Yo Yo
JF-Expert Member
- May 31, 2008
- 11,217
- 1,706
Dr F. Ndugulile Dr hapa hajibu kitu......phuulizi Dr unaweza kutujibu wakazi wa Kigamboni ile ndioooooo uliokubali mpango wa kuwazikeni inafaida gani?Dr. kwenye zile ndiooooo yako haipo pale??? Kama haipo ule mpango wa kutenga bilioni moja kwa ajili ya wafu wewe unaona ni akili ya kawaida imetumika hapo??? Uliupinga vipi mpango wa kitoto kabisa ule???Kwa faida ya nani mlipitisha zile fedha??? Yaani mnaacha kupitisha fedha ili wananchi walio hai wafaidike, mnatenga fedha kwa ajili ya kuwanufaisha watu hata tusiowajua maana hatujui ni lini nyie viongoz wetu wa kitaifa mtakufa. Hii akili ya ajabu sana.
Unataka kusema Lukuvi akizikwa kwao Isimani hatotulia huko chini??? Mnataka kuongoza taifa hadi mkishakufa???? Yan what was exactly the motive behind that thing, ni kwa faida ya nani hasa???Mnataka kusema sasa kuwa maiti ya kiongozi wa ccm inathamani kubwa sana kuliko wananchi waliohai wanaoishi hilo eneo. Yani waache kuzitumia hekta zote hizo kwa maendeleo yao ili wasubirie Lukuvi afe azikwe hapo.
Sisi watumishi tunaumia sana maana ndio walipa kodi wakubwa nchini. Wafanyabiashara si serikali imeamua wasilipe kodi??? Sasa tutendeeni haki basi mbona hata hicho kidogo kinachopatikana mnakichezea tena????Naumia sana kuona kodi yangu inatumika kwenye kuwatengea eneo la kuwazika. Hivi kaka wewe ukizikwa Kigamboni itakuwaje hasa.
Hivi ni athari gani hasa ingetokea kama hizo 29 bilion zisingeunda hicho chombo mwaka huu, then hizo fedha zote zikasambaza maji Jimboni kwetu???Unataka kusema faida tutayoipata kwa kuanzisha hicho chombo inafar outweigh benefits za sisi wapigakura wenu kupata a basic need kama maji ya kunywa????Hebu vaeni viatu vyetu! Nadhan mnataka kutuambia kuwa hii ni price tunayopaswa kulipa au cost ni cost tunayopaswa kuincur kwa kuchagua kuongozwa badala ya kuongoza. Haina shida!!Ila si busara unapokula na kipofu ukamsika mkono.
Michango yako bungeni itakuwa na maana tu kama ina outputs kwa wananchi wako. Lakin kwa style ile ya kigamboni, kwa kweli ni hata aibu kusema kuwa kiongoz wa eneo lile ni msomi. Nadhan hamtuelezi ukweli ila inaonekana ni ngumu sana kuiongoza hii nchi. Nashauri tufanye one thing at a time ila kwa style hii ya kujifanya vyote twaweza. Itafika miaka 50 mingine tutabak hapa hapa.
Last edited by a moderator: