Elections 2010 Prof Shivji aiponda Kauli Mbiu ya Rais Kikwete

Kaulimbiu ni maneno tu. Kama yana busara tuyafanyie kazi. Kama hayana tuyapuuze tu.

Lakini kaulimbiu peke yake haiwezi kutuletea uhuru wa kweli na maendeleo. Wala kuiondoa CCM madarakani hakuta leta mabadiliko (Si Kenya waliiondoa KANU......). Kutimua mafisadi na kutaifisha mali zao sio solution ( Idd Amin alijaribu hili na matokeo tunayajua).

Uhuru wa kweli na maendeleo yatatoka kwa jasho, juhudi na akili za wananchi wenyewe. Haswa wale wananchi wa kawaida walio vijijini.
 
PJ.Asante sana kwa kunuisaidia kujibu hili baada ya kusoma post ya Muheza na Bulesi jibu langu lilkuwa ndo hilo..Naona hawaelewi maana ya kuandaa ilani wanafikiri ni kwenda Jangwani na kubwabwaja,Jangwani ni sehemu ya kubwabwaja na sio ya kutafakari kwa kina na kuandaa agenda..Big Up once again PJ kwa jibu lako.

GS,

Hata kama mlikuwa mnaandaaa ilani, hiyo mikutano ya vijana kufanywa kwenye mahoteli haileti taswira nzuri kabisa.

Onyesheni mfano kwamba mko tofauti na hawa viongozi wetu ambao wanatumia mamilioni kwenye mikutano na semina kwenye mahoteli makubwa huku wsananchi wanakosa hata mlo.

Watanzania tumerogwa kukimbilia mambo ambayo hayana maana na kuacha mambo na mikakati ya maana.

Vijana wa CCM wamepoteza mwelekeo hivyo hivyo tokea walipoaanza kuiga mambo ya viongozi wao; mambo ya kuandamana na wenye pesa na madaraka na kuitisha mikutano ya mamilioni ya pesa. Kama kuna pesa wasaidieni vijana waweze kujitegemea.
 
Gender Sensitive,
Nikwepe vipi na nimejibu swali?..Yes, I was among marchers on Saturday...
Mkuu mimi sina sababu la kulaumu pasipo kuona ilivyokuwa. Na ajabu ssijui mnataka kuonyesha kitu gani zaidi ya kuchukua Ujumbe wenyewe.

Waafrika tuko nyuma sana ktk maswala ya kulilia haki zetu, sisi ni Watumwa wa akili hata ktk maswala mazito yanayotuathiri kila siku..
Haya badala ya kujiuliza tukajipanga tunaanza kuulizana kama nilikuwepo..Hii akili kweli jamani?..
Nina hakika sasa kwamba CCM itatawala mielele..
Mkuu Mkandara,
Hapa naomba nikukosoe kidogo.
Hawa jamaa waliuliza kama ulikuwepo na kwa kusoma ile post yako jinsi ulivyolaumu ngozi nyeusi kwa uchungu mkubwa. Ilikuwa ni kama vile ni wewe tu kati ya weusi aliyekuwepo katika maandamano hayo na wengine hawaku turn up.
Ndio sababu lilikuja swali kwamba pamoja na kujua hilo, wewe pia kama ngozi nyeupe ulikuwepo? na je ulipojua kuna issue hii wewe binafsi ulifanya juhudi gani kupanga mikakati ili ngozi nyeusi tuhusike? maana hata kwa wazungu si kwamba walijikuta tu wako kwenye maandamano bali kuna watu walipanga na walioguswa wakashiriki.
Toa jibu je wewe ulikuwepo?
Na ngoja niongeze swali lingine je umejihusisha vipi ili na sisi ngozi nyeusi wengine tushiriki? Usikwepe maswali kwa kuendeleza lawama tu.
 
GS,

Vijana mnafanyia mikutano yenu hotelini? Enzi za ujana wetu hilo lisingeliwezekana, tungelienda Jangwani.

Muheza2007, umenena! Mimi nawashangaa sana vijana wa siku hizi wanadai kwamba wana uchungu na nchi yao na umaskini wake lakini wako tayari kwenda kuhudhuria mikutano kwenye mahoteli ya bei mbaya na inahudhuriwa na vijana wasomi na wale wengine akina mbumbu wakiachwa solemba. Hapo tayari vijana wameishabaguana.

