Polisi watimua mbio kujinusuru na vijana wa CHADEMA

MVUMBUZI

JF-Expert Member
Jan 8, 2011
5,182
2,304
Ilikuwa kama sinema ya bure hapa NMB Clock tower jioni hii polisi wawili walipoacha lindo na kutimua mbio live waliposikia sauti za kundi kubwa la vijana waliotokea kwenye mkutano wa Chadema. Vijana hawa zaidi ya 2000 walikuwa wakisukuma gari ya Lema kutokea viwanja vya NMC huku wakiimba"bila Lema patachimbika". Walipofika round about ya clock tower wakawaona polisi waliokuwa pale benk na kupiga kelele haooo!!.Ghafla polisi wale 2 walinyanyuka na silaha zao wakatimua mbio bila kukimbizwa na mpaka naondoka eneo la tukio lindo lilikuwa bado limetelekezwa. Akina mama waliokuwepo eneo hilo walishikilia mbavu zao kwa kicheko kwani hii ni mara ya kwanza kuona polisi wenye silaha wakiwakimbia raia kwa spidi kubwa mithili ya wanariadha.
 
Acha hiyo ya clock tower. katika eneo la mkutano kulikuwa na defender ya polisi inapita barabarani ikijaribu kutanua njia kwa kasi mpaka ikamgonga mwendesha boda boda. baada ya kumgonga pembeni watu walilishambulia kwa mawe ilibidi wakimbie kwa kujiokoa. polisiccm ni waoga kama nini.
 
nimeshuhudia hapa friends corner polisi wakikimbia baada ya gari lao kushambuliwa na mawe.
 
Ilikuwa kama sinema ya bure hapa NMB Clock tower jioni hii polisi wawili walipoacha lindo na kutimua mbio live waliposikia sauti za kundi kubwa la vijana waliotokea kwenye mkutano wa Chadema. Vijana hawa zaidi ya 2000 walikuwa wakisukuma gari ya Lema kutokea viwanja vya NMC huku wakiimba"bila Lema patachimbika". Walipofika round about ya clock tower wakawaona polisi waliokuwa pale benk na kupiga kelele haooo!!.Ghafla polisi wale 2 walinyanyuka na silaha zao wakatimua mbio bila kukimbizwa na mpaka naondoka eneo la tukio lindo lilikuwa bado limetelekezwa. Akina mama waliokuwepo eneo hilo walishikilia mbavu zao kwa kicheko kwani hii ni mara ya kwanza kuona polisi wenye silaha wakiwakimbia raia kwa spidi kubwa mithili ya wanariadha.
kwa maana hiyo benk haina ulinzi na hapo ni Arusha!
 
Arusha ni ukanfa wa gaza. Kitachofuata siku za mbele huenda ni kuhakikisha kuwa rangi ya kijani haionekani popote.
 
Wewe unashangaa ppolisi wawili kukimbia wakati kuna 109 ilikuwa imejaza polisi walikimbia na wana silaha zao...
 
Jamani ccm someni alama za nyakati msipake mate kulazimisha mambo yasiyo wezekana
 
Nchi hii bwana yaani tayari niko gizani na kuna nyama kwenye freezer kwa ajili ya kesho! Mungu wangu naona itaniozea tu hapa. Umeme wagenda.
 
Haya ni matokeo ya muda mfupi ya vitendo vya PT kwa wananchi, madhara ya muda mrefu ni mabaya zaidi. Lakini sio viongozi wao wala watawala watakaolipa jicho stahili suala la uhusiano uliozorota kati ya PT na wanachi wa Tz
 
Na bado, polisi nyie ni baba zetu, kaka zetu, mama zetu, dada zetu na wadogo zetu. Acheni kabisa kulinda na kuelekezwa cha kufanya na ccm. Mnalipwa kwa kodi zetu, na hizi shule zetu za kata ni mwiba mchungu wa ccm. 2015 sio mbali, lowekeni vichwa vyenu, au badilikeni kwa 100% muwe neutral.
 
Nchi hii bwana yaani tayari niko gizani na kuna nyama kwenye freezer kwa ajili ya kesho! Mungu wangu naona itaniozea tu hapa. Umeme wagenda.

Pole sana kamanda. Ndio matokeo ya sera za umaskini na ubabaishaji wa ccm zinavyoumiza wazalendo kila siku kwa miaka 50+
 
Hali ya usalama wa polisi Arusha inazidi kuwa ngumu kwani mkutano ulikuwa na amani ila fujo zinatokea pale tu polisi wanapo onekana wanazomewa na kurushiwa chupa za maji kisa ni wao kukubali kuwakumbatia mabwenyenye ambao mda huo wanakuwa kwenye viyoyozi
 
Polisi hao bila shaka hawana elimu ya Uraia.Inakuwaje polisi kumkimbia raia pasipo kosa?Iwapo vijana wa CDM walikuwa wanania ya kutaka kuwavamia Polisi hao tena eneo la Benki hapa binafsi siungi mkono kwa vijana hawa.
 
Back
Top Bottom