Polisi wa AIRPORT MNUKO WA RUSHWA TUPU

ngoshwe

JF-Expert Member
Mar 31, 2009
4,131
931
Wakati mwingine askari polisi wa usalama barabarani wanashindwa kukaa barabarani badala yake wanajificha kwenye vibanda kuvizia madereva wafanye kosa ili waombe “posho”. Wiki iliyopita nilikuwa na jamaa mtukutu, aka "U-turn" kwenye mapishano ya kuingilia MNI Airport Dar katika barabara ya Nyerere, kumbe askari wa usalama barabarani wamejificha wanavizia posho, ghafla askari polisi akaibuka kwenye vibanda na kuanza kukimbilia barabarani klwa kasi ya ajabu akiwa na kofia mkononi ili kumpiga mkono, jamaa alipomwona akaongeza mwendo na kumwacha akiwa anapunga mkono tu huku kachama kinywa, kapoteza “posho”..

Leo naingia tena hapa Airport, ghafla naona Binti amevalia bluzi nyeupi na sketi ya kibluu ya khaki...anapunga mkono karibia na kuingia getini ambapo wateja wanachukulia kadi kwenye mashine ya kuruhusu kuingia uwanjani, nasimama kwa utii wa amri ya dola, nauliza ati kulikoni afande?..yupo “siriasi” anajibu ..nimekusimamisha nikukagee, …mara anaomba tufungue milango ya gari..anaulizaz kwenye begi kuna nini.., anadai anataka kukagua mizigo..nauliza huu ukaguzi wan je ya geti umeanza lini?..anajibu… nakagua , ni wajibu wetu ..hafungui begi anauliza nani anasafiri wewe au mkeo…namwambia mimi..anataka kukagua pochi ya mamsapu ..namwambia wewe mbona ueleweki,…unakagua nini?...anauliza..."naomba leseni yako'.." hasira zinanishika namjibu ..unanichelewesha..ebu sema unachotaka..anasema "leseni mzee" akisitasita, wakati huo huo magari mengine yanapita hayakaguliwi......hauliza mbona hayo hukagui? hana jibu...naishiwa uvumilivu namuuliza wewe unajuia kazi yako?..kwa hasira naondoa gari akiwa amesimama tu hana la kusema..eti huyu nae anataka rushwa kwenye geti..
 
Code:
..eti huyu nae anataka rushwa kwenye geti..
Mkuu,
Na yeye hapo ndio madhabahuni pake!...
Lakini kwa uwoga wa kibongo huwa tunastawisha sana biashara cgafu za hawa maaskari kwa kuwapa senti bila sababu!
Huyo anaonesha ungemtishia kidogo tu angeomba msamaha sana!
 
Mi nilipoona neno "mnuko" akili yangu yote inakaenda kwenye kikwapa! Kumbe ni rushwa inayozungumziwa.
 
Pole sana! Kuna polisi wengine wasumbufu sana hapo airport ukiwa unatoka safari ukifika nje wanakufata wanakuomba Passport ukiwaliza ya nini wakati nimeishagongewa ndani, wanasema wao ni wazee kitengo
 
Ulifanya vizuri kumuacha hapo maana hana cha kufanya na labda hata hakupangiwa awe pale kikazi.
 
Si nauliza tu?

Maana hakuna cha ajabu, nilikutana na mmoja ana fetish ya maskio!

Well, sikuona alama ya swali. Lakini kukujibu swali lako ni kwamba hapana. Sina fetish ya vikwapa (ingawa baadhi ya watu kama Zakumi na Companero wanazo). Nina fetish na boobies lol...or is this TMI?
 
Fetish ya boobies is way too common......Booooring! Lol

Way to go for Zakumi na Companero though sipati picha huwa wanafanya nini na hizo kwapa! :]
 
Back
Top Bottom