Prof Peter Erlinder na kifo cha Prof Juani Mwaikusa

Stuxnet

JF-Expert Member
Feb 12, 2011
10,394
17,984
Prof Peter Erlinder ambaye ni wakili anayewatetea watuhumiwa wa mauaji ya kimbari ya Rwanda ya mwaka 1994. Ameomba kuwasilisha utetezi wake kwa wateja anaowawakilisha kwenye mahakama ya kimataifa ya Rwanda kwa kupitia picha za video yaani 'video conference'. Anasema usalama wake uko mashakani kama atakuwapo mahakamani Arusha kimwili kwa kuwa Serikali ya Rwanda inatekeleza mpango wa kuwaua watetezi wote wa watuhumiwa wa mauaji ya kimbari. Profesa Peter ambaye ni mwanasheria wa Kimarekani anasema hataki yampate yaliyompata mwanasheria mwenzie Profesa Juani Mwaikusa wa UDSM aliyeuawa kikatili nje ya nyumba yake mwaka jana. Ingawa sitaki kuingilia mchakato wa DCI na mahakama lakini nataka mdau mwenye details zaidi atujuze!
 
Je ni kitu gani kinaendelea baada ya kuwakamata hao paid assassins? Je ni nani wa kusemea huyu marehemu asiye na hatia? Au tukihoji sana ni kuingilia uhuru wa mahakama?
 
Du ni kweli baada ya kukamatwa hao watu.........sijasikia nini kimeendelea; tafadhali mtujuvye wenye taarifa, halafu pia ndo kwanza nasikia kuhusika kwa Marehemu profesa Juani na kesi ya mauaji ya kimbari ya Rwanda; Labda niseme tu kuwa kunaweza kuwa na ukweli ndani yake. Kwa kuwa nilipokuwapo huko huko last two years kulikuwa na mwendelezo wa watu kuuwawa kwa visasi hivi vya kutoleana ushahidi na kuanzia jan mpaka March 2009 watu wa 5 waliuwawa kwa kuwa mashahidi wa kesi za zile za Gacaca!
 
Mnacheza na kagame nini?!!!!!! Visasi huko Ruanda ni kwa kwebnda mbele!!!!!!! Hata wengine waliokuja kutoa ushahidi Arusha, wengine walipoteza kazi na wengine walipotea, hawajulikani walipo.....
 
Back
Top Bottom