PPF Group Endowment Saga: THE FINAL REPORT

Status
Not open for further replies.

Ripoti hii ina mambo yake na ina hoja zake. Kama nilivyoahidi, baada ya hii ni sabbatical ya muda mrefu kupumzika (details in the report). Enjoy na tuwashukuru wale wote ambao wameweka mikononi mwetu mambo mazito kama haya na kutufanya sisi wengine tuwe kama vipaza sauti tu na sauti zale wasio na sauti.

Nawashukuru milele wale mashujaa ambao mabegani mwao nasimama. Wale ambao kwa pamoja tumesafiri safari hii ambayo tuzo yake ni dharau na taji yake ni kisasi. Safari ambayo imejenga marafiki wengi wa kudumu maisha yote lakini pia imejenga maadui wa kudumu. Kwa marafiki zangu asante, kwa maadui mapambano dhidi ya utawala wenu mbovu wenye kutukuza ufisadi yanaendelea kwani mmetengeneza uadui wa kudumu kati yenu na mamilioni ya Watanzania. Sauti zetu na za wale watakaokuja nyuma yetu zitakaa juu yenu mpaka msalimu amri.

Unaposoma ripoti hii enjoy na fanya uamuzi wa kubadilisha kura yako.

Yote Kwa Utukufu Mkuu wa Mungu

BONYEZA HAPA KUPATA NAKALA YAKO - LIMITED EDITION

Ukichelewa, ukikosa, Usiulize iko wapi?
Shukrani nimeipata, UBARIKIWE.
 
Ahsante Mwanakijiji...

JK - hili swala huhitaji ushahidi mwingine zaidi ya report hii. Tafadhari chukua hatua ya kuwaonea huruma hawa watanzania maskini kwa kuanza kuwashughulikia hawa watuhumiwa. Wafute kazi, kisha ruhusu tume ya Bunge kama ile ya Richmond/Downs ifamie pale PPF kwa uchunguzi.

Inasikitisha sana kuwa nchi hii imefanywa "Shamba la Bibi" kama waswahili wasemavyo. Nchi inakuwa mahali pa watu kujichumia Pesa na kuanza mbele. Kwa hahika, siku zinahesabika.

sikuelewa vizuri maana ya "shamba la bibi" hadi nilipoanza kufuatilia jambo hili. Sasa najua. Kwa bibi kila mtu anakula atakavyo.
 
Eeeeh mungu, watoto wangu watakuta kitu kwenye nchi hii!!! mbona kila shirika/idara watu wanachota tu...
 
.......Na wale ambao hawana nafasi ya kula zaidi basi wanategemea ndugu zao au jamaa zao
kuweza kuwekwa katika nafasi za ulaji. PPF na sakata la malipo ya kutoka katika mfuko wa
shukrani baada ya ajira kwenda kwa kundi la viongozi wanaoendelea na ajira kwenye mfuko
huu ni mfano mmoja tu. Kuna maeneo mengi ambayo yamekuwa yakitumiwa katika taasisi
mbalimbali kutengeneza utajiri wa haraka haraka kwa kisingizio cha “kufuata taratibu”. Hili
tunaliona kuanzia Bungeni ambapo kikundi cha watu 350 hivi kinajiamulia bila kuhojiwa na
yeyote kujilipa chochote na wakati wowote kwa kisingizio chochote. Tunaona jambo hili hili
kwenye taasisi nyingine (Ikulu ikiwemo) ambapo watu wako tayari kutumia fedha za umma
kwa kisingizio chochote bila kuhojiwa na yeyote. Watanzania kwa mamilioni wakitamania
nao wao zamu yao ije.
.......

Kwa mwendo huu hatufiki!
 
Ningependa kweli kujua wenye uchungu na posho za kina Slaa wako upande gani katika hili. Somebody got any idea?
 
Ningependa kweli kujua wenye uchungu na posho za kina Slaa wako upande gani katika hili. Somebody got any idea?
Wewe mchokozi anyway ufisadi ni ufisadi haujalishi ni upande gani wa sarafu upo. Shukrani nitaisoma baadae na kurudi ila kwa angalizo la juu juu naona mwanga wa kuanguka kwa uchumi wa Tanzania kama hatua mathubuti hazijachukuliwa kudhibiti madudu kama haya.
 
Ningependa kweli kujua wenye uchungu na posho za kina Slaa wako upande gani katika hili. Somebody got any idea?

