Polisi wapigwa kama wezi, wanusurika kuchomwa moto!

TABIA MBOVU nasema polisi wamezidi:

KUNA siku moja hivi karibuni nilikuwa natoka Arusha naja Dar,karibia kufika SAME traffic akanipiga mkono...NIlikuwa najiamini coz sijaoverspeed na kila kitu kilikuwa sawa.

Traffic akaanza kuniuliza maswali:fire extinguisher-nikamwonyesha,
leseni-nikampa
akaanza kuangalia tires-zote mpya mpaka sprear
triangle-nikamwonyesha
unatoka wapi na unaenda wapi nkamwambia-non of ya bussines adn leave pie as pie.

AKAKASIRIKA NA KUNIAMBIA NIMWONYESHE FIRST AID KIT.........................nikamwambia hata gari lenu hilo halina.NIKAMRUSHIA BUKU MBILI NKATIMUA coz nilikuwa na haraka.

IKO SIKU NITAKOMAA NAO.
 
Ebu hacha nidhamu za woga, unaona vitendo vinavyo fanywa na hawa polisi ni vizuri kweli, BIG UP Kagera, huku Dar tuko pamoja nanyi.

Ningekuwepo ningeshiriki kuwapiga hao jamaa,kama hujawahi pata adha ya polisi anayetaka rushwa kinguvu,lazima utaendelea kusema sheria kwanza,lakini kama ni kinyume chake,utaungana na jamii.

Yule mbakaji wa Wazo hill juzi hapa kaachiwa huru na aliyebakwa katiwa ndani,mpaka wakazia wa Boko walipoandamana kwenda kumtoa yule mama. Aibu tupu
 
Sorry siungi mkono kujichukulia sheria mkononi. Wananchi wafuate taratibu

Mkuu sisi kama wananchi tumefuata taratibu zote za kulalamika lakini kero zetu hazitatuliwi milele na milele je ukiwa kama wewe utaendelea kuvumilia kweli mpaka lini? Inafika kipindi tunasema enough is enough kinacho fuata ni kiminyo tu.
 
Sorry siungi mkono kujichukulia sheria mkononi. Wananchi wafuate taratibu

Ukiona wananchi wanajichukulia sheria mkononi ujue hawana imani na hizo taratibu. utafuata taratibu mara ya kwanza, no action!, ya pili, no action! what next?. Kilichopo hapa ni kwa jeshi la polisi na serikali kujisafisha ili kurudisha imani kwa wananchi. "There is nothing worse than being seen as a lemon .'The Market for Lemons' "- Arkerlof

Polisi wakiisha onekana hawafuati sheria na haki (ma-lemon), unatarajia wananchi wawachukuliaje hao polisi? (jibu ni vibaka)
 
Last edited:
Huo si utawala wa sheria.
Siungi mkono

Kunyanyasa raia wema ndo utawala wa sheria?
Kunyimwa haki zako za msingi kama unaishi maeneo ya Manzese kukosa huduma za msingi kama zahanati,maji,barabara n.k nao utawala bora?
Kutotoa haki kwa raia nao ni utawala wa sheria?
Kupunja mishahara,malikimbizo n.k kwa watumishi wa ngazi ya chini nao ni utawala wa sheria?
 
Mkuu, wamepigwa kidogo wangewageuza ma albino ingekuwa afadhali.Hivi huyu mganga aliyesema kuwa ma albino ni dili si angesema ma trafiki ma polisi ni dili wakapungua make wamezidi kuomba rushwa, juzi mimi naenda zangu tegeta, kupitia sum nujoma, trafiki ananipiga mkono bila angalu kujua hii gari iko tinted labda kuna bosi wake,nikasimama na kupaki gari, ngoja akague gari lote mara lete hiki mara lete kile, bahati mbaya sikuwa na fire extinguisher,akasema ni kosa lazima nilipe faini 20,000/=, nikamwambia,sikujua kama sina fire maaana tangu nimenunua uwa inakaa kwenye gari, labda vijana wanaonifanyia service ya gari wamechukua na sikujua, hivyo nipe onyo nikanunue kwasababu sikujua kama sina.Yule trafic bwana akasema sikuachii bwana lete 10,000 weka ndani ya leseni alafu nipe.Nikaona noma, kwenye leseni tena akichua vyote itakuwaje,nikamwekea kwenye triangle na kumpatia, aiseee nilitamani kumzaba vibao lakini sikuwa na jinsi akaniachia nikatimka zangu, hivyo jamaa wa bukoba wangewageuza dili.
 
