mirindimo
JF-Expert Member
- Nov 2, 2009
- 821
- 1,343
Naitwa Clement Nkwabi mkazi wa Geita. Napenda kukushirikisha suala la mdogo wangu Joel Raphael Nkwabi. Tarehe 15/12/2023 majira ya saa 2 usiku alienda kuangalia mpira lakini hakurudi. Tar.16 asubuhi mke wake alipigiwa simu na namba mpya. Kupokea ilikua sauti ya mumewe akimjulisha kuwa amelazwa hospitali ya wilaya ya Geita baada ya kupigwa risasi na polisi walipotoka kuangalia mpira.
Alimuomba mkewe ampelekee nguo za kubadilisha kwani alizokuwa nazo zimechafuka damu sana. Mke alipokea taarifa hiyo kwa mshtuko na kuwajulisha ndugu wengine wa mume. Wakaenda hosptalini ambapo walikumkuta yupo chumba cha Emergency. Wakamkabidhi nguo na kumuuliza imekuwaje.
Akamjibu kuwa walipotoka kutizama mpira, walivamiwa na watu ambao hawakujitambulisha. Wakawataka walale chini. Wakahisi ni majambazi hivyo wakakimbia ili kujinusuru. Lakini watu hao wakafyatua risasi.
Wenzie walikimbia lakini yeye alijeruhiwa kiunoni. Risasi ikabaki mwilini. Akakimbizwa hospitalini na tar.16 akafanyiwa operation kuitoa. Mke aliambiwa mumewe kapigwa risasi na askari wa mali asili. Alipouliza sababu akaambiwa ataifahamu mahakamani.
Kesho yake mke alimpelekea chai mumewe lakini hakumkuta hospitalini. Alipouliza akaambiwa aende kituo cha Polisi Geita. Akaenda lakini hakumkuta. Akaambiwa labda amepelekwa kituo cha Kasamwa, nako hakumkuta. Akaambiwa ajaribu kituo cha Katoro, lakini huko nako hakumkuta.
Tarehe 19/12/2023 mkewe aakapigiwa simu na namba mpya. Ilikua sauti ya mumewe ikimueleza kwamba yupo kituo cha polisi Buseresere, akilalamika yupo kwenye maumivu makali kwani alitoroshwa hospitali baada tu ya operation. Alidai hakuna dawa yoyote aliyopewa zaidi ya kutolewa ile risasi, na huko mahabusu hapati matibabu yoyote. Kesho yake mkewe allienda Buseresere lakini polisi wakakanusha kumshikilia. Akarudi nyumbani bila matumaini.
Na tangu wakati huo hajasikia tena sauti ya mumewe. Ndugu zake hatujui kama yupo hai au amekufa. Hatujui kwanini alipigwa risasi? Kwanini alitoroshwa hospitali? Kwanini hakupewa haki ya matibabu? Hata kama ni mtuhumiwa si angetibiwa kwanza halafu ashtakiwe? Tunaomba utupazie sauti ili ndugu yetu aweze kupata haki yake. Au kama amekufa watupe maiti tuzike, tujue moja.