Na ndio maana mwisho wa yote huaibika kwa laana! Unajua vile ni vitabu vitakatifu, kuapa kwa kuvinyanyua juu tena ukitamka "Ee Mwenyezi Mungu unisaidie" wakati mara baada ya kuvishusha chini unasahau na unatenda mambo kana kwamba hata yule aliyekuteua yuko likizo, matokeo yake ni AIBU kwa MADHAMBI unayokuwa umeyatenda! Tena nyingi ya nafasi za kuapa ni za Siasa, ambayo maana yake hasa ni "SI HASA". Sasa ya nini kutumia vitabu vya Mungu huku ukijua kuwa unachoenda kukifanya ni tofauti na kinyume na mapenzi ya Mungu? Ndio maana Baregu anajua hata kinachoenda kutendeka kwenye hiyo Tume ni USANII mtupu, Ndivyo Sivyo, na utapeli na hadaa kwa Umma. Kunyanyua vitabu vitakatifu ktk mizaha kama hii ni kukaribisha GHADHABU ya Mwenyezi Mungu!