachukuaji.
  • Funds zipo kama biashara yako ndiyo inaanza (Startup) au ni kukuza mtaji
  • Inakubalika haraka kama itakuwa katika mfumo wa cooperatives/association
  • Wanachama wa jinsia ya kike wawepo kwa wingi
  • Funds wanazotoa ni kuanzia $ 50,000 hadi $ 250,000 kwa mradi
Kama biashara yako ipo katika mfumo huo, angalia creteria zao hapa chini.

Criteria for financing applications

General information
  • Name and address of organisation
  • Continent, country and region, town or city of implementation
  • Date on which the organisation was founded
  • Type of organisation (association, foundation, ...)
Information about the organisation
  • Mission statement and objectives of the organisation
  • Views on political and socio-economic context (regional/local and national) and what kind of role your organisation plays in this
  • Organisation's position in local society (incl. collaboration with others)
  • Summary of the activities organised by the organisation if the proposed plan does not cover all of the organisation's activities
  • Organisational structure (incl. information about board and staff (gender specific))
  • Information about the way in which the target group is represented in the organisation
  • Planning, monitoring and evaluation system
  • Financial position, financial policy and financial management of the organisation (incl. existing sources of funding)
  • History and track record (what has the organisation done and achieved up until now)
Information about the plan of action for the coming period
  • Analysis of the existing situation, risks and opportunities in the working area in relation to the proposed plans
  • Characteristics, size and location of the intended target group (gender specific)
  • Long-term objectives of the plan of action (what kind of change do you ultimately hope to achieve in the situation of the target group)
  • Expected results at the end of this period
  • Strategy (how are the objectives to be achieved, how is sustainability safeguarded)
  • Start and end date of the proposed plan of action
  • Financial plan and financial policy for the period covered by the plan
  • Long-term budget broken down by activities (programmes/categories) per year in the local currency, including the contribution/financing requested from Bank and others
The request should be accompanied by the following:
  • Articles of Association/Charter of the organisation
  • Annual accounts for the last 2 years (if available or otherwise the most recent financial report) plus possibly auditor's reports for the last 2 years
  • References
Kama mahitaji wanayotaka wao hayana tatizo, funds zipo.
 
Heshima mbele wana JF,

Nimekuwa nahangaikia kupata habari au msaada wa mawazo kutoka sehemu mbalimbali nafikiri na hapa jamvini lazima kuna msaada mkubwa wa mchango naweza kupata kwani naamini hapa ni kitovu cha taaluma na ujuzi wa mambo.

Kwa muda mrefu sana nimekuwa nikifikiria na kutafuta njia mablimbali za kuweza kufanya sisi kama vijana wa kitanzania katika mambo ya kiuchumi (nikimaanisha kuwa na biashara kubwa) tunazoweza kuanzisha vijana na kutufanya kuondokana na mawazo ya kuajiriwa hasa kwa vijana wenye elimu ya chuo kikuu. Lakini ninasikitika sana kuona watanzania wengi tunagombea nafasi za kuajiriwa tu na serikali yetu haina msaada wowote wa kuwezesha kuleta mafanikio. Serikali yetu inatafafsiri ujasiriamali ni kumwezesha mtu kupata rizki, mi naamini bila viwanda vidogo vya kati huo ujasiriamali hautakuwa na manufaa yoyote, wazalishaji wanatakiwa wajue soko na processing ikifanyika thamani ya mazao yao inaongezeka kwenye masoko ya kimataifa.

Kwa mtazamo wangu nimekuwa nikiamini watu wenye elimu ya chuo kikuu wanatakiwa kuwa na mtazamo wa kuanzisha ajira kwani wao wamepevuka upeo tofauti na waliokosa elimu hiyo.

Kwa wanaJF wanaojua jinsi ya kupata resources jamani ninaomba msaada wa mawazo.

