Polisi Z`bar wayapiga stop maandamano ya waumini wa Kanisa la Anglikana dayosis Z'bar

Waende Pemba mashamba yako mengi tuuu na waPemba nijuavyo wako very humble watawapa tuuu maeneo wajenge hayo Makanisa
 
hayati Abeid karume alitaifisha ardhi zote za mkoloni baada ya mapinduzi inawezekana kuwa hiyo Ardhi wanaosema kuwa ni yao Kanisa la Anglikana walipatiwa na Wakoloni sio!!
Kibunango kawambie babu zako wasiweke nia na matumaini ya kupewa hiyo Ardhi kitu hicho wasahau kabisa!!!!
any way Zanzibar ni nchi ya Waislamu 99% ya raia wake ni Waislam.....Makanisa yaliyojengwa yanatosha kwa Wageni waliopo zanzibar...Wa Zanzibar hawataki tena kujengwa Makanisa katika nchi yao kwa sababu hayana faida yeyote kwa taifa lao na watu wao!!!!!:painkiller:

Ikiwa Waislamu ni asilimia 99, hivo hayo makanisa yaliozidi mia yanawatumikia wageni wakuja? kwani kabla mapinduzi yalikuwapo makanisa mangapi?
 
hayati Abeid karume alitaifisha ardhi zote za mkoloni baada ya mapinduzi inawezekana kuwa hiyo Ardhi wanaosema kuwa ni yao Kanisa la Anglikana walipatiwa na Wakoloni sio!!
Kibunango kawambie babu zako wasiweke nia na matumaini ya kupewa hiyo Ardhi kitu hicho wasahau kabisa!!!!
any way Zanzibar ni nchi ya Waislamu 99% ya raia wake ni Waislam.....Makanisa yaliyojengwa yanatosha kwa Wageni waliopo zanzibar...Wa Zanzibar hawataki tena kujengwa Makanisa katika nchi yao kwa sababu hayana faida yeyote kwa taifa lao na watu wao!!!!!:painkiller:

I am sorry to say that you sound like a proper fanatic! simply because of you poor thoughts and judgements! Disgusting human creature!
 
hayati Abeid karume alitaifisha ardhi zote za mkoloni baada ya mapinduzi inawezekana kuwa hiyo Ardhi wanaosema kuwa ni yao Kanisa la Anglikana walipatiwa na Wakoloni sio!!
Kibunango kawambie babu zako wasiweke nia na matumaini ya kupewa hiyo Ardhi kitu hicho wasahau kabisa!!!!
any way Zanzibar ni nchi ya Waislamu 99% ya raia wake ni Waislam.....Makanisa yaliyojengwa yanatosha kwa Wageni waliopo zanzibar...Wa Zanzibar hawataki tena kujengwa Makanisa katika nchi yao kwa sababu hayana faida yeyote kwa taifa lao na watu wao!!!!!:painkiller:
Iwapo ardhi yao imevamiwa, hapana shaka wataipata tu! Ni jambo la muda mfupi tu. Zaidi nilichosoma hapa ni ulafi na uroho wa baadhi ya watu na hasa linapokuja suala la ardhi.
 
Kusema kweli katika suala hili Karume Family wamecheza faulo mbaya kabisa, kwa sababu hata kutaifisha kuna taratibu zake, huwezi kuvamia sehem ya mtu mwingine kwa sababu una mapesa, vyombo vya usalama etc, hata mugabe hakufanya hayo anayoyafanya Karume Jr. nawasihi waathirika waende mahakamani ( ingawa sina hakika kama watatendewa haki )
 
Sipendi kukujibu, ila nafanya hivi kwa kumbukumbu za baadae. Ardhi ni mali ya serikali kwa mjibu wa sheria ya ardhi ya mwaka 1985(SMZ). Hii ina maana kuwa serikali ndio yenye wajibu wa kupima na kugawa ardhi visiwani hapo.

Kiwanja cha kanisa huko Mbweni kilishapimwa na kumilikishwa kwa kanisa hilo, na iwapo atatokea mtu mwingine yoyote kuendeleza eneo hilo ni wazi kuwa atakuwa ni mvamizi. Hivyo basi ni jukumu la kanisa kuona kuwa eneo lao halivamiwi.

Tatizo lao wanataka kufuga Kitimoto katika eneo hilo na wenyewe hawataki-Zanzibar hakuna ubalozi wa papa kama Tanganyika-Sorrrrrrrrrrrrrrrrrrrrry
 
Tatizo lao wanataka kufuga Kitimoto katika eneo hilo na wenyewe hawataki-Zanzibar hakuna ubalozi wa papa kama Tanganyika-Sorrrrrrrrrrrrrrrrrrrrry
Sidhani kama sababu hiyo ni ya msingi, ya kuwafanya hao wavamizi kuvamia eneo hilo. Kuhusu kitimoto mbona kinapatikana kwa nafasi hapo kisiwani!
 
wazanzibari acheni ubaguzi wa kidini na kukandamiza wakristo. jifunzeni kwa wabara mtapata uelewa.

ni kweli mkuu, wajifunze kwa waislamu wabara kukubali kuburuzwa! vinginevyo kasi ya wakiristo kumiminika visiwani itazidishwa, kisha wanungunike,"ethenic cleansing" kama walivotendewa wa Tibet na Wachina!
 
..waumini wa madhehebu ya Anglican, wakiongozwa na viongozi wao, wamekwenda ktk kiwanja walichoporwa na kuharibu mali.

..waumini hao wanadai kwamba aliyepora kiwanja hicho ameng'oa misalaba ktk makaburi ya wazee wao!!

NB:

..huyo binti ya Karume kwanini asije huku Tanganyika ambako kuna ardhi ya kutupa?

..kung'oa misalaba, tena kwenye makaburi, ni kukosa utu na heshima.

..huyu hana tofauti na kijana anayeshtakiwa kwa kuchoma Koran huko Zanzibar.
 
Hongera kanisa, kwa kuchukuwa sheria mkononi mwake, na wazenji pia makanisa yaliojengwa kwenye ardhi zilizokuwa za watu kabla mapinduzi, nao wayabomowe?
 
Kusema kweli katika suala hili Karume Family wamecheza faulo mbaya kabisa, kwa sababu hata kutaifisha kuna taratibu zake, huwezi kuvamia sehem ya mtu mwingine kwa sababu una mapesa, vyombo vya usalama etc, hata mugabe hakufanya hayo anayoyafanya Karume Jr. nawasihi waathirika waende mahakamani ( ingawa sina hakika kama watatendewa haki )

Kwa kusupport tu mbona hii ni kawaida na Waislamu kwa vile ni asilimia kubwa ndiyo waathirika wakubwa. Kuna kesi ya yule Mzee Abdulla wa Kiembesamaki ambayo aliyekuwa Mkuu wa Mkoa Abdulla Rashid, aliyekuwa Mkuu wa Usalama Mohammed Hija na nadhani Mansour shemegi yake Karume wamevamia ardhi ya huyu Mzee. Licha ya kupata ushindi mahakamani na kuamriwa kuvunja nyumba hizo mpaka leo hakuna lo lote lililofanyika.

Maeneo mengi na hasa ya beach za Unguja na Pemba yamevamiwa na ukoo wa Karume na wenyeji wanalalamika bila ya mafanikio
 
Sahau , not this time, hili ni Kanisa mkuu, ataitema tu ardhi, mbona wameiteketeza mali hawakufanywa kitu? na wajaribu waislamu kuchoma moto makanisa yaliojengwa kwenye ardhi zao, watakoma!
 
Kwa kusupport tu mbona hii ni kawaida na Waislamu kwa vile ni asilimia kubwa ndiyo waathirika wakubwa. Kuna kesi ya yule Mzee Abdulla wa Kiembesamaki ambayo aliyekuwa Mkuu wa Mkoa Abdulla Rashid, aliyekuwa Mkuu wa Usalama Mohammed Hija na nadhani Mansour shemegi yake Karume wamevamia ardhi ya huyu Mzee. Licha ya kupata ushindi mahakamani na kuamriwa kuvunja nyumba hizo mpaka leo hakuna lo lote lililofanyika.

Maeneo mengi na hasa ya beach za Unguja na Pemba yamevamiwa na ukoo wa Karume na wenyeji wanalalamika bila ya mafanikio
Naona hapo umechanganya stori, Hija alivamia eneo hilo, hukumu ilitolewa wakati Abdalla Rashid akiwa Mkuu wa Mkoa hata hivyo pamoja na ubabe wake alishindwa kuvunja nyumba ya Hija.
 
Naogopa ku-comment! lakini vitu vingine havihitaji hata theluthi ya akili kufikiri! MS angekuepo akaiona hii angefurahi huyo!! sijui ndo huyo anayejiita Buguruni kwa Mnyamani...
 
Picha:Kadhia ya kiwanja cha Mbweni Karume ajibu mapigo

Rais Mstaafu Aman Abeid Karume wa Zanzibar

  • Karume Amtetea Binti Yake Juu ya Kiwanja
RAIS Mstaafu wa Zanzibar, Amani Abeid Karume amtetea Mwanawe Fatma Karume kuwa ndio mmiliki halali wa kiwanja kilichopo Mbweni eneo la Mfuuni ambacho kimeingia katika mgogoro kati ya Kanisa la Angalikan na mwanawe huyo.
Akizungumza na waandishi wa habari nyumbani kwake jana, Mbweni, Karume alisema mwanawe ana hati kamili za kiwanja hicho kutoka serikalini kwa kuwa ametimiza vigezo vyote vinavyohitajika na hivyo anastahiki kujenga kwa kuwa kiwanja hicho ni chake.
Juzi Kasisi Msaidizi wa Kanisa la Angalikan Zanzibar, Mathew Wilfred Mhagama aliongoza maombi maalumu na kumtaja Fatma Karume kuwa ameporwa kiwanja cha kanisa hilo pamoja na sehemu muhimu ya makaburi ya wazazi wao ambayo yamekuwepo kwa miongo kadhaa katika eneo hilo.
Karume alisema kwamba ni yeye aliyechukuwa juhudi za kuyatunza makaburi yaliopo eneo la Mfuuni kutokana na waumini wenyewe kuyatekeleza makaburi yao kwa muda mrefu sana.
Alisema yeye na familia yake imefanya kazi kubwa ya kulilinda na kuliokoa kanisa hilo ikiwa pamoja na kutafuta mlinzi kwa kuwa muda mrefu lilikuwa halina mlinzi na milango yake ilikuwa ikiwa wazi kwa muda wa miaka kadhaa.
"Makaburi yale mlioyaona kwa muda wa miaka 20 sasa yanatunzwa na familia yetu… ni mimi binafsi na familia yangu yote ndio tunaoyatizama na baadhi ya wakati hupata nafasi ya kutoa pesa kwa ajili ya kulimiwa majani na kufanyiwa usafi katika eneo lote lile la makaburi yaliopo pale"alisema Karume huku akiwa amekaa na binti yake pembezoni.
Awali Karume alieleza masikitiko yake kutokana na kauli zilizotolewa na viongozi hao wa dini huku akisema hawajasema ukweli na badala yake wameendekeza jazba ambazo zimewafanya waumini wao kwenda moja kwa moja katika kiwanja na kufanya fujo la kuharibu mali ya mwanawe ambaye ni mmiliki halali wa kiwanja hicho.
Karume aliwaita viongozi walioongoza misa juzi katika kanisa la Angalika liliopo Mbweni na kukusanya kundi la waumini wa dini hiyo kwamba ni viongozi waliopotoka na wasiofuata maadili na mafundisho ya kitabu kinachowaongoza.
Alisema viongozi hao wamepotoka kwa kuwa wameshindwa kufuata maadili ya dini yao inavyowaelekeza na kitendo cha kujichukulia sheria mikononi mwao cha kuvunja vunja vifaa vilivyokuwa katika eneo la ujenzi na kuharibu mali ya watu ni kosa kisheria.
"Nimeshangazwa sana na hawa viongozi wa dini ni viongozi wa ajabu sana tena wamepotoka kabisa ..kwa sababu wameshindwa kufuata maadili ..naona wanakosa utu na heshima kwa wakubwa zao" alisema Rais Mstaafu Karume huku akiwa amekunja uso wake na kutafuna tafuna ulimi wakena kuongeza kwamba.
"Tangu enzi za baba yangu pamoja na mimi nimekuwa na uhusiano mzuri na kanisa hilo…..nimehamia hapa katika mwaka 1968 hakuna mtu yoyote katika eneo hili isipokuwa kanisa" alisema Karume na kuwageukia waandishi wa habari.
Hata hivyo Rais huyo mstaafu aliwapoza waumini wa kanisa hilo la Angalikan kwa kusema kwamba ujenzi wa mwanawe huyo hautoathiri wala kubomowa makaburi yaliopo jirani ya kiwanja hicho hasa kwa kuzingatia kwamba makaburi hayo yanatunzwa na familia yake kwa miaka mingi tu.
Akiongea baada ya kumaliza baba yake binti huyo Fatma Karume alisema hana mpango wowote wa kuharibu wala kubomoa makaburi ya waumini wa wakrito na ujenzi wake utaheshimu eneo hilo muhimu la makaburi.
"Mimi ndio mmiliki wa eneo hili kihalali na hati zote kamili za kisheria ninazo mimi dini yangu ya kiislamu na madhehebu yangu yananiagiza kuheshimu dini nyengine kwa hivyo sina matatizo wala nia ya kuharibu wala kubomoa makaburi wa dini nyengine kwa sababu ninaheshimu dini zote" alisema Fatma Karume ambaye kitaaluma ni mwanasheria.
Fatma naye kama baba yake alishangazwa na waumini wa madhehebu hayo ya kiangalikan kutokana na kuiruhusu kampuni moja ya Kichina inayojenga hoteli karibu na eneo la makaburi ambapo udongo unaochimbwa katika ujenzi wa hoteli hiyo inayojengwa humiminwa makaburi hapo kwa kuwa uongozi wa kanisa hilo umetoa ruhusa wenyewe.
Aliulaumu uongozi wa kanisa la Anglikana kwa kuruhusu kampuni inayojenga hoteli na kuweka kifusi na udongo katika makaburi ya Wakristo na hivyo kuyaharibu makaburi hayo ambayo waumini hao wanasema kwamba makaburi yao yamechimbwa na kungolewa misalaba yao wakati uongozi ndio uliotoka kibali cha uharibifu huo.
"Nimeshangazwa sana na uongozi wa kanisa hili kwa kwa kuiruhusu kampuni hiyo ya kichina kumwaga kifusi wanachokichota kule katika hoteli na kukimwaga katika eneo lile la makaburi….nimekuwa najiuliza nani anayepuuza na kudharau makaburi haya ni mimi au wao wenyewe walioruhusu hii kampuni kumwaga udongo"?alihoji Fatma Karume.
Juzi kanisa la Angalikan liliitisha misa maalumu ya maombi yaliongozwa na Kasisi Msaidizi, Mathew Wilfred Mhagama wa kanisa Mkunazini Zanzibar, kumshitakia Mungu wakidai wameporwa ardhi yao na binti wa rais mastaafu na kuwataka waumini hao kutembea kwa mguu hadi kwenye kiwanja kilichopo mbweni na kushuhudia ujenzi wa jengo linalomilikiwa na Fatma Karume.

http://www.mzalendo.net/wp-content/uploads/2011/01/DSC_7976.jpg http://www.mzalendo.net/wp-content/uploads/2011/01/DSC_7977.jpg

Rais Mtaafu wa Zanzibar Mh.Amani Karume akitoa Mapigo kwa waandishi wa habari
http://www.mzalendo.net/wp-content/uploads/2011/01/DSC_8164.jpg
http://www.mzalendo.net/wp-content/uploads/2011/01/DSC_8174.jpg
Fatuma Aman Karume (kulia) akiongea na wandishi wa habari kwenye eneo hilo la Mfuuni Mbweni.
 
Back
Top Bottom