BabaMorgan
JF-Expert Member
- Dec 18, 2017
- 4,141
- 10,872
Jana nimebahatika kuiona ikikatisha mitaa ya shaurimoyo kwa speed ile mi natangulia kufika Moro nikiwa na baiskeli yangu..Mkurugenzi wa shirika la reli nchini, Masanja Kadogosa amesema treni ya SGR itatumia saa moja na nusu kutoka DAR mpk Moro na itatumia msaa 3 kutoka DAR mpk Dodoma.
Ndipo waziri wa uchukuzi prof. Makame Mbarawa akasema "naomba wananchi waelewe hii treni siyo ya high speed kama zile za China na South Korea. Na hata ujenzi wa reli yake ni tofauti na hii ya kwetu ".
Source: ITV habari.
My take; Naona kama tumebadllishiwa gia angani. Mbona mwanzo tuliambiwa itakuwa treni ya mwendo kasi? Kama Dar mpk Moro ni saa moja na nusu, kuna haja gani ya kuitumia? Si ni bora watu waendelee kutumia IST ama Vitz zao tu?