Polisi watimua mbio kujinusuru na vijana wa CHADEMA

hiyo ni rasha rasha.ipo siku Tanzania tutapata uhuru.kumbuka Tanganyika ndiyo ilipata uhuru 1961 na si Tanzania.tuungane sote kumuondoa mkoloni Magamba.
 
Si polisi tu hapa ukionekana na vinguo vya kijani kama mwanaccm balaa na hasa ukiingia sokoni wale kinamama watakutupia nyanya usoni duuh arusha imesisimuka ile mbaya.
 
Acha hiyo ya clock tower. katika eneo la mkutano kulikuwa na defender ya polisi inapita barabarani ikijaribu kutanua njia kwa kasi mpaka ikamgonga mwendesha boda boda. baada ya kumgonga pembeni watu walilishambulia kwa mawe ilibidi wakimbie kwa kujiokoa. polisiccm ni waoga kama nini.




Sidhani kama ni uoga Mungi. Si rahisi kuwa na SMG halafu ukawa muoga. Nadhani utakuwa ni mpango mkakati kwa kuepusha shari, na hii taarifa mimi binafsi naipokea vizuri. Kuna busara imeamriwa hapo polisi Arusha. Polisi mmefanya busara sana leo Arusha. Big up! Si kila kukimbia ni cowardice. Kukimbia kwingine ni wisdom.
 
polis wanajua fika hatima yao.Watavuna walichopanda.Wakilimbilie huko ugambani maana mabomu na risasi cha mtoto. Wanamulikwa kiwizi.
 
sasa hapa cha kufurahisha ni nini?
Maisha ya polisi kuwa hatiani?
Hata kama hawakushiriki kwenye baya lililowapata CDM?

Unadhani ni sahihi?

hii ni 'mob justice' kama zingine tu.
Eti kwa sababu imefanywa na washabiki wa CDM tukenue? Hapana kwa hili.
 
Hivi hawa CCM wanadhani Tanzania ni mali yao? Wanadhani risasi za moto ndiyo jibu kwa maisha magumu ya watanzania ?
 
cha kujifunza hapa ni hawa Polisi wana mapenzi mema na CDM vinginevyo wangeza kuwapiga risasi kisha wakasingiza walikuwa wana vamia bank tungesemaje

nawashauri wangefanya kama wenzao wa Mbeya waliokuwa wanalinda bank ya Barclays wao walionyesha alama ya V kisha wakasema tuko pamoja vija hawakuwa na taabu nao
 
Polisi ya nchi hii wanakiuka malengo ya kuanzishwa kwa jeshi hilo. Badala ya kulinda usalama wa raia na mali zao wanakuwa maspy wa watawala na watu wa kuwaonea raia. Ngoja Chadema ichukue dola ndiyo watajua kwamba uspy unawatu wake.
 
jamani,kweli ccm imekufa,wasipokuwa makini tunakoelekea viongozi wa ccm wote watatembea kwa escot ya polisi vinginevyo tutawafanya vibaya
 
Unajua wakuu amini msiamini polisi wengi sana,ni supporters wa C.d.m,sema mfumo umewabana sana,mimi ni rafiki zangu ka wanne ni polisi na uwa naendaga kwenye sehemu zao za vilaji,yaani jinsi wanavyoiua magamba hauwezi amini,nasikia hata 2010 huko Moshi C.c.p magamba walilamba kula chache mpaka aibu!mfumo wa kiutawala unaochangia uoga wa kupoteza kazi ndio unawafanya polisi waonekane ni gambaz
 
Back
Top Bottom