Precision Air Sasa Ni Kama Dala Dala?!. Ndege Yasubiri Abiria Uwanjani!.

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,468
113,583
Wanabodi,

Naomba kuanza na pongezi kama ishara ya appreciation kwa vile Tanzania ni kama hatuna flag carrier hivyo ni ukweli usiopingika kuwa Shirika la Ndege la Precision ndio linatubeba Tanzania kama taifa hadi nje ya mipaka yetu hivyo linastahili pongezi za dhati!.

Jina la Precision lina maana ya precise, ambapo siku za nyuma ni kweli walikuwa very precise, kwa sasa linaanza kubaki ni jina tuu, hakuna tena ile precise na sana sana ni mauswahili yanaanza!.

Kuna wakati nilisafiri kwa ndege za shirika hili zikiwa ndizo pekee zinazokwenda huko. Reporting time ni saa 1:00 asubuhi ndege inaruka saa 3:30.

Nilifika saa 2:30 ikiwa nimechelewa kwa saa nzima kabla ya take off, walinigomea kucheck in eti nimechelewa sana na wameshafunga check in counter!. Niliwagomea kuwa kwenye ticket tuneandikiwa kabisa, check in counter inafungwa 40 min before take off, saa hizi ni 60min before, how can they close?!. Nililalamika mpaka basi kwa vile kwa ndege za local, saa moja kabla ya take off bado ni reasonable, waligoma kata kata!.

Kwa vile safari yangu ilikuwa ni dharura sana, nilifanya nilichokifanya ila nili board bila boarding pass!. Nilipitaje hizo security clearance zote bila boarding pass, God Knows!.

Ndani ya ndege likatolewa tangazo kuna abiria mmoja amezidi hivyo ndege haiwezi kuruka mpaka kila mtu aonyeshe boarding pass yake tena!.

Within no time nikadakwa!. Nikaombwa kistaarabu nishuke kumpisha mwenye siti yake. Niligoma kata kata na kuonyesha tiketi na kueleza niligomewa check in kwa kisingizio nimechelewa!. Mimi ndio nilikuwa abiria wa mwisho nikaambiwa dirisha lineishafungwa, huyo abiria wa mwisho katoka wapi?. Na kwavile tiketi yangu was OK, this means seat yangu ingekuwa empty!. Nikawagomea kata kata kuwa sishuki!. Na nikaeleza tena kwa sauti ya hasira kuwa nimefika 60 min before nikakuta wamefunga counter kwasababu wamefanya over booking!.

Wakaita airport security nishushwe nikawagomea labda nguvu itumike!.

Ndege ilianza kuchelewa Capt akaamuru nifanyiwe security clearance, huyo abiria akapewa jump seat tukaruka!. Japo tuliruka huku nyuma muziki wake ulikuwa mkubwa kwa jinsi airport yetu ilivyo porous!. Waka issue arrest hivyo kufika tuu, nilifikia mikononi mwa polisi kwa hoja nirudishwe na the same flight kwenda kujibu mashitaka Dar.

Baada ya kueleza kilicho nipeleka nilikubaliwa kujidhamini kwa return tiket yangu ambayo ilikuwa nirudi kesho yake!.

Kilichofuata ni history... ila the bottom line, Precision Air ili kuwa kweli ni precise!. That was then!.

Now, jana jioni nilikuwa tena abiria wa Precision nikitokea KIA kuja Dar. Ndege hiyo ilikuwa internation flight ikitojea Entebbe hivyo ndani abiria wa mataifa mbalimbali.

Abiria wote tukiwa tumeboard tunaona ndege haiwashwi!. Baada ya kusubirishwa sana bila kuambiwa chochote ndipo tukaelezwa kuna abiria anasubiriwa!. Ndege iliwashwa ikabaki ikiunguruma kwa dakika 15 nyingine huyo abiria akisubiriwa!.

Hatimaye alifika na tukaanza safari. Angalau Capt. alituomba radhi kwa uchelewaji na kuahidi to make it up for the lost time kwa cruising speed na kweli tulifika almost on time japo tulichelewa kidogo!.

Nijuavyo mimi abiria wa ndege anayesubiriwa ni yule tuu aliyekwisha check in!. Hii ndio ile ndege niliokataliwa kucheck in 1-hour before kwa kuambiwa nimechelewa lakini leo abiria wote wanamesha board halafu wanamsubiria abiria fulani aliyechelewa reporting time hadi boarding time!.

Hii inamaa kumbe siku hizi counter haifungwi tena kwa wachelewaji!. Au kuna uwezekano huyo abiria aliyekuwa anasubiriwa was "somebody"!. Akina siye tukichekewa tunazuiliwa, akina wao wanasubiriwa!. What a double standards?!.

Japo walitutangazia good news za kuanzisha safari za Lusaka na Lubumbashi 3 times per week!. Jee kuna umuhimu kwa zile routes kama za Mwanza na Kilimanjaro ambazo zina abiria wengi hivyo wana peleka ndege mbili mbili hadi tatu at the same time, Jee Precision waongeza frequence ya "Dala Dala Flight" kama ndege za kwenda Zenj?. Ambapo ndege inapaki na kuweka wapiga debe ikijaa ndipo inaruka ili hiyo ndiyo iwe ndege yetu sisi waswahili badala ya kuwakerehesha abiria wao wa kimataifa kwa kuwasubirisha waswahili tunao chelewa?.

Tuwapongeze tena kwa kuzidi kukuwa na pongezi nyingine ni kuliendesha shirika kufuatana na hali halisi ya sisi Watanzania, we don't keep time!, sasa ni mpaka ndege zina subiria abiria kama daladala!.

I love Tanzania!

I love Precision Air!.

Mungu ibariki Tanzania!.

Pasco.
 
Mkuu Pasco pole sana lakini si unakumbuka kwenye kitabu cha animal farm kuna msemo wa "all animals are same but some more same than the others"
 
Halafu nauli zao bado ni kubwa sana na wanalipisha kwa dola ukifanya booking online hata kwa local flights. Kwa mfano nauli ya kutoka DAR kwenda Mwanza na kurudi ni USD 396.8, sawa na karibu Tshs. 635,000/= ni halali kweli hii kwa safari ya saa moja tu? Hii inakatisha tamaa watu kwa kweli.
 
Precision ni kweli uswahili ni mwingi kwa sasa hawako time sensitive kabisa. Majuzi nilikuwa niondoke na ndege ya saa 9;50 kuelekea Nairobi kutokea KIA cha kushangaza tumesubiri hadi saa 9:50 hakuna cha ndege wala nini mpaka saa 10 nanusu ndo ikaja kutokea Mwanza. Wakati mwingine wanakwambia ndege inaondoka saa 3.30 usipofanya double check up unakuta umeachwa. mfano mzuri ni safari za Mtwara Dar huwa ni kichefuchefu tupu
 
Kunasiku nilikua nimepata dharura ya kikazi na ninatakiwa niende Zanzibar ilikua yapata saa 8 za mchana, nikaenda ofisi zao hapa Arusha kununua Ticket wakaniambia ndege zimejaa labda niondoke kesho! Kuna jamaa yangu mmoja akaniambia jaribu kwenda uwanjani unaweza bahatisha ndege wanasema Last minute booking! Basi nikakodisha taxi dereva akanifikisha uwanja wa ndege nikasema wacha nibahatishe, kufika pale uwanjani nikaikuta ndege ileile ambayo ilikua iruke baada ya kama dakika 20, basi nikaingia uwanjani pale nikakuta wafanyakazi wa shirika hilohilo walioniambia kua ndege zimejaa kule Arusha, nikaomba kama naweza kupata nafasi moja, basi nikafanikiwa lakini chakunishangaza nilipocheck inn ndani ya ile ndege kuna nafasi ya abiria kama 8 ziko tupu na ndege ikaondoka hivyo hivyo!:shock:
 
hatuna jinsi air tz ndio hivo imefilisiwa na wachache,Kenya wametuacha mbali.
waandishi pigeni kelele hili fichueni uozo wote wa air tanzania na bado wameenda kuazima ndege Misri badala ya kununua hata boeing moja kubwa 737 au 747 kwa mkopo.
 
