Polisi kuwakamata wabunge wa CHADEMA waliokatwa mapanga!

JESHI la Polisi Mkoani Mwanza, limeanza kuonekana kutaka ‘kuwageuzia kibao’ wabunge wawili wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mkoani Mwanza, waliovamiwa na kukatwa mapanga na watu wanaodaiwa ni wafuasi wa CCM, kwani polisi wanatarajia kuwakamata wabunge hao kuhusiana na tukio la kukatwa kwao mapanga usiku wa kuamkia Jumapili ya Aprili mosi, 2012. Siku hiyo, ilikua ni siku ya upigaji kura katika kata ya Kirumba mkoani Mwanza, ambako wabunge hao Highness Kiwia wa jimbo la Ilemela na Salvatori Machemli ambaye ni mbunge wa jimbo la Ukerewe walikuwa miongoni mwa viongozi waandamizi walioshiriki kampeni na mikakati ya chama
hicho katika uchaguzi wakiongozwa na Naibu Katibu Mkuu wao, Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe. Mgombea wa Chadema Dany Kahungu ameibuka na ushindi katika uchaguzi huo wa Udiwanai kata ya Kirumba. Polisi imesema, inaweza kuwakamata wabunge hao, wakiwa bado wamelazwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ya jijini Dar es Salaam wanakopatiwa matibabu, au inaweza kuwasubiri watoke hospitalini kisha iwakamate, huku wabunge hao wakiwashutumu polisi kuhusika na uvamizi huo kutokana na kushindwa kuchukua hatua kwa wahusika wanofahamika. Mkuu wa Upelelezi wa Jinai (CID) wa Jeshi la polisi Mkoani Mwanza (RCO), Deusdedith Nsimeki, amesema, inabidi wabunge hao wahojiwe kwani ndiyo wanaweza kuwa chanzo na watuhumiwa wa kwanza katika ghasia hizo zilizotokea usiku wa kuamkia Aprili Mosi mwaka huu katika eneo la Ibanda Kabuholo, Kirumba jijini Mwanza. “Hawa wabunge lazima tuwakamate watueleze vizuri kuhusiana na tukio la kukatwa kwao mapanga usiku. Watueleze kwa nini walienda huko Kabuholo gizani usiku tena bila kutoa taarifa polisi?. “Kukatwa kwao mapanga isiwe sababu ya kutokamatwa na polisi, lazima tuwakamate tuwahoji. Inawezekana wabunge hawa ndiyo chanzo kikubwa katika kesi hii. “Tunaweza kuwakamata wakiwa wamelazwa hospitalini huko huko, au tukaamua kuwasubiri watoke hospitalini halafu tuwakamate!. Sheria zinaturuhusu sisi kumsomea mashtaka mtu yeyote hata kama kalala kitandani”, alisema RCO Nsimeki ambapo alitania kwa kusema: “Unajua mtu anaweza kukutwa na mke wa mtu akakatwa mapanga na kichwa kikaning’inia, sasa utasema huyo mtu si chanzo?”. Hata hivyo, mwandishi wa habari hizi alipomuuliza RCO Nsimeki iwapo kuna watu wamekamatwa na polisi kuhusiana na tukio hilo la wabunge kukatwa mapanga na kuumizwa sehemu mbali mbali za miili yao alisema, hakuna mtu hata mmoja aliyekamatwa hadi kufikia jana
jioni. “Hatujakamata mtu yeyote kuhusiana na tukio hili. Lakini tulishaanza kazi yetu ya upelelezi na tutawakamata tu hilo halina tatizo”, alisema Mkuu huyo wa Kitengo cha Upelelezi Makosa ya Jinai Mkoani Mwanza. Kitendo cha jeshi la polisi mkoani Mwanza kushindwa kuwakamata watuhumiwa wa
