Nyamesocho
JF-Expert Member
- May 5, 2023
- 479
- 1,251
Maadhimisho ya miaka 62 ya Uhuru wa Tanzania Bara na utekelezaji wa dira ya maendeleo unaoishia 2025.
Kuna mengi yataelezwa leo pale ukumbi wa Jakaya Kikwete Dodoma mafanikio na changamoto kwa Dira ya maendeleo inayoishia 2025 na uzinduzi wa ukusanyaji wa maoni juu ya uundwaji wa Dira mpya ya maendeleo 2025-2050.
Dira ya maendeleo inayoishia 2025 serikali imejitahidi kwenye elimu na maji kwa asilimia 75 kufikia 2025 nadhani watakuwa wamefika asilimia 85,nyanja zingine bado sana.
Dira ya maendeleo 2025-2050 michango ni kama ifuatavyo:
1,Sekta ya kilimo bado sana,wakulima wengi wa nchi hii wanategemea kilimo cha jembe la mkono na mvua za msimu,Profesa Kitila hii ni aibu sana ,tunataka kufikia 2050 asiwepo mwananchi anayelima kwa jembe la mkono na msimu bali mashine na umwagiliaji na hapa ndo tatizo la ajira litapungua,vijana watapenda kilimo kuliko ilivyo sasa (Kilimo cha kijima hiki)
2,Viwanda bado sana na hii ni kutokana na kilimo cha kijima,boresha sekta ya kilimo automatically Viwanda vitakuja,wawekezaji watakuja wenyewe ikiwa kilimo kitaboreshwa ipasavyo.
3, Mazingira,tunataka kwenye Dira ya maendeleo 2025-2050 matumizi ya nishati mbadala yawe yamefikia asilimi 100,weka mkakati wa kila kaya kutumia gesi,umeme wa sola na kupunguza bei ya nishati hiyo ilingane na kuni na mkaa kama ilivyo mtaani katika matumizi ya kupikia ili kupunguza kiwango kikubwa cha kupikia mkaa na kuni ili kutunza mazingira.
4. Tuangalie pia population na rasilimali zilizopo kama vinaendana, watu wanazaliana kwa kasi lakini hatuoni mipango ya kuwawezesha watu hao kuajirika, tunaona vijana wengi wanakimbilia boda boda na jobless ni wengi sana mtaani hii ni hatari kwa usalama wa nchi.
5. Makazi ya watu bado ni duni sana,watu wanaishi kwenye nyumba za makuti, nyasi na tope, tunataka mkakati wa kuondoa makazi duni kwa kila Mtanzania kufikia 2050, mje na mkakati namna ya kuboresha makazi ya watu.
6. Matumizi ya ardhi bado sana, thamani ya ardhi kwenye hii nchi ipo chini sana, kasi ya upimaji ipo chini na ni gharama sana, na pia ondoa kipengele cha kwenye katiba kinachomilikisha ardhi ya nchi kwa Rais badala yake umiliki uwe kwa mwananchi moja kwa moja.
Ongezea mengine, Mheshimiwa Profesa Mkumbo atayaona.