Shivji kwa kudhamiria kwenda kuzungumzia Azimio la Arusha angelikataa kwenda kufanyia mkutano wa "Vijana" hotelini angedai mkutano uwe Jangwani lilipotangazwa azimio hilo wakati linazaliwa. Hhotelini si mahali pa kulizungumzia Azimio la Arusha lenye kaulimbiu ya Binadamu Wote ni Sawa na Afrika ni moja - inayodaiwa kwamba ni Kauli mbiu muhimu sana na yenye ku-inspire sana.
 
GS,

Vijana mnafanyia mikutano yenu hotelini? Enzi za ujana wenu hilo lisingeliwezekana, tungelienda Jangwani.
dah! yaani umeniwahi kweli. tena hoteli za kitalii kisha wanazungumzia kuhusu Tanzania tunayoitaka. Tanzania ya mahoteli ya kitalii? Tanzania ya wachache? au kuna vijana wengine ambao ni wengi waliwatuma kwenda kujadili? HAwa hawana tofauti na kauli mbiu za Jakaya. Wamwache na Shivji ajipumzikie
 
Mkuu,

Hapo kwenu, mbona na wewe ulikuwa unachungulia kwenye TV?

Sijakuona hapa chini japo barabarani!
Yawezekana kweli maanake watu kama nyie hamuwezi kuamini Mkandara ni tofauti nanyi..Pengine hata huamini Gender Sensitive alikuwa mkutanoni na Prof. Shivji!
sasa kama hukuniona yawezekana wewe ni kati ya wale Hooligans wanao protest na kuvunja maduka ambao hawakuwa ktk maandamano ila mjini kubomoa maduka na kuchoma magari ya Polisi ili mradi message yao imefika...

Maandamano yalikuwa shwari kabisa, ngozi ya **** wachache walikuwepo ni wanafunzi wa U of T na nadhani ni wawakilishi wa taasisi moja ya Ukimwi ndio niliowaona lakini hakuna organization wala Taasisi yoyote ya Afrika iliyokuwepo hata hao wanaoomba na kutegemea misaada huku wakilalamika na masharti ya IMF. It's shame!

Kifupi mkuu wangu kubishana haiwezi kusaidia na ndio tatizo la ngozi hi. yaani tunachukua muda wetu kubishana kitu ambacho kinatakiwa tuchukue hatua mara moja..Muhimu ni ujumbe wangu kwamba tusiwe na akili ya kitumwa jamani tujitokeze kuelezea matatizo yetu badala ya kila siku kumtegemea huruma ya Mzungu asiyeathirika na hawa G8 moja kwa moja...

Mkuu siku zote mimi niko wazi, nadhani ni mimi pekee hapa JF aliyeingia Chadema na kuwajulisheni siku ile ile nilopata Uanachama, mimi nakuja kwa jina langu, na mimi pia nimewaambia napoishi, kabila, dini na kwetu ni wapi.. Na hata ukitaka info yoyote ile iwe simu yangu au e-mail yangu mkuu nitakupa tuwasiliane..I'm down to earth kind a mamen, sii mtu wa kuficha ficha na hakuna mtu hapa JF aliyeweza kufanya hivyo kwa hiyo amini usiamini haiwezi kuondoa ukweli kwamba sisi bado kabisa tuna akili ya kitumwa na wanafiki..Na pengine ndipo Laana ya kutofanikiwa inapoanzia..
 
GS,

Hata kama mlikuwa mnaandaaa ilani, hiyo mikutano ya vijana kufanywa kwenye mahoteli haileti taswira nzuri kabisa.

Onyesheni mfano kwamba mko tofauti na hawa viongozi wetu ambao wanatumia mamilioni kwenye mikutano na semina kwenye mahoteli makubwa huku wsananchi wanakosa hata mlo.

Watanzania tumerogwa kukimbilia mambo ambayo hayana maana na kuacha mambo na mikakati ya maana.

Vijana wa CCM wamepoteza mwelekeo hivyo hivyo tokea walipoaanza kuiga mambo ya viongozi wao; mambo ya kuandamana na wenye pesa na madaraka na kuitisha mikutano ya mamilioni ya pesa. Kama kuna pesa wasaidieni vijana waweze kujitegemea.

Ubishi mwingine wala hauna maana.
Unafikiri kila kitu ni Jangwani tu,utaendaje Jangwani kama huna data.Lakini pili unafikiri kuwa Jangwni ndio kutatua matatizo,nani kakudanganya?ni wangapi wameenda Jangwani wamefanya nini kikubwa?
 
Yawezekana kweli maanake watu kama nyie hamuwezi kuamini Mkandara ni tofauti nanyi..Pengine hata huamini Gender Sensitive alikuwa mkutanoni na Prof. Shivji!
sasa kama hukuniona yawezekana wewe ni kati ya wale Hooligans wanao protest na kuvunja maduka ambao hawakuwa ktk maandamano ila mjini kubomoa maduka na kuchoma magari ya Polisi ili mradi message yao imefika...

Maandamano yalikuwa shwari kabisa, ngozi ya **** wachache walikuwepo ni wanafunzi wa U of T na nadhani ni wawakilishi wa taasisi moja ya Ukimwi ndio niliowaona lakini hakuna organization wala Taasisi yoyote ya Afrika iliyokuwepo hata hao wanaoomba na kutegemea misaada huku wakilalamika na masharti ya IMF. It's shame!

Kifupi mkuu wangu kubishana haiwezi kusaidia na ndio tatizo la ngozi hi. yaani tunachukua muda wetu kubishana kitu ambacho kinatakiwa tuchukue hatua mara moja..Muhimu ni ujumbe wangu kwamba tusiwe na akili ya kitumwa jamani tujitokeze kuelezea matatizo yetu badala ya kila siku kumtegemea huruma ya Mzungu asiyeathirika na hawa G8 moja kwa moja...

Mkuu siku zote mimi niko wazi, nadhani ni mimi pekee hapa JF aliyeingia Chadema na kuwajulisheni siku ile ile nilopata Uanachama, mimi nakuja kwa jina langu, na mimi pia nimewaambia napoishi, kabila, dini na kwetu ni wapi.. Na hata ukitaka info yoyote ile iwe simu yangu au e-mail yangu mkuu nitakupa tuwasiliane..I'm down to earth kind a mamen, sii mtu wa kuficha ficha na hakuna mtu hapa JF aliyeweza kufanya hivyo kwa hiyo amini usiamini haiwezi kuondoa ukweli kwamba sisi bado kabisa tuna akili ya kitumwa na wanafiki..Na pengine ndipo Laana ya kutofanikiwa inapoanzia..

Mkuu Mkandara nakubaliana na wewe kwa hoja zako za tangu awali.Nisichokubaliana na wewe ni kuhusu Prof Shivji kwenda kwenye maandamano.

Kwa uelewa wangu mdogo kuhusu Prof huyu ni kuwa yeye sio muuumini wa migomo hata kidogo hivyo sidhani kama angweza kushiriki kwenye mgomo moja kwa moja hata kama angekuwa nakubaliana na hoja za kufanya mgomo wowote ule.

Hivi kwa unavyomuona anaweza kuandamana kwenye mgomo kweli? Hivi umeshawahi kufanya analysis ya wanaogoma physically hapa Tanzania na kuangalia ni aina gani ya watu ambao huwa wanaandamana?
 
Ubishi mwingine wala hauna maana.
Unafikiri kila kitu ni Jangwani tu,utaendaje Jangwani kama huna data.Lakini pili unafikiri kuwa Jangwni ndio kutatua matatizo,nani kakudanganya?ni wangapi wameenda Jangwani wamefanya nini kikubwa?

Sawa GS,

Sio ubishi, nilikuwa natoa maoni yangu. mafanikio mema na mikutano ya mahotelini. Wanasema akili ni nywele na kila mtu ana zake.
 