tukio hilo, inaweza kuwashangaza watu wengi, ikizingatiwa na uzito wa tukio lenyewe. Aprili Mosi mwaka huu, usiku wa kuamkia upigaji wa kura katika uchaguzi mdogo wa Kata ya Kirumba, wabunge hao walitekwa na kundi la watu wanaodaiwa kuwa ni wafuasi wa CCM, wakati wabunge hao na makada wengine wa Chadema wakidaiwa walikuwa wakiwasambaza mawakala wa chama chao kurudi majumbani kwa ajili ya kujiandaa kwenda kusimamia kura za mgombea wa Chadema Kata ya Kirumba, Dany Kahungu katika uchaguzi huo mdogo. Katika tukio hilo, Mbunge wa Ilemela, Kiwia ndiye aliyeumizwa zaidi kutokana na
kupata majeraha makubwa sehemu mbali mbali za mwili wake ikiwemo sehemu ya kichwani na mgongoni, ambapo alilazimika kukimbizwa katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando (BMC), ya jijini Mwanza kwa matibabu zaidi, huku Machemli akikimbizwa Sekou Toure. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Liberatus Barlow (RPC), aliwathibitishia waandishi wa habari juzi na kusema kwamba: “Ni kweli wabunge hao wamevamiwa na kujeruhiwa kwa mapanga usiku, na sisi tulipokea taarifa kuwa wafuasi wa CCM wamewateka na kuwaweka chini ya ulinzi wabunge watatu wa Chadema, Kiwia, Wenje na Machemli”. Alisema baada ya kupata taarifa hizo, muda mfupi polisi walifanikiwa kufika eneo la tukio na kuwakuta wabunge hao ambao wakiwa wamewekwa chini ya ulinzi na
wafuasi hao wa CCM, ambapo polisi walipambana na kufanikiwa kuwaokoa. Kamanda Barlow aliwataja majeruhi wengine watatu waliokimbizwa katika hospitali ya mkoa ya Sekou Toure na kulazwa kuwa ni pamoja na Haji Mkwenda (21), ambaye amevunjika mguu wa kulia, Judith Madaru (26), ambaye amechomwa kisu sehemu ya ziwa upande wa kushoto na Ivori Festo Machimba (26), ambaye amejeruhiwa kichwani na mdomoni. Alitaja namba za magari yaliyokutwa kwenye eneo la tukio kuwa ni pamoja na T 377 ARF linalomilikiwa na mbunge Kiwia, T 729 DAD linalomilikiwa na Mohamed Juma pamoja na T 397 ANU aina ya Land Cruiser ambalo mmiliki wake hakupatikana. Wabunge hao wamehamishiwa hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa matibabu zaidi, ambako hali zao zinaelezwa kuendelea vyema, huku wote wawili wakishangazwa na kitendo cha polisi kushindwa kuwakamata watuhumiwa. Katika maelezo yake mtandaoni, Zitto Kabwe alisema mmoja wa majeruhi ni kiongozi wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) ambaye upo uwezekano wa kuwa alipigwa na wenzake katika vurugu hizo, na aliwaomba polisi kutomruhusu kutoka hospitalini.
“Kuna mmoja wa majeruhi ambaye yupo hapa mwanzoni alisema yeye ni mtu wetu na ameumizwa pia. Imegundulika ni mtu wa UVCCM, Ahmed Mkilindi ambaye ndiye alikuwa anaongoza kikosi kilichowavamia kina Kiwia. Amepata jeraha mkononi (friendly fire?). Mwenyekiti wa CCM mkoa yupo hapa kaja kumwona. Nimewaambia Polisi mtu huyu asitolewe hospitali kinyemela bali atoe maelezo polisi kwanza. Huyu ni mtuhumiwa wa kwanza kabisa. Hali ya Kiwia sio nzuri sana. Anatakiwa kufanyiwa ct scan kuona athari aliyopata (maana kapigwa na shoka na mapanga
kichwani). Bahati mbaya hapa Bugando kifaa hicho hakifanyi kazi,” alisema Zitto kabla ya wabunge hao kuhamishiwa Dar es Salaam. Zitto aliendelea kwa kusema, “Siasa za Tanzania zinazidi kujidhihirisha kuwa hazina tofauti na nchi nyingine za Kiafrika. Chama cha siasa kuwa na makundi ya wahuni na kupiga watu ni hatari na chama hicho kinakosa ‘moral’ authority ya kutawala. Tusubiri uchunguzi zaidi wa Polisi.
 