@Pasco

Nimewahi kuchelewa ndege uwanja wa Heathrow Uingereza nikiwa na ujumbe fulani na tulikuwa kama abiria 10 hivi kwa pamoja na tulijichanganya baada ya safari ndefu toka Miami na kubadili ndege pale London kuja Dar. Ilibidi BA itusubiri kwa zaidi ya nusu saa huku abiria wote wakiwa wameshaingia katika ndege na tulipoingia tulikuta wazungu wamenuna hadi wamekuwa wekundu lakini hatukujali maana cha muhimu ndege ilitusubiri ingawa sisi weusi.

Sometimes kusubiri abiria huwa ni kawaida kwa ndege zinazojua umuhimu wa wateja wao, usishangae hilo la KIA na Precision. Hilo la kwako wewe, hawakukutendea haki hata kidogo, walipaswa kukupa ruksa ku-check in walikuwa na muda wa kutosha.
 
Kaka Pasco,

Pole kwa masahibu, lakini nadhani una miss point, ile mara ya kwanza uliyochelewa ilikuwa kwa sababu wali over book (ni jambo la kawaida) hivyo abaria wao walipotimia na wale walio kwenye waiting list haraka wakafunga counter. Kwenye kadhia ya pili ni ndege ipo tupu kuna "vichwa" vinakuja kwa nini wasisubiri?
 
@Pasco

Nimewahi kuchelewa ndege uwanja wa Heathrow Uingereza nikiwa na ujumbe fulani na tulikuwa kama abiria 10 hivi kwa pamoja na tulijichanganya baada ya safari ndefu toka Miami na kubadili ndege pale London kuja Dar. Ilibidi BA itusubiri kwa zaidi ya nusu saa huku abiria wote wakiwa wameshaingia katika ndege na tulipoingia tulikuta wazungu wamenuna hadi wamekuwa wekundu lakini hatukujali maana cha muhimu ndege ilitusubiri ingawa sisi weusi.

Sometimes kusubiri abiria huwa ni kawaida kwa ndege zinazojua umuhimu wa wateja wao, usishangae hilo la KIA na Precision. Hilo la kwako wewe, hawakukutendea haki hata kidogo, walipaswa kukupa ruksa ku-check in walikuwa na muda wa kutosha.

Ndugu, kama ni international flight alafu abiria uko uwanjani tayari. Ni lazima wakusubiri, hata kama ni masaa kumi. Hii ni kutokana na sheria mpya za usarishaji wa ndege.

Miaka ya 90's terrorists walikuwa wanaatumia hii mbinu kuterekeza mizigo yao. Walijichelewesha ili ndege iondoke. Ili wenyewe wasiPande hiyo ndege.(Especial kwa connection flights) . Mara nyingi waliweka explosive materials inside their bags.

Kutokana na hii NTSB wali_order. Ndege haipaswi kupaa, hata kama ni abiria mmoja hayupo ndani ya ndege. Ikiwa mzigo wake, uko tayari kwenye ndege. Hii inaitwa luggage clearance.

So ndugu, ndo maana waliwasubiri. Hata kama masaa kumi. Either mizigo yenu Wangeishusha, alafu wao wakasepa (though ni usumbufu mkubwa, bora kuwasubiri)

Kwa refference zaidi fatilia air crash investigation cases. Utakutana na hii case, ninayo kuambia.

