astalavista
Senior Member
- Jul 7, 2014
- 156
- 159
POLISI_WANAHABA RI_SERIKALI. Kwanza niweke wazi kwamba nina maslahi na Wanahabari,ndio nina maslahi nao kwasababu mimi pia ni mmoja wa familia hiyo.. Jana kwa mara nyingine Tanzania ilishuhudia uhusiano mbovu kati ya Wanahabari na Watu wa Usalama(Polisi) .
Kupitia vyombo mbalimbali vya habari nilishuhudia wanahabari wakiongea kwa uchungu kiasi cha kupelekea kutoa machozi kuafuatia kupigwa kwa baadhi ya wenzao..INAUMIZ A NA KUSIKITISHA. Lakini nataka kusema kitu kwa Wanahabari hapa nchini,muda mrefu tumekuwa tukilalamika kwamba Serikali inanyima uhuru kwa vyombo vya habari tofauti na ilivyo andikwa katika katiba (act18 Freedom of êxpression).
Nataka kusema tumekuwa tunasahau kupigia kelele vitu vingine muhimu ambavyo vitakua nyenzo rahisi zaidi katika ufanisi wetu wa kazi(mfano kwa tukio lile la jana). Kuna msemo mmoja kwa wanahabari kwamba kutembea bila ya kuwa na KALAMU na KARATASI ni sawa na Mwanajeshi kwenda vitani bila kuwa na SILAHA.
Hii kauli sio mbaya,lakini lazima tukumbushane kwamba kuna mazingira yanatubidi kuwa na zaidi ya Kalamu na Karatasi. Ukweli ni kwamba kwenye matukio ambayo yanakuwa na hali ya vurugu na hatari zisizojulikana kama yale ya jana ni ngumu kwa watu wa usalama kutambua yupi ni mwanahabari na yupi si mwanahabari.
Kwa jinsi hali ilivyo sasa kubeba kamera pekee haitoshi kuwashawishi wanausalama kutambua wanahabari,na kwa mazingira hayo ya vurugu tusitegemee watu wa usalama kuomba vitambulisho vya kazi(huo muda hakuna). Kufuatia tukio la jana na matukio mengine huko nyuma,nafikiri sasa wanahabari umefika wakati wa kupaza sauti kwa wahusika wa vyombo hivyo vya habari kupatiwa mavazi maalumu kwa shughuri malumu kama hizo.
'PRESS JACKET' tujiulize wangapi wanayo? Kina nani walivaa ama wanavaa katika matukio kama yale?Kwanini hatuna? Na je hayana umuhimu kweli?. Tukubali sasa kwamba hata kwa upande wetu kuna upungufu katika vitendea kazi. Hata wanajeshi wakienda vitani wanakuwa tofauti na siku za kawaida. Hata watu wa afya kuna mazingira wanakuwa tofauti na siku za kawaida(mf' wale wa Ebola).
Kwanini si wanahabari?
Tunafanya kazi kwa mazoea sana.
Wasallam.