Hawa police mie nashindwa kuwaelewa kabisa hivi nini hasa hawapendi wapinzani wanaogopa nini wapinzani wakishinda,kazi kuonea tu watu ambao wako innocent wameshindwa kukamata wezi wa EPA nk,angalia kule Arusha walimkamata yule wakili machachari ati wamemkuta ana hela kibao kwa acc hivi na yule mse.....nge Andrew Chenge na ile mijifweza kibao tena kaiita vijisenti mbona hawajamkamata hadi leo kulikoni kuonea watu ambao hawako serikalini???Na ole wenu nyie Police Chdema tuchukue nchi 2015 amtatafuta kwa kwenda na hata kabla ya Dr Slaa kuapishwa tutakuwa tumefunga mipaka yote hakuna tigo yoyote atakaetoka baada ya hapo ni Konga,Segedansi,keko na kwingineko ole wenu siku ikifika mtalipa yote mliyokuwa mkifanya
 
Inashangaza eti watu wa ccm waliwapigia simu wakiwa wamewaweka chini ya ulinzi pasipo kuwakamata hao watu wa ccm jeshi la polisi linajipunguzia uaminifu mbele ya watz wangefanya hivyo watu wa upinzani tungesikia wamekamatwa
 
Wakamatwe kama watuhumiwa au wahojiwe kama sehemu ya tukio? kama kulikuwa na ghasia kama anavyosema jamaa wa upelelezi mwanza, kwa nini polisi hawakufika kutuliza vurugu kama kawaida yao?mh, mambo ya ngosweeeeeee.....
 
Mkuu wa Upelelezi wa Jinai (CID) wa Jeshi la polisi Mkoani Mwanza (RCO), Deusdedith Nsimeki, amesema, inabidi wabunge hao wahojiwe kwani ndiyo wanaweza kuwa chanzo na watuhumiwa wa kwanza katika ghasia hizo zilizotokea usiku wa kuamkia Aprili Mosi mwaka huu katika eneo la Ibanda Kabuholo, Kirumba jijini Mwanza. "Hawa wabunge lazima tuwakamate watueleze vizuri kuhusiana na tukio la kukatwa kwao mapanga usiku. Watueleze kwa nini walienda huko Kabuholo gizani usiku tena bila kutoa taarifa polisi?.
"Kuna mmoja wa majeruhi ambaye yupo hapa mwanzoni alisema yeye ni mtu wetu na ameumizwa pia. Imegundulika ni mtu wa UVCCM, Ahmed Mkilindi ambaye ndiye alikuwa anaongoza kikosi kilichowavamia kina Kiwia. Amepata jeraha mkononi (friendly fire?). Mwenyekiti wa CCM mkoa yupo hapa kaja kumwona. Nimewaambia Polisi mtu huyu asitolewe hospitali kinyemela bali atoe maelezo polisi kwanza. Huyu ni mtuhumiwa wa kwanza kabisa. Hali ya Kiwia sio nzuri sana. Anatakiwa kufanyiwa ct scan kuona athari aliyopata (maana kapigwa na shoka na mapanga
kichwani).Tusubiri uchunguzi zaidi wa Polisi.
Huyu muechimiwa hapo juu alisema huyo Ahmed ni mtuhumiwa wa kwanza, baadaye mwisho amesema Kiwia na Machemli ni watuhumiwa wa kwanza. Hivi kuna watuhumiwa wa kwanza wangapi?
Hivi kuna ulazima kwa Mbunge au mtu yeyote kila anapotaka kutoka usiku gizani atoe ripoti polisi?
Hiyo nyekundu, amekusudia nini kusema ni mtu wetu? Ni polisi mwenzao au magamba mwenzao?

Hii ripoti na maelezo ya huyu muechimiwa, yanatia kinyaa.
 
