Power Breakfast (Clouds FM) wawapasha TANESCO!

Ivi tanzania ni dar peke yake?
Mbona apa songea hakuna umeme miaka yote ni migao ni kila siku, na hatujawahi kuona inajadiliwa mahali popote?

Ama kweli ilala ndo Tanzania na Kinondoni ndio Dar.


Ama kweli ulicho kisema ndio kila nitoapo michango yangu hata hapo PB Clouds FM huwa nauliza mbona JK na serikali yake kila maendeleo yoyote yana anzia DAR na katiba wameivunja kwani makao makuu ya nchi ni DODOMA hata mipango ya kuhamia DODOMA hawajafikilia sasa o haya siwaelewi ila kweli Kuto kufanya mabadiliko itatughalimu sana sie watanzania ndio haya sasa tuyajua kuwa KATIBA ya nchi ikibadilika kweli serikali yetu itakuwa makini sana katika uwajibikaji na utekelezaji na kuwa na wabunge wengi wa upinzani nyie mumejionea CCM wasivyopenda maendeleo waka mtoa SITTA uspika na kuweka watu wao Ana & Job ili wakidhi matakwa yao na sio ya wananchi jamani nchi inaongozwa na CCM au na serikali UCCM unatokea wapi??

 
Wana JF,

Kuna wakati tukisema TANESCO ni wazembe katka swala la uwajibikaji check wanakuambia atio transformer imekufa na waseme ni aina gani ya transformer iliyo kufa, Kumbukeni Arusha Pale kua kiwanda kina itwa Tanelec Limited (Tanelec Limited) ni maarufu kwa utengenezaji wa transformer na ziko Company mbili tu Afrika kama sijakosea na nyingine iko S.Africa.

Napatwa na kigugumizi sana na board nzima ya Tanesco kushindwa kununua hizo Transformer tokea pale Arusha na kuwahudumia watanzania wanao kubwa na matatizo ya kutokuwa na transformer maeneo yao.
 
Nakubali kutokubali hoja ya kuwa TANESCO wameshindwa kazi. Tatizo hapa si TANESCO pekee na watendaji wote...tatizo ni Wizara ya Nishati na Madini ambayo ipo chini ya Serikali ya CCM.Je,Clouds FM walipitia sera ya Nishati na Madini ya mwaka 2003 na kuhoji uadilifu na utekelezaji wake?.Inashangaza watu kulaumu tatizo bila ya kutafuta chanzo cha tatizo.Mimi nadhani tungepaswa kujiuliza ni kwanini tuna kampuni MOJA ya kusambaza umeme kabla ya kulaumu. Yanayopigiwa kelele TANESCO yapo kila idara ya kazi serikalini na makampuni binafsi.Tufikie mahali tukubali tunahitaji mabadiliko ya mfumo mzima.Nitamuelewa mtu atakayetoa mapendekezo ya kuiboresha TANESCO badala ya kulaumu.Nawadharau wanaodharau taalumu za watu, ni wajinga.
 
Kwa kweli hata mimi nimeipenda labda hawa jamaa wataamka... tumechoshwa na huu umeme wa kukatika katika bana....
 
Kigogo aiingizia Tanesco hasara ya mamilioni
Leon Bahati

UJEURI wa kigogo mmoja ndani ya Shirika la Umeme (Tanesco) wa kutosikiliza mafundi wake, umesababisha transfoma kubwa inayofanya kazi katika njia kubwa ya umeme wa gridi ya taifa, kituo cha Kipawa kuungua, Mwananchi limebaini.Kuungua kwa transfoma hiyo kumesababisha wakazi wa mkoa wa Dar es Saalam kuingia katika mgawo wa umeme wa lazima wa saa nne hadi sita kila siku na ambao Tanesco imesema utadumu kwa wiki tatu.

Mgawo huo unaelezewa umeisababishia Tanesco hasara inayokadiriwa kufikia Sh 1 bilioni, kutokana na gharama za kuagiza transfoma nyingine pamoja na makusanyo ya fedha ambayo shirika hilo litayakosa kutoka kwa watumiaji umeme viwandani na makazi ya watu kutokana na mgawo huo.