Sorry siungi mkono kujichukulia sheria mkononi. Wananchi wafuate taratibu

Kwani hao polisi walipokodi teksi na kwenda nje ya kituo chao cha kazi na nje ya eneo lao la kazi walifuata taratibu zao za kazi? Au wanavyoenda huko kuvizia kuomba rushwa ni taratibu zao za kazi?

Ukumbuke kuwa hakuna hata mwana JF mmoja atakayeunga mkono kitendo cha kupiga polisi au raia mwingine bila sababu, ila inaonesha kuwa kwa kiasi kikubwa raia wenye hasira kali wanaanza kusema SASA BASI!
 
The epitomy of chaos.

1. Serikali haina mifumo mizuri ya masoko inayohakikisha wananchi wanaweza kulipwa vizuri baada ya kuuza mazao yao, a recipe for chaos.

2.Wananchi wanaona hakuna mifumo mizuri ya kuuza mazao yao, hivyo wananvunja sheria kwa kutumia njia za magendo, a recipe for chaos.

3. Polisi, ambao ni sehemu ya ukiritimba wa kiserikali unaosababisha wananchi wakose kuweza kuuza mazao yao kwa uhuru, wanaongezea machungu kwa wananchi kwa kutaka kuwatoza rushwa, a recipe for chaos.

4.Wananchi kwa kukerwa na "uonevu" wa serikali na wafanyakazi wayo, wanaamua kuchukua hatua mikononi mwao na kuwaadibisha askari hawa, chaos.

Jinsi ninavyoiona hali hivi sasa mambo yanajichanganya polepole, tutafika sehemu ambapo tutashindwa kurudi nyuma na matokeo yake yatakuwa mabaya sana, narudia mabaya sana.

Mkuu Bluray,

Umenikumbusha amri haramu aliyoitoa Kiweru wakati akiwa mkuu wa mkoa wa Kagera kwamba yeyote atakayeonekana anavusha kahawa kwa magendo kwenda Uganda apigwe risasi. Kuna watu wengi walipoteza maisha katika jitihada zao za kuukwepa umasikini. Kwa nini mtu akauze kahawa yake Uganda wakati kuna bei inayokubalika Tanzania? Je tumeishajiuliza ni kwa nini private companies zilizuiwa kununua kahawa Kagera? Jibu ni rahisi wanawanyonya wananchi kwa kuwapa bei mbovu ya kahawa ili warudishe pesa walizochota kuisaidia CCM kushinda. Je huku sikuwafanya wananchi kuwa masikini kwa makusudi?

Siungi mkono watu kujichukulia sheria mkononi lakini hawa wananchi wanaonyesha wamechoka na uonevu!!!!

Tiba
 
wapigeni sana tu rushwaaa noma
Jamani, maslahi ya Polisi ni duni saana though hii haijastify wao kuwanyanyasa wananchi.
Masuali ya kujiuliza:
1. Je wananchi hawavunji sheria hadi wanaomba rushwa?
2. Na km wamechoshwa na rushwa kwanini basi wasiache uvunjaji sheria?
3. Kuwapiga polisi ndio utatuzi wa matatizo yao au kujenga uhasama?
4. Inamaana hawa wananchi wahatahitaji tena msaada wa polisi?
5. Mmeshawahi kusikia malalamiko ya hawa wananchi kwa vyombo husika.
Nami ni mwananchi wa kawaida lakini siungi mkono kujichukulia hatua mkononi
 
Jamani, maslahi ya Polisi ni duni saana though hii haijastify wao kuwanyanyasa wananchi.
Masuali ya kujiuliza:
1. Je wananchi hawavunji sheria hadi wanaomba rushwa?
2. Na km wamechoshwa na rushwa kwanini basi wasiache uvunjaji sheria?
3. Kuwapiga polisi ndio utatuzi wa matatizo yao au kujenga uhasama?
4. Inamaana hawa wananchi wahatahitaji tena msaada wa polisi?
5. Mmeshawahi kusikia malalamiko ya hawa wananchi kwa vyombo husika.
Nami ni mwananchi wa kawaida lakini siungi mkono kujichukulia hatua mkononi

Lakini wacha wapate kipigo, kwani wao wanapokuwa wanaenda kuwakamata watu ambao hwana hatia eti kwasababu kiongozi fulani kasema wakati wa kampeini, wao ubongo wao unakuwa umeahama?

Ebu rejea walivo enda kuwasweka ndani viongozi wa kanisa huko B'mlo ambao walizuia mkutano wa CCM kufanyika kanisani, nadhani polisi inabidi waadabishwe ili nao siku nyingine wajifunze kutumia ubongo wao kidogo!

Kama polisi wangekuwa waungwana hawatumiwi na viongozi kuwanyanyasa raia wema, basi wananchi wagekuwa na huruma nao, lakini wao wamejitenga na jamii na kuamua kuinyanyasa kwa amri za wakubwa, kwahiyo jamii ikiwageuka akili zitawarejea!
 
"In every action there is equal opposite reaction" Physics form two!!
Polisi wamezidi mno, kuna wakati nilienda village nikakuta polisi anatoka wilayani anaenda kijijini kuuliza insurance cover kwa trekta ambalo limepakiwa ndani (haliko barabarani) na leseni ya mwendashaji wakati trekta iko uani wanakijiji kwa ogopa kushikwa wanalipa mshiko (rushwa). Polisi wa mikoani wamezidi kunyanyasa wananchi hasa Arusha, Manyara na Dodoma (Self exprience). I support wananchi wajirekebishe.
 
hII NZURI KUSIKIA NA BADO KWA HAWA POLICE WA BARABARANI NAO WANAHITAJI KIPIGO KAMA HICHI.KWANI WANAPENDA KUPANDIKIZA MAKOSA KWENYE MAGARI YA WATU KISA WAPATE HELA KWA KWWELI INABIDI IFIKE SEHEMU TUWE TUNAADHIBU KILA KUKICHA.
ASANTE KWA TAARIFA ILIYOVUNJINVUJIKA.

Hili naliunga mkono, kama mwezi mmoja na nusu nyuma nilikuwa napita kwa shughuli zangu huko Katesh, mbele ya kituo cha polisi cha Katesh (barabara ya kutoka Singida) huwa kinawekwa kizuizi, Trafiki Polisi akanisimamisha, na maongezi yakawa kama hivi:

