Polisi watimua mbio kujinusuru na vijana wa CHADEMA

Ilikuwa kama sinema ya bure hapa NMB Clock tower jioni hii polisi wawili walipoacha lindo na kutimua mbio live waliposikia sauti za kundi kubwa la vijana waliotokea kwenye mkutano wa Chadema. Vijana hawa zaidi ya 2000 walikuwa wakisukuma gari ya Lema kutokea viwanja vya NMC huku wakiimba"bila Lema patachimbika". Walipofika round about ya clock tower wakawaona polisi waliokuwa pale benk na kupiga kelele haooo!!.Ghafla polisi wale 2 walinyanyuka na silaha zao wakatimua mbio bila kukimbizwa na mpaka naondoka eneo la tukio lindo lilikuwa bado limetelekezwa. Akina mama waliokuwepo eneo hilo walishikilia mbavu zao kwa kicheko kwani hii ni mara ya kwanza kuona polisi wenye silaha wakiwakimbia raia kwa spidi kubwa mithili ya wanariadha.

Lazima wakimbie maana vijana wa CDM walikuwa wana rizm ya viroba na ndumu wangewadhuru bure askari wetu watiifu wise decision!
 
Lazima wakimbie maana vijana wa CDM walikuwa wana rizm ya viroba na ndumu wangewadhuru bure askari wetu watiifu wise decision!

Tatizo umekurupuka usingizini ili uende viwanja la sivyo isingekuwa ngumu kwako kuelewa kwamba mkutano wa CDM haukufanyika bar bali uwanja wa wazi. Jifute tongotongo na kapige mswaki ndo urudi kuchangia.
 
Heading tu ilinifanya nismile halafu content ikamalizia kwa kunivunja mbavu! Dah! Nimeona km vile nilikuwa eneo la tukio.
 
Tatizo umekurupuka usingizini ili uende viwanja la sivyo isingekuwa ngumu kwako kuelewa kwamba mkutano wa CDM haukufanyika bar bali uwanja wa wazi. Jifute tongotongo na kapige mswaki ndo urudi kuchangia.

Mwambie mkuu,, maana anawaza kim.a'gamba ga'mba tuuuu

:bump2:
 
Ilikuwa kama sinema ya bure hapa NMB Clock tower jioni hii polisi wawili walipoacha lindo na kutimua mbio live waliposikia sauti za kundi kubwa la vijana waliotokea kwenye mkutano wa Chadema. Vijana hawa zaidi ya 2000 walikuwa wakisukuma gari ya Lema kutokea viwanja vya NMC huku wakiimba"bila Lema patachimbika". Walipofika round about ya clock tower wakawaona polisi waliokuwa pale benk na kupiga kelele haooo!!.Ghafla polisi wale 2 walinyanyuka na silaha zao wakatimua mbio bila kukimbizwa na mpaka naondoka eneo la tukio lindo lilikuwa bado limetelekezwa. Akina mama waliokuwepo eneo hilo walishikilia mbavu zao kwa kicheko kwani hii ni mara ya kwanza kuona polisi wenye silaha wakiwakimbia raia kwa spidi kubwa mithili ya wanariadha.

Kama walikuwa na silaha na wakatimua.

Tulitizame hili jambo hivi!

Wangeweza kusubiri wavamiwe na hatimaye wajitetee kwa kufanya mauaji kama walivyowahi kufanya mauaji hapo Arusha.

In that case then !!!

Walichokimbia ni kufanya au kutegeneza mauaji mengine hapo Arusha kitu amabacho Wanajua kabisa kuwa Pasingekalika...

"WITO" CCM itafakari kwa makini Ushujaa wa hao "askari watimua mbio" na kuwapa nishani ya kuepusha Maafa ambayo yangetokea kama wangesuburi kushambuliwa na wao kujitetea.
 
