BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,377
- 8,121
Uchunguzi huo utafanywa na Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai kwa kushirikiana na Taasisi nyingine za Uchunguzi na Fedha ili hatua stahiki za kisheria ziweze kuchukuliwa.
Msemaji wa Jeshi hilo, David Misime ametoa tahadhari na kusema "Ni lazima kila mmoja wetu atambue kuna matapeli, usalama wa fedha au mali yako unaanza kwanza na wewe mwenyewe, hakuna utajiri au kujipatia fedha kwa njia rahisi kiasi hicho bila kutoka jasho kwa kufuata sheria".
Kampuni ya Kalynda E-Commerce inatuhumiwa kuendesha biashara za Upatu na kuwadhulumu wawaliokuwa wateja wake kiasi kikubwa cha fedha na kutoweka katika mazingira ya kutatanisha.
======================
Jeshi la Polisi Tanzania limesema,kutokana na baadhi ya Wananchi kulalamika kutapeliwa fedha zao na kampuni ya Kalynda E Commerce kwa njia ya mtandao, Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai kwa kushiriana na Taasisi nyingine za kiuchunguzi na za kifedha wameanza kuchunguza malalamiko hayo ili hatua stahiki za kisheria ziweze kuchukuliwa.
Msemaji wa Jeshi la Polisi, David Misime amesema “Wakati hatua hizo zinaendelea kuchukuliwa, Jeshi la Polisi lingependa kutoa tahadhari kwa mara nyingine kwa Watanzania, tahadhari zilishawahi kutolewa kuanzia sakata la kampuni nyingine ambazo ziliwahi kujinasibu kutoa huduma kama hizo lakini waliojiingiza waliambulia kupoteza fedha na mali zao”
“Jambo la kujiuliza, kama hayo wanayokuvutia nayo ni ya kweli, kwanini wasiwahamasishe ndugu zao na ukoo wao wakatajirika kama wanavyo kudanganya?, hiyo huruma kwako wewe ambaye hamfahamiani inatoka wapi?”
“Ni lazima kila mmoja wetu atambue, kuna Matapeli na usalama wa fedha au mali yako unaanza kwanza na wewe mwenyewe, hakuna utajiri au kujipatia fedha kwa njia rahisi kiasi hicho bila kutoka jasho kwa kufuata sheria,
“Tukumbuke Matapeli hao wapo watakaokuvuta kwa kukupa fedha na faida kama walivyokutangazia kupitia mitandao lakini lengo ni ili uweke kiasi kikubwa zaidi wakupige vizuri au wachukue fedha zako au wawapige utakao wahamasisha kujiunga nao”