Mwanakijiji Issue sio posho za akina Dr. Slaa pekee yake, ni watu wote nchi hii wakipata nafasi husau shida walizonazo WATANZANIA wengi Vijijini na Mijini na kujikumbuka wao wenyewe tu, angalia kipata wapatacho Waheshimiwa Wabunge, Mawazili, Wakurugenzi na watumishi wengine ambao POSHO kwao ndio maisha yao ya kila siku. Wako hapo kupindisha taratibu au kuibua taratibu mpya na kuihalalisha na kuifanya iaminiwe na Jamii kama ni kawaida tu. (Business as usual)
Tumepoteza mwelekeo kama TAIFA, na Taifa tunalolijenga ni Taifa la ajabu sana duniani hapa, Maendeleo tutayaona tu yakipita na Nchi jirani zetu watakuwa wakisonga mbele sie tunabakia kulalamika tu. Ooooh, Serikali haitujali, kama sie hatutachukua hatua mapema tukawaachia watu kama hawa ndio wawe waamuzi wa HATMA ya maisha yetu siku zote, sie wanyonge mie na wewe Janga la Umaskini litatumaliza.
Cha Mwisho Ndugu yangu Mwanakijiji, nitasikitika sana kama utautoa mchango wako (withdraw your contribution on the fight againist corruption) kwa kutokutuandikia makala kama hizi ili mie na wale tusioweza kuandika katika lugha nyepesi watanzania wakaielewa. kama nimekupa vizuri pale mwanzo umedokeza hilo. Nitasikitika sanaa tena sanaaa, najua utakuwa hujalitendea haki Taifa hili (you will be a hypocrite), utakuwa msaliti mkubwa kwa vizazi vijavyo. Kumbuka maneno ya Mahatma Gadhi - India mpaka siku anauwawa hakuacha kuwakomboa watu wake kifkra - wewe unaita FIKRA PEVU.
 
MM

Shikamoo!!

Kazi umeifanya ni nzuri, tusubiri walifanyie kazi.

NYONGEZA:

Mwishoni mwa March 2008 ndipo walipolipwa hayo magolden shakehand ya uizi kwa kisingizio cha mwisho wa ajira/mkataba. Mwezi wa nne, mmoja wao Bwana Baduru Msangi alilipwa milioni 36 kama LONG SERVICE AWARD ya kutimiza miaka 35 NIC-PPF. Kama ajira ilikoma March, 2008 na bodi ya PPF iliridhia, inakuwa je huyu aliyepewa mkataba mpya akapewa long service award. This rabish and uizi. Erio Ajibu hizi hoja hapa.

Ripoti hii ina mambo yake na ina hoja zake. Kama nilivyoahidi, baada ya hii ni sabbatical ya muda mrefu kupumzika (details in the report). Enjoy na tuwashukuru wale wote ambao wameweka mikononi mwetu mambo mazito kama haya na kutufanya sisi wengine tuwe kama vipaza sauti tu na sauti zale wasio na sauti.

Nawashukuru milele wale mashujaa ambao mabegani mwao nasimama. Wale ambao kwa pamoja tumesafiri safari hii ambayo tuzo yake ni dharau na taji yake ni kisasi. Safari ambayo imejenga marafiki wengi wa kudumu maisha yote lakini pia imejenga maadui wa kudumu. Kwa marafiki zangu asante, kwa maadui mapambano dhidi ya utawala wenu mbovu wenye kutukuza ufisadi yanaendelea kwani mmetengeneza uadui wa kudumu kati yenu na mamilioni ya Watanzania. Sauti zetu na za wale watakaokuja nyuma yetu zitakaa juu yenu mpaka msalimu amri.

Unaposoma ripoti hii enjoy na fanya uamuzi wa kubadilisha kura yako.

Yote Kwa Utukufu Mkuu wa Mungu

BONYEZA HAPA KUPATA NAKALA YAKO - LIMITED EDITION

Ukichelewa, ukikosa, Usiulize iko wapi?
 
Nadhani hapa ni suala la chama cha wafanyakazi PPF ndicho kinatakiwa kioneshe njia. Wanasiasa hawaliwezi hili.
 
Ripoti hii ina mambo yake na ina hoja zake. Kama nilivyoahidi, baada ya hii ni sabbatical ya muda mrefu kupumzika (details in the report). Enjoy na tuwashukuru wale wote ambao wameweka mikononi mwetu mambo mazito kama haya na kutufanya sisi wengine tuwe kama vipaza sauti tu na sauti zale wasio na sauti.

Nawashukuru milele wale mashujaa ambao mabegani mwao nasimama. Wale ambao kwa pamoja tumesafiri safari hii ambayo tuzo yake ni dharau na taji yake ni kisasi. Safari ambayo imejenga marafiki wengi wa kudumu maisha yote lakini pia imejenga maadui wa kudumu. Kwa marafiki zangu asante, kwa maadui mapambano dhidi ya utawala wenu mbovu wenye kutukuza ufisadi yanaendelea kwani mmetengeneza uadui wa kudumu kati yenu na mamilioni ya Watanzania. Sauti zetu na za wale watakaokuja nyuma yetu zitakaa juu yenu mpaka msalimu amri.

Unaposoma ripoti hii enjoy na fanya uamuzi wa kubadilisha kura yako.

Yote Kwa Utukufu Mkuu wa Mungu

BONYEZA HAPA KUPATA NAKALA YAKO - LIMITED EDITION

Ukichelewa, ukikosa, Usiulize iko wapi?

Nani kama MM,

Kwa kweli nimesoma hii attachment sina maneno kama kweli PCCB, tume ya maadili na usalama wa taifa na serikali ipo hai basi overhall ppf nzima ya dada asia aka erio
 
Ok MMM, i hope with this document Hosea atasema vijana wake hawaoni issue hapo na mkulo atasema wewe mzushi

Tanzania bwana, si shamba la bibi tena ni kitu ingine kabisa

tunaishi kama tumbili!!:A S 100:
 
Thanks mwanakiji for critical analysis of various issue for the best of many Tanzanians.
 
hivi hawa wakurugenzi bado wako hapo PPF wanafanya kazi kama kawaida? PCCB mko wapi? nchi hii kweli wajinga ndo waliwao!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom