Polisi, TCRA wazungumzia akaunti ya Mange Kimambi

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,557
21,515
1.jpg

Jeshi la Polisi limetaka liachwe liendelee kufanya kazi yake kwa weledi katika kushughulikia suala la Mtanzania aishiye ughaibuni, Mange Kimambi, ambaye anatuhumiwa kuchapisha taarifa zinazodaiwa kuwatusi mitandaoni watu mbalimbali wakiwamo viongozi.

Akizungumza na Nipashe kuhusiana na uwezekano wa wao kuifunga akaunti ya Kimambi ikiwa sehemu ya hatua wanazochukua kwa sasa, Msemaji wa Jeshi la Polisi, Barnabas Mwakalukwa, alisema ni kweli jeshi lao linalifanyia kazi suala hilo.

Hata hivyo Mwakalukwa hakutaka kukubali au kukataa juu ya kile kilichodaiwa kutokea kwenye akaunti ya Kikambi na badala yake kutaka apewe muda wa kulifanyia kazi ndipo alitolee maelezo ya kina.

“Hili jambo lina mambo mengi sana. Watu wengi wanahusika na taasisi nyingi (pia) zitahusika kulishughulikia, Hivyo tunaendelea kupokea mawazo ya watu mbalimbali kuhusu namna ya kwenda nalo… mawazo wanayotupa tunayafanyia kazi lakini naomba mtuache kwanza tunaendelea kulishughulikia,” alisema Mwakalukwa.

Aidha wakati Msemaji wa Polisi akisema hayo, TCRA ilisema kuwa haiwezi kufunga wala kuingilia akaunti ya Kimambi kwa sababu huo siyo wajibu wake kisheria.

Msemaji wa TCRA, Semu Mwakyanjala, aliiambia Nipashe kuwa mamlaka yao haina nguvu za kisheria kufanya kazi hiyo bali wenye wajibu wa kufanya hivyo ni kitengo cha kudhibiti uhalifu wa mitandaoni cha Jeshi la Polisi.

Akifafanua zaidi, msemaji huyo alisema makosa yote yanayohusu mitandao, yakiwamo ya watu kutishiwa maisha, kutukanwa, kuibiwa kwa njia ya mtandao au kunyanyaswa kwa namna yoyote mtandaoni, wanaohusika ni polisi na siyo TCRA.

“Masuala ya akaunti za watu kwenye mitandao kama hiyo unayosema (ya Kimambi)… mwenye mamlaka ya kuingia na kuzifunga ni Jeshi la Polisi. Bunge liliipa mamlaka ya kisheria polisi kuchunguza na kukamata wahalifu kama hao… waulizeni wao,” alisema Mwakyanjala.

Hata hivyo zipo taarifa mitandaoni zilimkariri Mtanzania huyo aishiye Marekani kuwa kilichotokea ni matokeo ya kazi ya wadukuzi wa mitandaoni, maarufu kama ‘hackers’ kupoteza akaunti yake yenye wafuasi takribani milioni 1.5.

Pamoja na hayo upo ujumbe wa lugha ya kigeni uliokuwa ukisambaa kwenye mtandao wa instagram ukionyesha kuwa akaunti inayofahamika kuwa ni ya Kimambi, imefungwa na waendeshaji wa mtandao wa Instagram kwa sababu ya kuwapo kwa malalamiko dhidi ya machapisho ya akaunti hiyo.

Chanzo: Nipashe
 
Ingawa simfahamu huyo binti.....lakini mtiririko wa wingi wa habari kumhusu huyo binti.....hasa kwenye masuala ya kitaifa......ni ishara kuwa tunaishi kwenye taifa lenye viongozi au watawala wasiokuwa na ajenda na mikakati ya kutawala na wasiokuwa na vipaumbele kama taifa........

Watu aina ya huyo binti wapo kila taifa duniani.....lakini kwa kuwa mataifa hayo yana mambo mengi ya kufanya kama ajenda za taifa lao....kamwe hawawezi kuhangaishwa na jambo dogo kama hilo.........

Lazima tutambue kuwa tunaishi kwenye nyakati za mwangaza.....nyakati za taarifa kiganjani.....

Pia tunaishi katika ulimwengu ambao kila mtu ana mtazamo tofauti na kila mtu ana mtindo wake wa kutoa maoni yake......tunapaswa kuukubali ukweli huo ili maisha yaendelee......
 
Tuacheni kudanganyana... Yaani polisi wa tz anaweza ingia na kufunga account ya mtu ya INSTAGRAM?? mbona wanatufanya watoto hawa policcm??

Ivi FB na instagram ambao wanawekeza mamilioni ya dola kwenye security ya server zao alafu leo policcm aje ku hack kipuuzi tu!!!

Kuingia kwenye account ya mtu na kuifunga ina maana wana uwezo wa ku hack server za instagram au facebook huko marekani kitu ambacho si kweli!!

Kama wana uwezo wa kuingia na ku hack account ya insta kwann wameshindwa ku hack server za jf mpaka wakaanza kimbizana mahakamani??

Yaan umeshindwa kuingia na kupata data za member wa jf utaweza kuingia na kufunga account ya mtu wa insta?? Acheni upuuzi basi nyie policcm!!
 
Policcm wa wanadhidi kujidalilisha, badala ya kujikita kwenye mambo ya muhimu wao wamejikita kwenye udaku.Polisiccm nao wanafuatilia udaku wa Mange, Poor Policeccm walioshindwa kuwakamata watu waliotaka kumuua Lissu wataweza kumkamata Mtu aliye US? Huyu Mzee wakitengo cha propaganda cha Policcm Mr. Siro inaelekea akiwa ofisini kwake anashinda na account ya Mange kusoma udaku kama Zee la Magogoni linavyofuatilia udaku udaku. Sishangai kuwa na Taifa la watu wanaopenda udaku udaku
 
Ingawa simfahamu huyo binti.....lakini mtiririko wa wingi wa habari kumhusu huyo binti.....hasa kwenye masuala ya kitaifa......ni ishara kuwa tunaishi kwenye taifa lenye viongozi au watawala wasiokuwa na ajenda na mikakati ya kutawala na wasiokuwa na vipaumbele kama taifa........

Watu aina ya huyo binti wapo kila taifa duniani.....lakini kwa kuwa mataifa hayo yana mambo mengi ya kufanya kama ajenda za taifa lao....kamwe hawawezi kuhangaishwa na jambo dogo kama hilo.........

Lazima tutambue kuwa tunaishi kwenye nyakati za mwangaza.....nyakati za taarifa kiganjani.....

Pia tunaishi katika ulimwengu ambao kila mtu ana mtazamo tofauti na kila mtu ana mtindo wake wa kutoa maoni yake......tunapaswa kuukubali ukweli huo ili maisha yaendelee......
Mchango uliotukuka
 
HOW COMES IT WA BONGO WAIFUNGE ACCOUNT INSTAGRAM

AMBAYO SERVER ZAKE ZIKO MAREKANI NA SYSTEM ADMN YUPO MAREKANI.

YAANI MTU YUPO MAREKANI ANA CREATE ACCOUNT AKIWA MAREKANI SERVER ZIPO MAREKANI DAH HALAFU IT WA BONGO ANAKUJA KUIFUNGA.

BADO SIAMINI AMINI LABDA ACCOUNT YAKE WSIBLOCK HAPO SAWA
 
Ingawa simfahamu huyo binti.....lakini mtiririko wa wingi wa habari kumhusu huyo binti.....hasa kwenye masuala ya kitaifa......ni ishara kuwa tunaishi kwenye taifa lenye viongozi au watawala wasiokuwa na ajenda na mikakati ya kutawala na wasiokuwa na vipaumbele kama taifa........

Watu aina ya huyo binti wapo kila taifa duniani.....lakini kwa kuwa mataifa hayo yana mambo mengi ya kufanya kama ajenda za taifa lao....kamwe hawawezi kuhangaishwa na jambo dogo kama hilo.........

Lazima tutambue kuwa tunaishi kwenye nyakati za mwangaza.....nyakati za taarifa kiganjani.....

Pia tunaishi katika ulimwengu ambao kila mtu ana mtazamo tofauti na kila mtu ana mtindo wake wa kutoa maoni yake......tunapaswa kuukubali ukweli huo ili maisha yaendelee......
Huu mchango unaweza kuukopea mkopo bank
 
Kama kawaida yao polisi wana dedicate resources kibao kwenye mambo yasiyo na umuhimu wowote isipokua tu kumfurahisha mkuu. Kuhusu uwezo wao wa ku hack account ya instagram hawana uwezo huo ila wanaweza kulipa watu wenye ujuzi kutoka dunia ya kwanza kufanya hiyo kazi. Haitakua mara ya kwanza kwa polisi na watu wa "kitengo" kulipia "malicious services" kutoka nje
 
Watu wanafik
Ntatoa zawadi nono Mwakyanjala na huyo Mwaki mwingine mkiweza kufunga account ya Instagram mnacheza na taaluma za watu ninyi...
Polisiccm wanafikiria kupiga watoto na akina mama mabomu ya machozi wamemaliza taaluma zote duniani.
Anyways polisiccm zaidi ya Tanzania open University wanaweza kusajiliwa wapi kujiendeleza kielimu?maana polisiccm wengi ni standard seven na form four failure
 
Back
Top Bottom