kwa kufata process utahangaika sana. utaenda kuapa kwa mwanasheria, utapeleka barua ya mwajili, cheti cha kuzaliwa, barua ya balozi, alfu 50 ada, kama unaenda kusoma barua ya shule, passport size nne, unaenda kuapa mahakamani, mwishonimwishoni ndo unapelekwa fingerprint. baada ya hapo ndo utasubilia kama wiki tatu hivi. utaenda pale unasign unapewa pass yako. kama una hela ya bia nipm nikupe maelekezo vizuri la sivyo viatu vitaisha kwa safari za posta to kurasini kama upo dar.mbinga utabidi uje dar kwanza.
Kama unataka kupata hati ya kusafiria kwa ajili ya kwenda kusoma,unapaswa uwe na vitu vifuatavyo:
1. Cheti chako cha kuzaliwa,
2. Cheti cha kuzaliwa cha mmoja wa wazazi wako au affidavit,ambayo utengenezwa kwa wakili au hakimu,na kuilipia kati ya Tsh. 3000 hadi 5000,
3. Barua ya kupata admission ya huko unakoenda kusoma. Yaani barua ya mwaliko wa shule,
4. Vyeti vyako vya shule.
Pamoja na hayo,tafadhali fika kwenye ofisi ya uhamiaji iliyo karibu nawe ili uweze kupata maelezo zaidi. Andaa Tsh. 50,000 za malipo.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.