NoTe: kwa sheria za kucheck_in, abiria unatakiwa uwe airport 2 hrs kabla ya safari. Watakusubiri kama umesha_check in, na uko uwanjani (especial kwa connection flights, hii ni kutokana na usalama). Otherwise, kama huja_check in hupaswi kusubiriwa. Na niko kuruhusiwa kucheck_in jus 30 min before ya safari
 
Pole sana mkuu kwa masaibu hayo
Inauma sana pale kunapokuwa na double standards
Mie nilijua upo morocco mkuu
 
Sasa hili li-precision linaanza maroroso baada ya kutuuzia hisa zao?
Wengine tumezamisha tulichokuwa nacho tukidhani tunawekeza kwenye shirika makini, kumbe imekula kwetu. Inauma sana.
 
ndio mashirika yetu ya ndege hayo tena......mbona kuna mashirika kama Rwanda Air, BA, Kenya Airways, Ethiopian Airways yapo very decent and precise sasa hawa precision wasitake kujiharibia dakika hizi wakati ndio imekua kama kampuni mama ya Tanzania, coz kupoteza route ya ndege ni mara moja but kuirudisha it takes years.......na la mwisho kwa hawa mabwana wangefanya kujiwekeza kwenye soko la ndani zaidi hili washike route zote then route za nje zitatokana na kujiimarisha ndani ya Tanzania kwanza
 
@Pasco

Nimewahi kuchelewa ndege uwanja wa Heathrow Uingereza nikiwa na ujumbe fulani na tulikuwa kama abiria 10 hivi kwa pamoja na tulijichanganya baada ya safari ndefu toka Miami na kubadili ndege pale London kuja Dar. Ilibidi BA itusubiri kwa zaidi ya nusu saa huku abiria wote wakiwa wameshaingia katika ndege na tulipoingia tulikuta wazungu wamenuna hadi wamekuwa wekundu lakini hatukujali maana cha muhimu ndege ilitusubiri ingawa sisi weusi.

Sometimes kusubiri abiria huwa ni kawaida kwa ndege zinazojua umuhimu wa wateja wao, usishangae hilo la KIA na Precision. Hilo la kwako wewe, hawakukutendea haki hata kidogo, walipaswa kukupa ruksa ku-check in walikuwa na muda wa kutosha.
Never on earth, check the regulations of IIATA and it is specified that time is of utmost important since even the pilots are paid by the time they fly. However more assuring is that the air ticket is supposed to be durable for a year for an international flight, thus if you are late your ticket is still valid. Some flight they may charge u a small amount of money for the inconvenience caused. Otherwise, time for flying is time for flying since if you do not fly you may disturb others to land or take off.
 
Mkuu
Sikulazimishi kukubaliana nami lakini hivyo ndivyo ilivyotokea na BA ilitusubiri Heathrow kwa karibu saa nzima huku abiria wote wakiwa tayari kwenye ndege isipokuwa sisi tu na tulipofika tukaondoka. na kwa taarifa yako wakati BA ilipokuwa inafanya safari za usiku from dar to Joburg, tiketi ilikuwa lazima uitumie kwa siku husika na usiposafiri siku hiyo kwa kuchelewa bila kuahirisha mapema ilikuwa huwezi kusafiria tena tiketi hiyo hata iweje. lakini mashirika mengine ni tofauti. So inategemeana na shirika na shirika. Mie mteja mzuri wa BA that's why nakwambia kwa uzoefu wangu kwao
 
Halafu nauli zao bado ni kubwa sana na wanalipisha kwa dola ukifanya booking online hata kwa local flights. Kwa mfano nauli ya kutoka DAR kwenda Mwanza na kurudi ni USD 396.8, sawa na karibu Tshs. 635,000/= ni halali kweli hii kwa safari ya saa moja tu? Hii inakatisha tamaa watu kwa kweli.
Sisi ni kama tumelogwa. Nauli ya kutoka DAR kwenda BUKOBA kwa ndege ni kubwa kuliko kutoka London kwenda New York
 
Back
Top Bottom