Polisi: Shikamoo Mzee
Mimi: Marahaba, pole na kazi
Polisi: Si unajuwa tena Mzee wangu, chumia juani ulie kivulini,
Mimi:Kweli kabisa
Polisi: Naomba Leseni Mzee
Mimi: Hii hapa
Polisi: anaifunguwa leseni anaitazama "Mbona nyepesi hii Mzee"
Mimi: Kwani kuna zingine huwa nzito?
Polisi: Si unajuwa tena Mzee, juwa kali?
Mimi: Hapa mna bahati, kituo cha polisi kipo karibu, hali ya hewa baridi, huko: nilikotoka (Dar) wenzenu ndio wanashinda kwenye joto kutwa.
Polisi: Kule lakini ma-kastama wengi.
Mimi: Kimya
Polisi: Naomba kadi ya gari
Mimi: Nikampa (original)
Polisi: Hii kadi mbona haijathibitishwa?
Mimi: Ithibitishwe na nani na hiyo ni orijino?
Polisi: Unajuwa Mzee siku hizi kuna mashine za kukopi zinatowa kadi kama orijino?
Mimi: Sijui hilo, ni vizuri kwa kunifahamisha.
Polisi: Itabidi hii kadi ikachunguzwe
Mimi: Sawa, ichukuwe niandikie barua ili nisisumbuliwe nnako kwenda mbele, uandike na jina lako na namba yako na sababu za kuizuwia hiyo kadi, unipigie na muhuri wa kituo chenu.
Polisi: Sawa, weka gari pembeni.
Mimi: Nikasogeza gari pembeni, bado kaishikilia leseni yangu na kadi yangu.
Polisi: Akalizunguka gari, halafu akatazama zinakobandikwa Insurance kwenye kioo cha mbele, akaniuliza iko wapi stika ya zima moto?
Mimi: Sina Stika ya zima moto na wala sijui kama kuna sheria ya kuweka stika ya zima moto.
Polisi: Kosa la pili hilo Mzee
Mimi: Sawa
Polisi:Unayo faya ekstingwisha?
Mimi: Nnayo, nikafungua gari langu nikamtolea
Polisi: Unazo trayengo?
Mimi: Nikafungua tena gari nikamtolea:
Polisi: Kwani unaenda wapi Mzee?
Mimi: Kwa leo naishia hapa Katesh
Polisi: Kwa hiyo huna haraka Mzee?
Mimi: Kijana, tafadhali niulize maswali yanayohusu kazi yako, kama umemaliza, niandikie karatasi ya kuchukuwa hiyo kadi unayokwenda kuichunguza.
Polisi:Unataka kunifundisha kazi yangu Mzee?
Mimi: Tafadhali fanya kazi yako.
Polisi: Unayo fasti aidi kiti kwenye gari?
Mimi: Kwa bahati nilikuwa nimefatana na Mama ambae ni daktari na alikuwa na box la mabandeji na madawa mengine kibao: Ndiyo nnayo fastoaidi kiti. Nikafunguwa tena gari nikamtolea box zima la madawa.
Polisi: Mbona hili boksi halina alama ya msalaba mwekundu?
Mimi: Nikaanguwa kicheko cha ajabu, hata sijuwi kilitoka wapi, nikamwambia mimi MuIslam situmii msalaba.
Polisi: Hatuongei mambo ya dini hapa, halafu unacheka nini?
Mimi: Niandikie makosa yangu, mpaka sasa sijui mangapi? wewe unakumbuka, huku naendelea kucheka.
Polisi: Itabidi, unisubiri.
Mimi: Naanza kushikwa na hasira, kijana sikiliza, nimekustahamilia muda mrefu naona unazidi, nikusubiri kwa sababu gani? sasa nnakuambia wewe kaa na hivyo vitu, mimi naondoka, lakini ntarudi hapa baada ya muda si mrefu namba jina lako na namba yako.
Polisi: Unataka kunitisha?
Mimi: Ndio, sasa nakutisha na ntakufanyizia kweli, namba za Mwema zipo kwenye simu yangu, nakwenda kuichaji ikiwaka tuu, utamjibu yeye. Kwaheri.
Polisi: Ngoja Mzee, mbona unahasira hivi, sisi tuko hapa kwa ajili yenu na kulinda usalama wenu.
Mimi: Nawasha gari
Polisi: haya chukuwa vitu vyako Mzee, samahani kwa usumbufu.
Mimi: Navipokea, huku naondoa gari na "Pumbafu" kubwa inanitoka.

Sasa jamani, askari kama huyu kwa nini asipigwe mawe mpaka kufa? anatafuta kila sababu ya kutaka rushwa!
 
Polisi wana usimamizi mbovu na hiyo imechangia kujisahau. Kawe polisi jamii wameokota silaha na kuripoti kituoni hakuna aliyejali. silaha ikachukuliwa na polisi wa oystabay ikaenda kwa mkuu wa kanda lakini mkuu wa kituo kawe hajui. Kuna polisi kawe?
 
Hili naliunga mkono, kama mwezi mmoja na nusu nyuma nilikuwa napita kwa shughuli zangu huko Katesh, mbele ya kituo cha polisi cha Katesh (barabara ya kutoka Singida) huwa kinawekwa kizuizi, Trafiki Polisi akanisimamisha, na maongezi yakawa kama hivi:

Dar Es Salaam!