Nimefanya feasibility study kwa miaka kadhaa sasa na hatimaye nimeaandaa business plan ya kufanya processing ya cassava (mihogo) kutengeneza starch. Mali ghafi hakuna asiyejua inapatikana nchi kwetu popote pale unahitaji kuwahakikishia wakulima soko tu na watakufanyia mambo ya kutosha. Hii itainua uchumi wa wakulima wadogo sana na hasa kwenye maeneo ambayo kilimo cha pamba kimeanguka na mikoa kame kama ya kati isiyo na zao la biashara kwani popote inastawi

Soko lipo juu sana na lengo ku export tayari kuna watu wanahitaji sana kuimport kutoka Tanzania nimejaribu kutangaza na kupata response nzuri sana. Kuna soko kubwa sana nchini (yote inaagizwa toka nje esp SA) kuna soko kubwa sana pale TBL na viwanda vingine vinavyotengeneza madawa, nguo, bia, tambi, biscuits, noodles, almost viwanda vyote vinavyotengeneza vyakula (canned na bottled) vinahitaji starch.

Tatizo kubwa nililonalo ni kwamba natafuta source ya funds kuanzisha kamradi haka ambacho profit margin yake ipo juu sana. Nipo tayari kwa mazungumzo specific ya jinsi ya kufanya ili mradi niweze kutimiza hii ndoto. Mradi huu unaweza kuwa expanded katika muda wa miaka 2 au 3 ukawa na plant nyingine ya kuzalisha ethanol kwa kutumia waste materials baada ya kuprocess cassava na tayari nimeanza kudraft plan yake. Nimejaribu kupita Tanzania investment bank na kuongea nao wakawa na interest ya kusaidia ila nikawa sina colateral wala mdhamini mwenye assets nzuri (mimi mtoto wa mkulima tu hata elimu yangu ni ya kuungaunga tu) ninaweza kuraise kidogo tu. Nimepita na NBC ikawa vilevile tu na mradi unakubalika na tatizo siaminiki tu kwa vile sina historia ya kushika pesa kubwa.

Ninaweza kusimamia hii kazi na ikawa juu kiasi cha kuridhisha na kushindana na biashara kubwa tu hata kuanzisha zingine safi zaidi.

Haya wadau naomba reference kwenye source au tujiunege na kuona nini cha kufanya. Nipo kwa wazi nasikiliza mawazo yenu na ushauri! unaweza kuchangia au kuniPM vyovyote utakavyoona

Ahsanteni sana
Unafikiria kiwanda wakati mradi uko zaidi katika fikra. Cha kufanya ungeshirikiana na SIDO kubuni mtambo mdogo endapo biashara itatoka ndipo sasa ufikirie kulitafutia mtaji mkubwa. Angalau bidhaa iwe sokoni, iandikishwe (haki miliki), wateja wawepo; pengine hata baadhi ya wateja wanawezaingia ubia na wewe kufanikisha mradi huu
 
Dont worry mkuu, nimepata mbia mwenye uzoefu wa hii biashara na mambo yote ya kimsingi yanaendelea vyema. SIDO unayoiongelea wewe ya hivyo ilikwenda na Nyerere iliyopo sasa hivi ni ofisi chakavu tu na kilio cha hatuna pesa wala bajeti. Hii kitu nimeifanyia feasibility study na sio kukukurupuka tu mzee. Anayetambua hii biashara akiisoma project kwenye paper tu anakubali, hata hivyo hiki sio kiwanda tunaanza na factory ndogo kama pilot kama ulinisoma vizuri hapo nyuma. Kwa aina hii ya processing for viable project inatakiwa isiwe chini ya 0.5tonnes/hour sasa kwa level hiyo SIDO has nothing to do zaidi ya kushauri tu go ahead.

Mbia ndio mtejaa huyohuyo kama umesoma, anataka products anunue mwenyewe kama materials za kiwanda chake cha plastics so hii sio biashara kama ya daladala tulizozoea za kucopy na kupaste

Mzuzu songa mbele,kama jua limekuchomozea amka nalo. Pale SIDO pamechoka ile mbaya.
 
