Profesa Maji Marefu afunguka: Wabunge wanawategemea Waganga wa Kienyeji, lakini huishia kuwadhihaki

DSN

JF-Expert Member
Feb 2, 2011
2,837
1,674
Mbunge Profesa Ngonyani aka Maji Malefu kafunguka kwa wabunge kuacha kuwatangazia jina baya waganga wa kienyeji baada ya kuwatumia kufanikisha ubunge wao,baada ya hapo uwachukulia vinginevyo.Wakati akisema hivyo sura za wabunge walio wengi walionekana dhahili kujua nini anamaanisha.

Naomba kuwasilisha ujumbe huu ni moja ya ujumbe muhimu sana kwa Taifa na hasa Wabunge wetu ambao wengi wetu wamekuwa wanafiki na kujifanya si washirika wa waganga wa kienyeji.

Nawsilisha.
 
Mbunge anayekwenda kwa jina la Profesa Majimarefu leo jioni hii amezua minong'ono ndani ya ukumbi wa Bunge baada ya kutamka wazi bila kumumunya maneno kuwa anawashangaa waheshimiwa wabunge kwa kuwadharau waganga wa jadi ilhali wao (wabunge) huwafuata wakati waganga wa kienyeji wakati kampeni ili 'wafanyiwe mambo' na kuibuka washindi ktk uchaguzi. "Baada ya uchaguzi wabunge huwaona waganga waliowafikisha hapo walipo kuwa si lolote si chochote" alisema na kuongeza "Naamini hakuna Mtanzania yoyote ambae hawajui waganga wa kienyeji hususan sisi tuliopo humu ndani". Baada ya kauli hiyo ndipo kulisikika minong'ono ambayo binafsi sikuelewa kama ni ya kukubaliana naye au kutofautiana naye! Aliyasema hayo alipokuwa akichangia mjadala wa bajeti ya wizara ya Vijana, Utamaduni na Michezo.
Chanzo: TBC kipindi cha kutoka Bungeni.
 
Bunge la safari hii ni drama tupu manake limesheni kila aina ya watu;
wafungwa=Rage
witch dr=Maji Mafupi
wachungaji=Lwakatare

Kazi ipo
 




nadhani emotions zimezidi kuwa high

mshafturu sasa hebu pateni commercial break kabla hamjaenda tarawehe
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom