Elections 2010 Prof Shivji aiponda Kauli Mbiu ya Rais Kikwete

huyu prof issa g. Shivji anajifanya anatetea sana sera za mwalimu, huku akiwa mpinzani mkubwa sana wa muungano ambao nyerere aliupigania hadi mauti yake!

Juzi hapa amekuwa champion wa ku-inspire wazenj wamruhusu karume kuendelea na uongozi baada ya muda wake kwisha bila hata kujali katiba ya jamhuri ya muungano inasemaje! Amekuwa pia mtetezi wa uzanzibari dhidi ya bara au kwa kifupi, ubaguzi!

Soma vitabu vyake utaelewa ninasema nini! Amejifunika mwavuli eti kwamba anatetea mambo ya azimio la arusha, kumbe ni unafiki mtupu!
wewe(buchanan) ni mbaguzi na mdini mkubwa sana, hufai kuishi katika jamii ya watu waliostaarabika...... Ushindwe na ulegee!!!!...aamen
 
....asante sana Regia kwa taarifa nzuri ulotuletea...ubarikiwe
 
Japo lugha waliyotumia N-HANDSOME,BULESI NA MUHEZA sio nzuri ila hajo yao ina msingi sana. Kwa kweli wengi tuanahangaika kujenga hoja ya Kufufuliwa kwa Azimio la Arusha hivyo kwa kujifungia Peacock na Kempnski hatuwezi kufanikiwa. Nashauri wakati vyama vya siasa vinafanya kazi yao ni sisi wanaharakati wengine tusiotaka kujifungamanisha na vyama tuanzishe rasmi harakati za kudai kupitiwa upya kwa Azimio la Arusha kwa nia ya kurejeshwa kwake.

Tukiweza kujenga pressure ya kutosha kwa kuelimisha wananchi wengi iwezekanavyo kuhusu Azimio la Arusha, vyama vya siasa vitakuwa havina budi kuifanya kama sera yao
 
Kaulimbiu ni maneno tu. Kama yana busara tuyafanyie kazi. Kama hayana tuyapuuze tu.

Lakini kaulimbiu peke yake haiwezi kutuletea uhuru wa kweli na maendeleo. Wala kuiondoa CCM madarakani hakuta leta mabadiliko (Si Kenya waliiondoa KANU......). Kutimua mafisadi na kutaifisha mali zao sio solution ( Idd Amin alijaribu hili na matokeo tunayajua).

Uhuru wa kweli na maendeleo yatatoka kwa jasho, juhudi na akili za wananchi wenyewe. Haswa wale wananchi wa kawaida walio vijijini.
Naomba nitofautiane kidogo na wewe mkuu, Kauli mbiu inabeba lengo kuu na muelekeo mzima wa watu au organization. Kauli mbiu ndio inayokupa changamoto ya mikakati ya jinsi ya kufikia lengo la kauli mbiu. Mfano, 'Maisha bora kwa kila mtanzania' ingeweza kuwafanya CCM wafikirie na kuidentify setbacks za kutokuwepo maisha bora kwa kila mtanzania na kwamba only a few are benefitting from the sweats of the rest of Tanzanians. This will take them a little further and perhaps discover that there is massive corruption and mismanagement of public finances by those few, and in the end set some measures to stop this evil.
Pia unaconclude kuwa kuwaondoa CCM hakutaleta mabadiliko just because Kenya waliiondoa KANU na hakuna mabadiliko. Kwanza unafanya comparison ya 2 different countries ambazo zinaweza kuwa na tofauti kadhaa za kwa mfano ni watu wa aina gani wameingia madarakani afterwards, je ni wezi, wavivu, wasio na vision au ni watu wenye kutuletea mabadiliko ya kweli. So it depends tumebadilisha serikali tukaiweka serikali ipi. Na bado sikubaliani na wewe unapoisight Kenya kuwa ni mfano mbaya, already Kenya jana tu wamesign a new constitution ambayo ina mabadiliko mengi tu mazuri kwa maendeleo ya nchi yao, and that is to me, a positive move towards success.
La mwisho umetoa mfano wa Uganda na Idd Amin kuwafukuza wahindi. Nakubaliana na wewe kwamba hiyo haikuwa good move by any measure of standards. But today ukienda Uganda utashangaa kuona kuwa uchumi wa Uganda upo mikononi mwa indigenous, ukifika mjini unaona maduka makubwa sana na biashara kubwa tu za waganda wazawa unlike your country ambayo wewe ni shahidi ni akina nani wameshika huu uchumi.
 
Muda mfupi uliopita nimetoka kushiriki kwenye mdahalo wa kuandaa Agenda za Vijana za Tanzania tunayoitaka leo na baada ya uchaguzi kwa kifupi Ilani ya Vijana.

Mjadala huu uliandaliwa na Asasi ya Vijana ya TYVA na umefanyika katika Hotel ya Peacock Mnazi Mmoja Jijini Dar es salaam.Mgeni rasmi katika mdahalo huo alikuwa ni Professa Issa Shivji Mwenyekiti wa Kigoda cha Mwalimu Nyerere.

Katika ufunguzi wake kiongozi huyu machachari na mwenye uchungu wa dhati na nchi hii alisema mambo mengi lakini nitaleza machache yaliyonigusa sana.

Prof alisema kuwa Azimio la Arusha limesahaulika kabisa na alishangazwa sana mwaka 2007 amabpo azimio hili lilikuwa linatimiza miaka 40 lakini Serikali na watu wengine hawakuthubutu kulikumbuka lakini Serikali iliazimisha miaka 30 ya Chama Cha Mapinduzi.

Prof aliturudisha nyuma na kueleza kuwa Kauli Mbiu ya Azimio la Arusha ya Binadamu Wote ni Sawa na Afrika ni moja ni Kauli mbiu muhimu sana na yenye ku-inspire sana.

Akaponda kauli mbiu ya Maisha Bora kwa Kila Mtanzania kuwa hainspire wala haina mvuto badala yake inasababisha kila mmoja kuhangaika kivyake iwe kwa kula rushwa au kwa njia yeyote ile ilmradi tu afikie hayo maisha bora. Akasema Slogan hii ni ya kibaguzi inaleta matabaka.

Habari ndio hiyo.

Regia

Ningekuwa jimboni kwako HAKIKA ningekupigia kura, lakini nampigia kura Halima Mdee, kwani yuko jimboni mwangu - KAWE! People's Power!
 
Back
Top Bottom