Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 1,901
- 944
MBUNGE PROF. KITILA MKUMBO - MAARIFA YAPATIKANE KWA LUGHA MBILI & LUGHA ISIWE KIKWAZO KWENYE KUPATA ELIMU
Mbunge wa Jimbo la Ubungo, Dar es Salaam Mhe. Prof. Kitila Mkumbo akichangia hotuba ya bajeti ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia amesema ni muhimu maarifa yapatikane kwa lugha ya kingereza na Kiswahili na lugha isiwe kikwazo kwenye kupata Elimu katika mtaala mpya wa Elimu unaokuja.
"Namshukuru Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kuniahidi kuleta Chuo cha VETA kwenye Jimbo la Ubungo hususani Kata ya Makuburi ambayo ina idadi kubwa ya viwanda maana pale tuna kiwanda cha pili kwa ukubwa cha kutengeneza Nguo na kinaajiri watu zaidi ya 4000 na EPZA kubwa kuliko zote Tanzania" - Mhe. Prof. Kitila Mkumbo, Mbunge wa Jimbo la Ubungo
"Naunga mkono Sera inavyopendekeza kwamba lugha mbili zinatumika kufundisha Kiswahili kwenye ngazi ya chini na kingereza kwenye ngazi inayofuata. Mjadala huu tunaweza kujadili kwa kuzingatia Uzalendo wa Lugha, Utamaduni na Kuangalia Taaluma (Kupanua wigo kwa vijana na hali halisi)" - Mhe. Prof. Kitila Mkumbo
"Hali halisi ni makosa kudhani kingereza ni lugha ya wakoloni, waingereza wapo Milioni 67 lakini Duniani tuna watu Bilioni moja wanaotumia kingereza kama lugha ya kwanza. Kingereza kuwa lugha ya wakoloni kiliisha siku nyingi ndiyo maana kuna Kingereza cha West Africa, South Africa, Kenya, Canadian ni kuonyesha kuwa Kingereza kwenye lugha ya kikoloni kilishatoka zamani" - Mhe. Prof. Kitila Mkumbo
"Asilimia 53 ya Tovuti (Website) zote Duniani zinatumia lugha ya kingereza. Lugha zinazofuata ni chini ya Asilimia 10. Kichina ni asilimia 2, Kifaransa ni asilimia 4, Kirusi ni asilimia 6, Kijerumani ni asilimia 6, Kihispaniola ni asilimia 5 na Kireno ni asilimia 3. Lugha ya kingereza inaendelea kuwa lugha ya Taaluma na Biashara Duniani" - Mhe. Prof. Kitila Mkumbo
"Nchi 10 zenye mfumo bora wa Elimu Afrika; Seychelles ๐ธ๐จ, Mauritius ๐ฒ๐บ, Afrika Kusini, Botswana ๐ง๐ผ, Kenya ๐ฐ๐ช, CapeVede na Namibia ๐ณ๐ฆ nchi 7 zinatumia Kingereza kama lugha ya kufundishia na nchi tatu zinatumia kiarabu kufundishia hizi Algeria ๐ฉ๐ฟ, Tunisia ๐น๐ณ na Egypt ๐ช๐ฌ " - Mhe. Prof. Kitila Mkumbo
"Africa zinazosemekana kwa ubora wa Elimu ni Seychelles ๐ธ๐จ na Mauritius ๐ฒ๐บ na zinafana na Tanzania ๐น๐ฟ kwasababu wao wana lugha yao. Seychelles na Mauritius lugha yao ya Kitaifa ni Klior lakini lugha yao ya kufundishia ni Kingereza lakini ndiyo nchi ambazo tunazungumza zina ubora katika Elimu" - Mhe. Prof. Kitila Mkumbo
"Nchi 47 Duniani zinatumia Kingereza kama lugha ya kufundishia. Nchi 143 Duniani Kingereza ni somo la lazima. Takwimu za matokeo ya darasa la saba miaka 3 iliyopita ambayo tunatumia Kiswahili, Dar es Salaam shule 50 za juu zote zinatumia Kingereza kama lugha ya kufundishia ikiwemo Shule ya Msingi Olympio ya Serikali ambayo ni moja ya Shule za Serikali zinazotumia Kingereza" - Mhe. Prof. Kitila Mkumbo
"Hatuwezi kulaumu Kingereza kama ndiyo chanzo cha wanafunzi kushindwa kwasababu Shule za Msingi tunatumia Kiswahili lakini tafuta Shule 50 bora utakuta ni ambazo zinatumia kingereza" - Mhe. Prof. Kitila Mkumbo
"Tunapoandaa Mitaala tunaangalia sababu nyingi ambayo moja ya Msingi kuizingatia ni Matakwa ya Wazazi (Wazazi wanataka nini). Kabla Shule binafsi hazijapamba moto Tanzania, Watanzania wa Kati walikuwa wanapeleka watoto wao Kenya ๐ฐ๐ช na Uganda ๐บ๐ฌ, walikuwa hawafuati Elimu walikuwa wanafuata Kingereza" - Mhe. Prof. Kitila Mkumbo
"Utafiti katika ya mwaka 2015-2017 tuliuliza Wazazi, ungetaka watoto wako wafundishwe na lugha gani, Asilimia 63, Wazazi 6 mpaka 7 kati ya 10 walisema wanataka watoto wao wafundishwe kwa kingereza kuanzia Awali mpaka Chuo Kikuu. Utafiti wa mwaka 2022 unaonesha ni asilimia 70" - Mhe. Prof. Kitila Mkumbo
"Lugha ni nyenzo muhimu sana kwenye suala la Elimu. Ni muhimu watoto na walimu watumie lugha ambayo wanaijua lakini lugha huzaliwi nayo lugha unaipata kwenye mazingira. Tanzania kuna tatizo kubwa la lugha ya kingereza na Kiswahili " - Mhe. Prof. Kitila Mkumbo
"Jambo la Msingi, hutatui tatizo kwa kulikimbia, unalitatua kwa kulikabili. Tuna changamoto kubwa sana ya walimu kwenye somo la kingereza kwa idadi na ubora wao. Nchi zingine walikiri tatizo na wakaamua kufungulia milango" - Mhe. Prof. Kitila Mkumbo
"Tufungulie mipaka miaka 5 mpaka 10 waje walimu wa Kingereza kutoka ndani ya nchi za Afrika, wakati tunawapelekea Kiswahili tunakaribisha walimu wa kingereza, ndani ya Miaka 5 mpaka 10 tatizo hili litakuwa limeisha. Tuwekeze sana kwenye walimu wa somo la kingereza" - Mhe. Prof. Kitila Mkumbo
"Tunakipenda Kiswahili chetu, watoto wa kitanzania lazima wawe na kingereza kizuri na Kiswahili kizuri. Kitabu kitakuwa kwa lugha ya Kiswahili na kingereza na mitihani atapewa ya lugha ili ajibie lugha anayoweza kujibia. Muhimu ni kwamba maarifa yapatikane kwa lugha mbili Kiswahili na kingereza, na lugha isiwe kikwazo kwenye kupata Elimu" - Mhe. Prof. Kitila Mkumbo