Habari zilizolifikia gazeti hili kutoka ndani ya Tanesco zimeeleza kwamba kigogo huyo alitoa amri ya kuruhusu umeme kwa msongo mkubwa kuzidi uwezo wa transfoma hiyo, licha ya tahadhari iliyotolewa na mafundi.
Msemaji wa Tanesco, Badra Masoud alithibitisha kuharibika kwa transfoma hiyo yenye uwezo wa kudhibiti umeme wa msongo wa megavolti Ampaya (MVA) 45.

Ingawa msemaji huyo alisisitiza kwamba kuharibika kwa transfoma hiyo ni hitilafu ya kawaida, habari za kuaminika zimeeleza kuwa ni uzembe wa kigogo huyo mwenye taaluma ya uhandisi wa umeme.
Kulingana na habari hizo za ndani ya Tanesco, kigogo huyo ambaye jina tunalihifadhi, wiki iliyopita alitoa amri kwamba mafundi warekebishe transfoma hiyo ifanye kazi kwa kiwango cha juu ili kuondoa matatizo ya umeme yaliyokuwepo katika baadhi ya maeneo jijini Dar es Salaam.

"Aliambiwa na mafundi wake kwamba kufanya hivyo ni hatari kwa sababu transfoma hiyo ni chakavu na baadhi ya vifaa vya kinga dhidi ya hitilafu vimeondolewa," kilieleza chanzo hicho.
"Lakini … (kigogo) huyo alishikilia msimamo kwamba watekeleze amri hiyo. Mafundi walifanya marekebisho hayo Ijumaa (wiki iliyopita) na siku iliyofuata, yaani Jumamosi transfoma hiyo ikalipuka na kuungua."
Chanzo hicho kilieleza kwamba kulipuka kwa transfoma hiyo kulitokana na umeme uliopo katika gridi ya taifa kuwa na kawaida ya kuongezeka na kupungua.

"Unajua umeme wetu haueleweki. Una tabia ya kuongezeka na kupungua. Sasa hali hiyo ilisababisha transfoma hiyo kuzidiwa nguvu na kuungua," kilieleza chanzo hicho.
Chanzo hicho kilisema: "Unajua bosi huyu ni mtu asiyeshaurika. Ni jeuri; ana taaluma ya uinjinia wa umeme, lakini mafundi wanaofanya kazi na transfoma hizo ndio wanaozijua kuliko yeye."
Chanzo hicho kilieleza kwamba transfoma hiyo ni chakavu, lakini pia baadhi ya vifaa vya kuilinda na hitilafu ya umeme vimeondolewa.

Kilieleza kwamba vifaa hivyo viliondolewa na baadhi ya mafundi kutokana na amri ya vigogo wa kigeni waliokuwa wanasimamia Tanesco miaka ya nyuma.
"Kuanzia hapo transfoma hiyo, imekuwa ikifanya kazi kwa kiwango cha chini kwa sababu ya mapungufu hayo ya vifaa hivyo vya protection (kuilinda na hitilafu)," kilisema chanzo hicho.
Baada ya tukio hilo, chanzo hicho kilieleza kwamba kigogo huyo alikataa kwenda kutembelea kituo cha Kipawa licha ya wenzake kwenda na kushauriana na mafundi.

Mwananchi lilipowasiliana na Badra, alimtetea kigogo huyo akisema kwamba hahusiki na kwamba hitilafu hiyo ni ya kawaida.

"Transfoma kama hiyo iliwahi kuungua Mbeya. Kwani nani alihusika… Hii ni hitilafu ya kawaida tu, hakuna mkono wa mtu. Huo ni uzushi," alieleza Badra.
Badra alisema kwa sasa Tanesco ipo katika mkakati wa kuweka Transfoma nyingine ili kuepuka hasara inayoendelea kulikumba shirika hilo.
Msemaji huyo alishindwa kueleza mara moja hasara itakayopatikana wala gharama ya transfoma hiyo ambayo aliilezea ni "kubwa sana isiyoweza kubebwa na magari ya kawaida, ikilinganisha na transfoma nyingine zinazoonekana barabarani."

Mtaalamu mmoja wa Tanesco alielezea tofauti iliyopo kwamba transfoma za vituo vikuu zina uwezo wa kipimo cha megavolti wakati za kawaida zinazosambaza umeme kwa wateja, zina uwezo unaopimwa kwa kilovolti (KVA).
Hitilafu hiyo, alisema itasababisha mgawo wa umeme kwa maeneo mengi jijini Dar es Salaam kutokana na kituo hicho kuhudumia wilaya zote; Ilala, Temeke na Kinondoni.

Maeneo yatakayoathirika, Badra aliyataja kuwa. ni Segerea, Kinyerezi, Bangulo, Tandika, Temeke, Mtoni, Mashine ya Maji, Yombo Vituka, Yombo Buza, Yombo Kilakala, Mbagala Kilungule, Maeneo ya Viwanda Vingunguti, Karakata, Banana, Kipunguni na Kivule.

Maeneo mengine ni Kitunda, Mwanagati, Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Chang'ombe, Temeke, Keko, Mtoni, Barabara ya Nyerere, Barabara ya Kawawa, Tazara, Vingunguti, Kiwalani, Segerea, Bangulo, Yombo Kilakala, Mbagala Kuu, Mbagala Kilungule, Banana, Kivule na Kitunda.
Souce: Mwananchi Monday, 22 November 2010 20:43
 
Tanesco hawataki kununua vifaa vinavyotengenezwa na Tanelec kwa sababu uongozi wa Tanelec haukubali ufisadi wa kuto 10%. Tanesco ina hisa katika Tanelec lakini kwa tamaa ya kupata 10% wananua vitu hafifu kupitia katika makampuni ya manayangau wa Tanzania. Ikifanyika independent audit ya manunuzi pale Tanesco asilimia 75 yab tenda anapewa mfanyabiashara mmoja wa pale pugu road kupitia katika makampuni yake.
hatufiki bila kufumua mfumo wa ufisadi ndani ya tanesco na wizara husika.
 
Kwa wale mnao wafagilia hao clouds fm kiukweli mimi sijapenda kabisaa zile kauli zao za asubhui hazikuwa na matamshi mazuri wala siyo fundisho katika jamii huo ni uzalilishaji siyo siri kwa kauli zao laiti ningelikuwa mimi ningewashtaki kabisaa,jamani hebu fikilia kama ndiyo mzazi wako engineer then mtu analopoka lopoka tu bila kujua makosa ni yanani,i believe makosa hayo siyo ya wafanya kazi mambo mengine tusiwe tunashabikia tuuuuuuu.sikupenda na nilichukia sana
 
Vuruga vunja imesha anza wizara ya ardhi, naomba baada ya ardhi ihamie TANESCO maana ni kitendo cha aibu sana mgao wa umeme kuanza baada ya uchaguzi, kwanini mgao haukuanza wakati wa kampeni?

Where u are!
Jana nilipiga simu tanesco mikocheni nikahoji mgao mmetangaza ni masaa manne mpaka sita ss inakuwaje ni saa la kumi nikajibiwa nimwulize eng.mkurugenzi nilichoka sana.
Huyu mkuu hajui kuna watu wliojiajiri bila umeme maisha yao na familia hayaendi?
Kwa nn wadanganye muda??...
Big G.hando nitakutafua jioni
 
Kwa wale mnao wafagilia hao clouds fm kiukweli mimi sijapenda kabisaa zile kauli zao za asubhui hazikuwa na matamshi mazuri wala siyo fundisho katika jamii huo ni uzalilishaji siyo siri kwa kauli zao laiti ningelikuwa mimi ningewashtaki kabisaa,jamani hebu fikilia kama ndiyo mzazi wako engineer then mtu analopoka lopoka tu bila kujua makosa ni yanani,i believe makosa hayo siyo ya wafanya kazi mambo mengine tusiwe tunashabikia tuuuuuuu.sikupenda na nilichukia sana

ebu tumbie tanesco wamekupa shillingi ngapi kuja kuwatetea mana wenyewe hawawezi kujisafisha mana ni makiritimba
 
