Poll: Kitafunio kipi bomba kwa chai?

mara nyingi huwa naingia humu asubuhi halafu ninapoteza sana muda jamii photo,jumapili huwa sitembelai jamvi kabisa msalimie madam b.halafu ni kweli unapenda kiporo kuliko kipongo.

Madam b yupo hapa na Misukosuko ya nguo za ndani.
 
Chapati za kusukuma na chai ya maziwa ya mchaichai, au

kiporo cha wali wa nazi na maharage, kisamvu au samaki, au
uji lishe na wali kama hapo juu, au

Tambi za kukaanga na sukari zilizochangwanywa na iliki na rosti la maini ya ngombe pembeni kisha unashushia na chai ya tangawizi au juisi, au

Vitumbua, maandazi laini, na kipande cha kuku mchemsho kisha unashushia na chai ya mchaichai. aaaah mambo yanakuwa swadata!

Kawaida nikiamka asubuhi mida ya saakumi na moja naywa maji ya uvuguvugu kiasi na kijiko cha asali na ndizi mbili au tatu mbivu kama zipo kisha ndio apiga mswaki kuoga halafu mida ya saa nne au tano nikipata kati ya hivyo hapo juu siku yangu inapita swafi mpaka jioni. Huwa sioni shida kubeba kiporo ofisini inapobidi.

Then ushuzi ukija najisingizia aah tumbo langu leo lina gesi kumbe siri ya kiporo hahaha!
 
Back
Top Bottom