Mkuu nashukuru sana kwa kunitia moyo, watu wengine hawajui kwamba nilianza na vyombo vyote vya nyumbani ambavyo vinahusika moja kwa moja na hakuna cha maana nilichopata. Hakuna mamlaka hapo nyumbani inayohusika ambayo sijapita kupata mawazo na resources zao baadaye nikakata tamaa nikaja kwenye jamvi kupata kama kuna watu wana mchango. Nikatangaza BID na partner-up huko ndo nikaanza kupata angalau response za kutia moyo. BID nipo kwenye ushindani wa projects stage ya 2 na patner-up ndo nilipata wawekezaji wawili tukakaa na mmoja ndo hadi sasa keshawekeza si haba na sasa tumesajiliwa na kuweka ofisi, tunategemea msimu huu wakulima waanza kuona soko limekuja ili wazalishe zaidi na pia tutakuwa na micro-finance facility kwa mikopo midogo kwa wakulima baadaye tutatoa gurantee kwa wakulima wakubwa wanaotaka kufanya biashara na sisi

Tupo kwneye maznugumzo bado na nipo ughaibuni sasa kwa gharama za mwekezaji tunaplan zaidi on how to go ahead

Mgagaa na upwa hali wali mkavu.
 
Nashauri kiwanda kijengwe newala maana kule mihogo inalimwa kwa wingi na inastawi sana
 
nimesoma baadhi ya mabandiko hapa na kila napogusa naona kuwa hapa nchini hakuna msaada katika suala zima la kuwafadhili wajasiriamali. sasa nchi hii ipo kwa manufaa ya nani?
 
Mzuzu,

Hongera sana kwa ujasiri na kuthubutu ambavyo vimeleta mradi huo.

Hivi wadau kuPM ni kufanyaje? Nami ninataka kuwa PM watu kadhaa hapa waliochangia thread hii, ni namna fulani ya mawasiliano ya Ki JF?
Natanguliza heshima.
 
Mkuu je umeshapata eneo la kufanya huo mradi wako?maana sio mradi mdogo huo unahitaji eneo la kutosha,kama bado maeneo yapo kigamboni kupia mwasongwe unaweza kupata heka moja kwa laki na nusu kwa hiyo kama una nguvu unaunganisha heka mia moja,au hata mkuranga
 
Nimepata Mkuranga na tunazungumza na RUBADA kupata eka 4000 zaidi halafu tunataka kupromote kilimo so leongo ni kuleta soko la wakulima tungependa zaidi wakulima wabakin na maeneo yao ili wazalishe na kuinua vipato vyao. Shamba litakuwa ni kwa back up na mafunzo zaidi kwa wakulima. Kuchukua ardhi yao ni kuwaongezea umaskini badala ya kuwapunguzia

Mzuzu niko nawe,wakulima wetu wafundishwe na waendelee kumiliki ardhi zao za asili ili tuwasaidie kujikwamua kimaisha zaidi. Moto huo endelea nao mkuu,mbele yako kweupe.
 
Mzuzu, nimekuwa nakusoma sana. Muda ukiwadia basi ntakutafuta kwa jina lako haswa ili niangalie ni anga zipi nitaweza kuungana na wewe na kama sivyo basi nitakutafuta kama Mzuzu ili nijifunze wapi pa kuanzia. Naamini hutakuwa na choyo ili na mie nisaidie watu wangu wa Sikonge. Jenga tu Reli Mkuu, naamini hutakuwa na hiana wengine tukitumia RELI zako kuja kupita kukufuata huko uliko.

Kwa maana hii, niseme wazi kuwa tunakutakia kila la kheri. Tuko nawe hata kama hutuoni tukiweka maelezo hapa.
 
Mkuu kazana,na mimi nakazana upande wa pili huko huko mkuranga,ipo siku tutaonana uso kwa uso. Ushauri wangu wa bure,usiruhusu wanasiasa kukukaribia mkuu,ni waharibifu. Ila yule mama Mkurugenzi wa Wilaya ni poa sana mkuu,ukiweza kamuone mapema ili kama unahitaji lo lote la kimaendeleo ni bonge la msaada sana.:A S-key:
 
Huyu mama ndo tunafanya naye mkuu ni mzuri sana tunakwenda vizuri kaka! natumaini tutaonana uso kwa so muda si mrefu ila mkuu wewe ni mdau muhimu naweza kukutafuta very soon tunaplan kuongea na chama cha wakulima muda mfupi ujao na kuona jinsi ya kufanya nao kazi kama shughuli zako zipo Mkuranga tutaonana mapema

Poa mkuu,kwa sasa niko lindi na nitarudi dar mwishoni mwa mwaka. ila project zangu nafanyia hapo Mkuranga.
 
Back
Top Bottom