guys, tanesco inafanya matengenezo muhimu sana, nadhani baada ya muda mambo yatakuwa fresh sana, NO umeme wa mgao tena!
kwa hivo inabidi tuwe wapole kidogo kwa muda huu
nimeshawishika kuchangia hapa, unaleta habari za matengenezo muhimu wakati mjadala wa vyanzo vya umeme haujakamilika, this tanesco is a big sh.it tatizo ni wanasiasa wanaoinfluence mambo mengi ya kitaalamu wakati wao si wataala wa fani husika, mwisho wa siku this sh.it itakuja na resolution ya kuongeza bei ya umeme kwa watumiaji. na watumiaji watatafuta mbinu za kukwepa kulipia gharama za matumizi yao. Mi nina imani kuwa tanesco inaweza kujiendesha kwa tija ya hali ya juu taitzo ni umangimeza. Unazalisha let say 100MWh halafu unakusanya revenue ya 20MWh utegemee nini hapo. Kuongeza bei ya umeme ili ku offset uncollected revenue si suluhisho kwani ni kudisappoint loyal customers. aaah tupeni kazi tuifanye hiyo jamani tanesco you are big sh..it
 
huo mgao umetangazwa Dar,sasa mwanza tynahusika vipi na ili giza za almost 2 weeks now?
hakuna siku umeme umewaka 12 hrs kuanzia asubuhi adi 12 jioni,au saa 11 jioni adi kesho yake!!
what is this yu tanesco-mwanza??yani mkoa unakaa giza 12 hrs usiku???
this is so serious...halafu mtu kakaa tu pale juu ya kiti eti anaongoza nchi??????
 
Hii ni aibu kubwa sana. Kuna directors managers na hata ministry inayo-oversee shughuli za TANESCO. Huu ni ujinga gani tena? Kwa nini hali kama hii inatokea ghafla hivyo? Ndio kusema serikali/TANESCO hawakujua nini kitatokea? Ooh walijua lakini ni kipindi cha uchaguzi hivyo iliwabidi kukaa kimya!!

Huu unafiki wa kisiasa unatuumiza wananchi. Niseme uchaguzi umeisha sasa na kwa kuwa TANESCO mmemkaa kisiasa zaidi tufahamisheni tu watu tupange ratiba.

Serikali/TANESCO ni lazima muelewe kuwa tofauti nanyi wananchi hatukurupuki bali tuna mipangilio ktk maisha ya kila siku. Mfano Arusha, Umeme haupatikani kwa zaidi ya saa 16 kwa siku na hakuna taarifa kwa umma harafu kuna managers wa mikoa!je wanamanage nini? Kama hata kutoa taarifa inashindikana?

Ombi langu kwa serikali na hususani wizara husika kuwa wazi. Ushindi iliopata CCM ni lazima uwe translated kwenye hizi huduma za msingi kama umeme. Si kweli kuwa wananchi wamechagua serikali (assuming hakuna uchakajuaji matokeo) ili ije kufanya upuuzi huu, watu wasiojua kuwa kutakuwa na tatito la umeme na kuandaa mbinu mbadala? Haya kwa sasa shida nini? Je maji yamepungua ni mitambo imeharibika? Ni nini hasa ambacho kimewakuta serikali/TANESCO by surprise. Nasema kwa utashi wa kawaida tu wanachotegemea wananchi toka kwa serikali si ubabaishaji wa aina hii.

Wakati JK anafungua Bunge ameongelea mengi kuhusu nishati na vyanzo mbadala. Hivi hiyo mikakati was it textbook standard au ni mipangilio ya serikali hii? SHAME!

JK anataka kukumbukwa kwa uongozi wake na mchakato huo ameona uanzie miaka mitano ya mwisho na si toka mitano ya kwanza. Mimi namshauri AAMKE sasa kwani kama ilivyopita miaka mitano ya kwanza na hii itapita fasta na kwa bahati mbaya sana dalili si nzuri hata kidogo kwani approval ratings kwa JK hazionyeshi picha nzuri.
 
Hii Wizara ya Nishati na Madini imejaa Ufisadi tupu ikiongozwa na huyu Fisadi Ngeleja.
Katika kipindi Cha Kampeni Ngeleja alimshurutisha Meneja wa Tanesco kumpatia Nguzo za umeme kutoka Stoo pale Nyakato zikaanza kusombwa kwa wingi na kwa kasi kupelekwa Sengerema haya yote yalifanyika kwa amri kwakweli Watendaji tutawalaumu bure tu.
 
Back
Top Bottom