Pole sana nimeamua nikupongeze hayo yote uliyoandika hapa ni ya kweli bila chumvi. Sisi tunaoendesha magari kama wapenzi tu na sio fani yetu hayo yamewahi kunikuta tena mara nyingi. Kwa hiyo kama Wizara hazitachukua hatua na kuanisha wajibu wa Askari pamoja na watendaji wengine wa umma kwa ujumla hivi vipigo vitaenda mpaka kwa Manesi na Madaktari hospitalini, wizara ya ardhi,manispaa zote na hata Ikulu!!!

Kwa mfano unakwenda TRA unapewa sticker ya road licence ambayo kwa masharti yao wanakuagiza uikate na kubandika upande wa kushoto wa kioo cha mbele cha gari period! Utaratibu wa zamani kabla ya kubadilika kwa mfumo wa namba na leseni inamtaka dereva atembee na kadi halisi kwenye gari au nakala halisi iliyothibitishwa.

Times have changed lakini kwa vile askari wa Trafiki wengi wao wamekulia police lines na elimu yao ya kupepea bado wanangangania uwepo wa Kadi ya kuandikisha gari ambayo haina mantiki kabisa. Kwenye sticker ya road licence kuna taarifa zote muhimu kuhusu gari isipokuwa tu ukubwa wa Engine(cc) na jina la mmliki ambalo kwa makusudi halikuwekwa kwa sababu za kiusalama.

Maswala ya kuwa na first aid kit pamoja na fire extinguisher ni ya lazima kwa PSV only kwa private vehicles hakuna mantiki in fact ni optional!! Hata kufunga mikanda ni elimu tu na ushauri kwani ni vigumu kuenforce this stupid policemen!!

Mbona mabasi yote ya abiria hayana mikanda but a stupid cop flags you to check if you have fastened your seat belt wanayo akili kweli au wanaganga njaa,, ni sawa kutoa elimu kwa umma but to enforce ni ndoto ya mchana . Mimi nikiwa highway to the regions where I can cruise ndipo mkanda unanijia hapa mjini kuna foleni and a lot of matuta ya viazi wanayoweka hawa wapumbavu wa TANROADS (engineers thinking politcally with instant theories)!!!
Lingine askari wa trafiki anakukuta na kosa anapaswa kukuandikia notification kama nni minor offence na dereva unapaswa kuiweka sahihi and then kwa mujibu wa sheria husika unapaswa kwenda kulipa internal revenue TRA na kwasilisha GRR !PERIOD!!! Within 20days endapo utakiuka wanapaswa kutoa warrant ya kukamatwa gari na mmliki na kupelekwa kwa pilato !! Huu wizi wa trafiki kukusanya pesa za serikali barabarani bila ya kukupatia GRR ni Ujambazi SUGU!!! NAWAOMBA mkatae ni wizi per se na mabosi wa trafic RTO hilo wanalijua fika HIZO pesa bila GRR wanazipeleka kwenye tumbo street!!

Sipendi kuvunja sheria but with this trend nawashauri madereva watembee na mikia ya taa kwenye magari a stupid question from a cop should be answered kwa bakora after all hawana pingu not armed and kwa unene wa matumbo yao ni bakora kwa kwenda mbele hata wakiwa kumi!!!
 
Mnaoshabikia tabia ya kujichukulia sheria mkononi nadhani hamjawahi kushuhudia huo ujinga. Ni ujinga huu ndio umesababisha kifo cha mwanafunzi wa Mzumbe ambaye licha ya kutokuwa na silaha yoyote wala kifaa chochote cha kufanyia uhalifu pamoja na ukweli kwamba alionekana kuwa ni mlevi, bado alisulubiwa na wanaojikulia sheria mikononi. Kwa msiojua madhara yake endeleeni kuchekelea huo upuuzi.
 
[
Sasa jamani, askari kama huyu kwa nini asipigwe mawe mpaka kufa? anatafuta kila sababu ya kutaka rushwa![/QUOTE]

Hicho ulichompa ndicho kichapo wanachostahili na siyo kuwapiga au kuwachoma moto
 
Back
Top Bottom