BRELA: Kalynda ilipewa leseni ya kuuza vifaa vya kielektroniki

Kingsmann

JF-Expert Member
Oct 4, 2018
4,448
16,314
Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) imesema leseni ya kampuni iitwayo Kalynda E-Commerce Limited iliyotolewa Juni 21, 2022 ni kwa ajili ya uuzaji wa jumla wa vifaa vya kielektroniki na mawasiliano pamoja na ufanyaji wa biashara ya kiteknolojia ya kimataifa mtandaoni.

BRELA imesema kumekuwa na taarifa zinazoleta taharuki kuhusu kampuni hiyo kufanya biashara ya upatu ya kukusanya fedha kutoka kwa wananchi kwa ahadi ya kupata faida ndani ya muda flani kinyume na bidhaa au huduma iliyoombewa leseni.

Taarifa ya BRELA imesema leseni ya biashara ya Kalynda E-Commerce Limited inamruhusu kufanya biashara ya masoko na mauzo ya bidhaa kwa njia ya mtandao pekee, hivyo ufanyaji wa biashara kinyume na leseni iliyotolewa ni kosa la jinai chini ya kifungu cha 19 cha sheria ya leseni za biashara, Sura Na. 208.

Aidha, Wakala imetoa angalizo kwa umma kuwa kabla ya kuingia kwenye mahusiano ya kibiashara na kampuni yoyote ni vema kupata uthibitisho wa uhalali na uwepo wa kampuni hiyo pamoja na biashara husika kutoka BRELA na mamlaka nyingine za Serikali.

Swahili Times.

--
1.jpg
2.jpg
 
Hata matangazo ya ITV , ya hao Kalynda - yalikuwa hayaonekani kwa BRELA ?

Yawezekana ni mradi wa kigogo serikalini , kwa sababu kampuni ina leseni zaidi ya 3 , zote zimetoka serikalini na zinaoneshwa public na pili matangazo yao yalikuwa wimbo ITV
 
Hata matangazo ya ITV , ya hao Kalynda - yalikuwa hayaonekani kwa BRELA ?

Yawezekana ni mradi wa kigogo serikalini , kwa sababu kampuni ina leseni zaidi ya 3 , zote zimetoka serikalini na zinaoneshwa public na pili matangazo ya yalikuwa wimbo ITV
Jiongeze basi hapo kuna mtu mzito wewe

Brela wamepiga chenga ya mwili habari imeisha hiyo

Tatizo mnaendeshwa na tamaaa zitawauwa

Subirini tubuni mchezo mwingne lazima tuwapate wajinga wengine tena
 
Hata matangazo ya ITV , ya hao Kalynda - yalikuwa hayaonekani kwa BRELA ?

Yawezekana ni mradi wa kigogo serikalini , kwa sababu kampuni ina leseni zaidi ya 3 , zote zimetoka serikalini na zinaoneshwa public na pili matangazo ya yalikuwa wimbo ITV
Tambua itv n kampun ya biashara wao Kaz yao n kupokea matangazo yaliyolipiwa

Jukumu la kujua biashara n halali au siyo halali si lao zpo mamlaka zenye jukumu Hilo

Nadhan watanzania uelewa wetu n mdogo Sana kuhusu majukumu ya vyombo mbalimbali vya serikal na binafsi

Lakin pia alert ilitolewa humu watu hawakuelewa kitu

Mambugila nchi hii hawawez kuisha

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Brela wanaibuka kusema hayo baada ya watu kulizwa. BRELA walikuwa wapi siku zote wakati Kalynda wakipiga promo na watu wakijiunga?
 
Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) imesema leseni ya kampuni iitwayo Kalynda E-Commerce Limited iliyotolewa Juni 21, 2022 ni kwa ajili ya uuzaji wa jumla wa vifaa vya kielektroniki na mawasiliano pamoja na ufanyaji wa biashara ya kiteknolojia ya kimataifa mtandaoni.

BRELA imesema kumekuwa na taarifa zinazoleta taharuki kuhusu kampuni hiyo kufanya biashara ya upatu ya kukusanya fedha kutoka kwa wananchi kwa ahadi ya kupata faida ndani ya muda flani kinyume na bidhaa au huduma iliyoombewa leseni.

Taarifa ya BRELA imesema leseni ya biashara ya Kalynda E-Commerce Limited inamruhusu kufanya biashara ya masoko na mauzo ya bidhaa kwa njia ya mtandao pekee, hivyo ufanyaji wa biashara kinyume na leseni iliyotolewa ni kosa la jinai chini ya kifungu cha 19 cha sheria ya leseni za biashara, Sura Na. 208.

Aidha, Wakala imetoa angalizo kwa umma kuwa kabla ya kuingia kwenye mahusiano ya kibiashara na kampuni yoyote ni vema kupata uthibitisho wa uhalali na uwepo wa kampuni hiyo pamoja na biashara husika kutoka BRELA na mamlaka nyingine za Serikali.

View attachment 2384974

Swahili Times.
wajinga ndio waliowahi
 
Tambua itv n kampun ya biashara wao Kaz yao n kupokea matangazo yaliyolipiwa

Jukumu la kujua biashara n halali au siyo halali si lao zpo mamlaka zenye jukumu Hilo

Nadhan watanzania uelewa wetu n mdogo Sana kuhusu majukumu ya vyombo mbalimbali vya serikal na binafsi

Lakin pia alert ilitolewa humu watu hawakuelewa kitu

Mambugila nchi hii hawawez kuisha

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
Kwa hio naweza kwenda kutangaza biashara za.magendo ITV kisa wanafanya biashara za matangazo?
 
Back
Top Bottom