Uchaguzi 2020 Prof. Lipumba: Tutasimamia kwa makini Sekta ya Kilimo na Maendeleo ya Viwanda

CUF Habari

JF-Expert Member
Dec 12, 2019
239
234
IMG_20200909_185931_646.jpg
"TUTASIMAMIA KWA MAKINI KATIKA SEKTA YA KILIMO NA MAENDELEO YA VIWANDA", PROF. LIPUMBA

Dira ya Mabadiliko ya CUF inakipa kilimo nafasi ya pekee katika mikakati ya kukuza uchumi na hivyo kuwaondolea umasikini wananchi wengi na hasa wa vijijini, na kuhakikisha Taifa linakuwa na chakula cha kutosha na ziada ya kuuza nje ya nchi.

Katika miaka mitano ijayo, bajeti ya sekta ya kilimo itakayoandaliwa na serikali ya umoja wa kitaifa chini ya CUF itakuwa kati ya asilimia 10-15 ya bajeti yote, na italenga katika kuimarisha maeneo yafuatayo:
  1. Utafiti na elimu kwa wakulima na huduma za ugani;
  2. Upatikanaji wa mbolea na pembejeo nyingine kwa bei nafuu;
  3. Kurahisisha upatikanaji wa zana za kilimo ikiwa ni pamoja na matrekta;
  4. Masoko ya uhakika ya ndani na nje ya nchi;
  5. Bei nzuri kwa wakulima;
  6. Kutengeneza barabara za vijijini; na
  7. Kusambaza umeme vijijini kwa kutumia nishati mbadala kama vile gesi iliyogunduliwa nchini, biogas inayotokana na mabaki ya mimea na vinyesi vya mifugo, jua na upepo.
Wakulima watahamasishwa kutumia TEHAMA kupata taarifa za masoko ya mazao na pembejeo, hali ya hewa na mafunzo ya kilimo bora. Dira ya mabadiliko ya CUF inakusudia kuasisi Mapinduzi ya kweli ya kilimo nchini, yatakayoongeza uzalishaji na tija kwa kuijenga upya sekta ya maendeleo ya viwanda.

Serikali ya umoja wa kitaifa chini ya CUF intaweka mkakati madhubuti wa kuanzisha na kuendeleza viwanda vinavyotumia malighafi ya ndani ya nchi na kuajiri watu wengi - kama vile viwanda vya nguo na mavazi, viatu na bidhaa za ngozi, vifaa vya matumizi ya nyumbani na vifaa vya umeme na electroniki.
 
CUF mmekosa mvuto sababu ya tamaa yenu ya kukubali kukiuza chama, ni ujinga ulio pitiliza leo kujifanya nyie ni wapinzani.

Lipumba kakimaliza chama kilichokuwa kinapendwa Tanzania mzima.
 
10 hours just five comments tena zote negative, mtajua maana ya usaliti wenu.
 
Back
Top Bottom