Mkuu Mkandara nakubaliana na wewe kwa hoja zako za tangu awali.Nisichokubaliana na wewe ni kuhusu Prof Shivji kwenda kwenye maandamano.Kwa uelewa wangu mdogo kuhusu Prof huyu ni kuwa yeye sio muuumini wa migomo hata kidogo hivyo sidhani kama angweza kushiriki kwenye mgomo moja kwa moja hata kama angekuwa nakubaliana na hoja za kufanya mgomo wowote ule.Hivi kwa unavyomuona anaweza kuandamana kwenye mgomo kweli?hivi umeshwahi kufanya analysis ya wanaogoma physically hapa Tanzania na kuangalia ni aina gani ya watu ambao huwa wanaandamana?
Duh, kumbe ndio umenielewa Profesa ajiunge na maandamano.. hapana mkuu wangu sikusema hivyo. Nilichokisema kwake ni kuhusiana na yanayotokea nchini kwetu. Haya ya maandamano ni ktk kufikisha ujumbe jinsi waafirka tulivyokuwa nyuma kushiriki maswala ambayo yanatuhusu sisi moja kwa moja..

Nilitegemea sana watu kama Prof.Shivji kuwa msitari wa mbele ktk watu ambao wanapigania haki nchini kwa vitendo yaani yeye awe mtu wa mbele kuanzisha ama kuungana na watu wanaopinga Utawala mfumo mzima wa Kiutawala uliopo.

Nina hakika Upinzani ukipata watu kakma hawa pengine inawezekana lisilo wezekana kinyume cha hapo sioni kabisa Upinzani kufanikiwa ikiwa Upande wa Upinzani hakuna vichwa vya kutosha..Hizi habari za kuzngumzia magazetini hupita kama Upepo na ndicho sisi Waafrika tunakifanya yaani kila siku tunalalamika ktk magazeti na pembeni lakini inapofikia swala la kujitoa mhanga wengi wanaingia mitini..
 
Mwalimu Shivji nae anyamaze upepo upita kwanza, amechanwa chanwa kwenye hukumu ya mgombea binafsi maana alitaka kuleta visheria vya India Bongo.
 
aisee tuna kazi...anyway kufika tutafika ila
shivji sijawai mchambua kiivo ila kauli mbiu inayoongezeka "zaidi" mh!!!
 
Duh, kumbe ndio umenielewa Profesa ajiunge na maandamano.. hapana mkuu wangu sikusema hivyo. Nilichokisema kwake ni kuhusiana na yanayotokea nchini kwetu. Haya ya maandamano ni ktk kufikisha ujumbe jinsi waafirka tulivyokuwa nyuma kushiriki maswala ambayo yanatuhusu sisi moja kwa moja..

Nilitegemea sana watu kama Prof.Shivji kuwa msitari wa mbele ktk watu ambao wanapigania haki nchini kwa vitendo yaani yeye awe mtu wa mbele kuanzisha ama kuungana na watu wanaopinga Utawala mfumo mzima wa Kiutawala uliopo.

Nina hakika Upinzani ukipata watu kakma hawa pengine inawezekana lisilo wezekana kinyume cha hapo sioni kabisa Upinzani kufanikiwa ikiwa Upande wa Upinzani hakuna vichwa vya kutosha..Hizi habari za kuzngumzia magazetini hupita kama Upepo na ndicho sisi Waafrika tunakifanya yaani kila siku tunalalamika ktk magazeti na pembeni lakini inapofikia swala la kujitoa mhanga wengi wanaingia mitini..

Nimekupata sasa.....kumbe nilkuwa nimeenda chaka..
 
Profesa ana haki na kuwa na maoni yake lakini ukweli azimio la arusha lilishindwa kabisa kwani hata katika kipindi kile tulishindwa kujitosheleza kwa chakula na viwanda ambavyo tulitaifisha tulishindwa kuviendeleza kwa ufanisi na nchi hii ilikuwa inategemea misaada na mikopo kutoka nchi za skandinavia na benki ya dunia. Na hao pia ilifika mahala wakatuchoka. Kuhusu kauli mbiu ya chama cha JK hiyo ni kauli mbiu yao na si lazima itu-inspire wote na kama haina mvuto basi ni heri kwa upinzani.
 
Ubishi mwingine wala hauna maana.
Unafikiri kila kitu ni Jangwani tu,utaendaje Jangwani kama huna data.Lakini pili unafikiri kuwa Jangwni ndio kutatua matatizo,nani kakudanganya?ni wangapi wameenda Jangwani wamefanya nini kikubwa?