Wamesoma alama za nyakati wanaelewa kabisa wanaarusha wana hasira ya kuvuliwa ubunge kwa mbunge wao so wakijaribu kuanzisha vurugu zozote huo mji hautakalika watalipiza kisas kwa serikali na chama tawala coz tetes zinasema ni hukumu ya kisiasa
 
Nadhani jina "vijana wa Chadema" ambalo hutumika sana hasa kwenye vyombo vya habari halitoi picha kamili; hawa watu wanapaswa kuanza kutambulika kama "wazalendo" kutokana na kile wanachokipigania.
Itapendeza iwapo jina hili litaanza kuzoeleka vinywani mwetu.
 
Mie nashangaa, mtu mzima anasema polisi kakimbia na silaha zao, kumbe ulitaka polisi ajitunishe kwa silaha? akili zingine bwana ni ngumu kuzielewa zinataka nini.
 
Hao police wanastahili pongezi,wametumia busara kubwa sana,otherwise sa hzi tungekua tunaongea mengne,ikumbukwe police wanaolinda sehemu kama banks,huwa wanakua na SMG mkononi,so endapo ingetokea bahati mbaya hao vijana wa chadema wakawaletea fujo kwenye eneo lao la kazi nao wakaamua kujibu mapigo,nadhani madhara yake yangekua makubwa sana na yangeligharimu taifa kwa ujumla.natoa pongezi zangu kwa hao police.
 
mafisadi/waovu na vibaraka wao hukimbia mbio hata wasipokimbizwa na mtu, ndivyo hata Biblia inavyonena
 
Vijana wa CDM wala hawakuwa na shida nao walijihisi tu kutokana na tabia yao ya kupendelea magamba.
 
Kwa mtu makini,mzalendo mwenye nia njema na nchi hii hawazi kutishia polisi wakiwa lindoni ama kuchekelea kuona Polisi wakitimua mbio kuliacha lindo hasa lindo muhimu kama la benki kwa sababu zozote zile,badala yake aionapo kuna dalili za kuashiria uvunjifu wa amani atashirikiana na Polisi kupigana hata kupoteza maisha yake kwa maslahi ya taifa na mali za umma.

Sote tunajua benki hutunza pesa za umma,hususani NMB kuna pesa za watu wakaada za chini kabisa,hivyo lolote likitokea hata kama Pesa ya mteja wa benki haipotei ila uchumi huyumba.

1.Ni kwanini hao wafaasi wa CDM wazomee polisi akiwa lindoni na hata kuwatia hofu?
2. Ni kwa nini hao akinamama wanachekelea kitendo cha polisi kukimbia lindo?

Aidha nini kingetokea kama Polisi nao wangeamua kutumia uhuni wa kuzomea na hatimaye kusimama imara kwa lolote lile kukabiriana na hao vijana 200,vifo ama majereha yangekuwa juu ya nani?sasa uzalendo uko wapi?

Napenda kushauri tuwe makini tuwapo kwenye mikusanyiko ya watu kama mikutano na maandamano maana watu wenye nia mbaya na nchi hii wanaweza wakatumia mianaya hiyo kuanzisha vurugu ili kutekeleza na kufanikisha uharifu.Viongozi wa vikao kama hivyo inawapasa wawe makini
 
polisi msikubali kuwa vibaraka kwani ninyi hamlindwi wakati magamba wanalindwa, ninyi ni ndugu zetu na tunaishi sote mtaani magamba wanaishi sehemu mnazokesha mkiwalinda kwa silaha za kivita, je enyi polisi nani anakulindeni, msipobadilika msijeshangaa mkaanza kuuawa wakati magamba yataendel3a kupeta na kutoa taarifa za uongo kuhusu vifo vyenu
 
Acha hiyo ya clock tower. katika eneo la mkutano kulikuwa na defender ya polisi inapita barabarani ikijaribu kutanua njia kwa kasi mpaka ikamgonga mwendesha boda boda. baada ya kumgonga pembeni watu walilishambulia kwa mawe ilibidi wakimbie kwa kujiokoa. polisiccm ni waoga kama nini.

CCKM na ile kwao-Ichimuisebu
 
Kilicho wakimbiza wanakijua vizuri,huwezi kumfanya mtu mjinga daima. Atakuwa mjinga kwa muda tu,ndiyo kinachotokea hapo.
 
Back
Top Bottom