Profesa Handlay Mwafwenga mwenye digrii Tisa achukua fomu ya Uspika wa Bunge. Anena mazito

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
84,035
142,131
Prof Mpoki Mafwega amechukua fomu ya kugombea Uspika wa bunge na kuahidi atashinda na kuweka historia mpya nchini kwani bunge siyo kwa ajili ya wanasiasa pekee.

Prof Mpoki amesema tokea mwaka 1954 wakati wa mkoloni hapajawahi kuwa na Spika wa bunge aliyetoka kwenye sekta ya Utumishi wa umma hivyo amechukua fomu ili kuhitimisha utamaduni huo.

 
Mzee Pius Msekwa alianza kazi kama katibu wa bunge. Katibu wa bunge ni mtumishi wa umma. Samuel Sitta aliwahi kuwa DG wa TIC kabla ya kuwa Spika; mfanyakazi wa TIC ni mtumishi wa umma Job Ndugai aliwahi kuwa mtumishi wa TANAPA, hii nayo ni taasisi ya umma.

Huyu profesa auze vision yake akiwa spika, atafanya nini na bunge ataliendeshaje ili maadui watatu umasikini, ujinga na maradhi viondoke kwa haraka.

Kuna adui mwingine ukosefu wa ajira na mitaji au dhamana ya kupata mitaji ili wawe sehemu ya kuzalisha kwa kutumia elimu na nishati waliyonayo.

Suala la Tz haijawahi kutoa spika ambae ni mtumishi wa umma ni nyepesi sana, kwani wapiga kura wa spika sio watumishi wa umma, na hata ingekuwa spika anachaguliwa na Watz wote, bado number ya watumishi wa umma ni ndogo sana kumfanya mgombea ashinde kiti cha uspika.

Otherwise, kulikuwa na hoja ya James Mbatia kwenda mahakamani kusimamisha mchakato wa kinyang'anyiro cha uspika kwa kuwa barua ya aliekuwa spika ilikuwa addressed kwa mamlaka nyingine na sio katibu wa bunge. Jim Mbatia kafikia wapi??
 
Naona CCM mmepanga makada wenu kila nyanja .

Yani hapo kapangwa ili aonekane mchakato ni wa usawa na kila mtu anayo nafasi ya kushinda kumbe watu wa CCM wana jina lao kibindoni tayari.

Hadi lini CCM mtaendelea kuona watanzania kuwa ni wajinga?

Kwa bunge hili la kijani tupu lisilo na mvuto hata haieleweki wengi wa wabunge wameingiaje hapo watu wahangaike nalo?
 
Sio tu kibondoni huenda hata tayari anao mhuri wa moto kuwa hana kizuizi Cha kuvuka🤔.ila Kwa kadiri ya weledi wa kitanzania.
 
Sitaki kuongeza chochote hebu msikilizeni wenyewe

View attachment 2077354

D36B54B4-95E5-4E8B-9856-8F9D4B41068D.jpeg
 
Back
Top Bottom