Hivi ile Malaria haikubaliki katika viwanja vya wazi pale ilimsaidiaje kijana wa kitanzania? GS si unajua kuna wengine lazima waseme ...Uhuru wa kuongea...wee kaza buti acha waseme
 
Mimi nadhani hii ngozi nyeusi ina manatizo sanaa. Leo hii hapa kwetu kuna maandamano makubwa sana ya kupinga malengo ya mikutano ya hawa vigogo wa G8 na G20 wanavyotutenda nchi maskini..Maajab ya Musssa hakuna ngozi nyeusi kabisaaa yaani kama wapo basi wanachungulia madirishani.

Imefika mimi kujiuliza, hivi ndivyo tunategemea mabadiliko yanaweza kuja kwetu ikiwa sisi wenyewe tunajificha majumbani mwetu tukisubiri wazungu waandamane on our behalf?...kisha kesho utasikia tukilalama kwa matusi yote..

Ni ushauri wangu tu Prof. Shivji kama unaweza kuyaona makosa kama haya kwa nini usiwe msitari wa mbele kuhamasisha wananchi ktk Upinzani badala yake ni kukosoa tu makosa mabyo tayari yamekwisha fanyika!. Uchaguzi mwezi wa 10 wewe umejjiandaa vipi kuwasaidia wananchi kukiondoa chama kinachowanyima haki zao za msingi!..

Change starts with you na siyo kumtegemea Prof.Shivji!!Kama umeona hayo yote,anza kuhamasisha kwa upande wako na ndio tutafikia mabadiliko yaliyo ya kweli.
 
Change starts with you na siyo kumtegemea Prof.Shivji!!Kama umeona hayo yote,anza kuhamasisha kwa upande wako na ndio tutafikia mabadiliko yaliyo ya kweli.
Duh! mkuu wangu nifanye nini zaidi unachokitaka?
 
Hivi ile Malaria haikubaliki katika viwanja vya wazi pale ilimsaidiaje kijana wa kitanzania? GS si unajua kuna wengine lazima waseme ...Uhuru wa kuongea...wee kaza buti acha waseme

Asante kwa kuleta hoja hii.Ngoja nikae sawa niichambue kwa mapana yake.
 
Profu eeeeh ni bora huyu kikwete angetuacha na maisha yetu yaleyale ya siku zote kuliko haya ya kwake ya maisha bora kwa kila mdanganyika ama kweli sisi watanzania tuna laana kama si laana basi tuna vichwa vigumu huyu jamaa kikweti hakuna alichofanya cha maana nashangazwa sana na ninasikitishwa na wa tz wanavyomiminika kumsikiliza mauongo yake na ahadi nyingi za chama cha chukua chako mapema yaani ccm ovyo kabisa siku hizi nikipita mitaa mbalimbali naona mabango kibao ya huyu mtalii rais yaani hasira zinanipanda sana natamani kuyachana kwani hayo mabango ya picha za huyu mtalii yametengenezwa kwa kutumia pesa za walipa kodi wa nchi hii ambao ni sisi yaaani nimechoka na chama hiki cha majambazi wasio na huruma na wananchi masikini kama mimi
 
Huyu Prof Issa G. Shivji anajifanya anatetea sana sera za Mwalimu, huku akiwa mpinzani mkubwa sana wa Muungano ambao Nyerere aliupigania hadi mauti yake!

Juzi hapa amekuwa champion wa ku-inspire Wazenj wamruhusu Karume kuendelea na uongozi baada ya muda wake kwisha bila hata kujali Katiba ya Jamhuri ya Muungano inasemaje! Amekuwa pia mtetezi wa Uzanzibari dhidi ya Bara au kwa kifupi, ubaguzi!

Soma vitabu vyake utaelewa ninasema nini! Amejifunika mwavuli eti kwamba anatetea mambo ya Azimio la Arusha, kumbe ni unafiki mtupu!

Mkuu, sio kweli kwamba Kutetea Azimio ndio atatetea kila kitu alichofanya Mwalimu, mimi bado sijaona unafiki wa Shivji hapa, kama Wazanzibar wana haki ya kuwa na nchi yao (Kwa mtazamo wake) basi ana haki ya kulisema hilo na wala sio kukaa kimya eti kwa sababu Nyerere alitetea Muungano
 
Back
Top Bottom