Mimi nawaomba POLISI wasitake kuwa chanzo cha ukosefu wa AMANI nchini, kwa nini saa hizi ndiyo wanazungumzia kwamba wabunge wana kesi ya kujibu-kuna kitu gani wanaofia? Hivi nchi hii wabunge hawana adhi, kwani nchi hii imetangaza hali ya hatari kwamba wananchi hawarusiwi kutembea kuanzia saa fulani mpaka saa fulani-HAKUNA, tuzungumze ukweli bila upendeleo wangekuwa ni Wabunge wa CCM wamevamiwa na kujeruhiwa kwa mapanga na mashoka na polisi ikapata habari unafikili saa hizi Mwanza kungekalika kweli?

Hii ni aibu kubwa kitaifa, mimi binafsi silioni kama ni tukio la KAWAIDA, hapa busara ya JK inahitajika haraka sana; Wabunge wanakatwa mapanga na mashoka sisi tunaona hilo ni jambo la KAWAIDA!!! Hiki kikundi kilicho fanya unyama huu walidhamilia nini-wawaue, alafu nchi hii ingetegemea pangekuwepo AMANI kweli; kwani mbunge akihitwa mahali fulani time yoyote haruhusiwi kwenda kuwasikiliza wapiga kura wake, kuna haja gani yakuweka mitego hili kuwajeruhi binadamu wenzao - inasikitisha sana.

Rwanda ilianza hivi hivi tusije tukajidanganya kwamba janga hilo aliwezi kutokea kwenye TAIFA letu, Serikali isiruhusu ma-vigillante wakawa wanajichukulia sheria mkononi, taifa likivurugika hakuna ambaye atabaki salama,TUSIJIDANGANYE.

Uchaguzi ulikwisha mwaka jana kwa nini watu waendeleze vinyongo na kutokuelewana-WHY?
 
Inasikitisha sana. Hivi ni kweli hawa polisi wameshindwa kukamata wahalifu eneo la tukio? Hainiingii akilini kwa polisi kueatuhumu wabunge wa upinzani waliojeruhiwa eti hawakuwa na kibali, inamaana huyo Ahmed Mkilindi na wanaCCM wenzake walikuwa na kibali cha kwenda kujeruhi usiku huo? Kwanini alijifanya ni mwanaCDM? Kwanini Mwenyekiti wa CCM MKoa alikuja kumuona Ahmed Mkilindi hospitalini? Mbona hawamkamati huyu Ahmed Mkilindi kwanza? Hivi wananchi wakiamua kuchukua sheria mikononi dhidi ya matendo kama haya tutawalaumu? Kwanini mnatulazimisha tukose imani nanyi kabisa?
 
Ninazidi kupoteza imani na jeshi la polisisiemu kila kukicha.

Nilimsikia RPC wa Mwanza jana akihojiwa redioni yaani anaongea utumbo mtupu!

Hawa watu sijui wamepeleka wapi akili zao na weledi wao!
 
jamani kila siku tunalalamika jeshi la polisi tz ni kichaka cha watu wasiojitambua...tubadili mfumo hata kama utatugharimu lakini utazaa matunda..wabunge hao wana bahati maana jamaa wangeweza kuvuta trigger ile style ya Zombe na kutuletea visingizio vyao vya chekechea
 
Jogoo awike asiwike kutakucha tu,hizi ni dalili za kifo cha mumiani CCM.
Tumeteseka sana,tumeonewa sana,tumedhulumiwa sana,tumenyanyaswa sana tunaomba 2015 ifike hata haraka tupate ukombozi.
 
Kila jambo lina mwanzo na mwisho,ukwel utafichwa but mwishowe ukwel huu utajileta tu na kama police wanaficha ukwel wataishia kuumbuka na kudharaulika tu.
 
CHANZO: Polisi kuwakamata wabunge wa CDM waliokatwa mapanga | Fikra Pevu | Kisima cha busara!

“Kukatwa kwao mapanga isiwe sababu ya kutokamatwa na polisi, lazima tuwakamate tuwahoji. Inawezekana wabunge hawa ndiyo chanzo kikubwa katika kesi hii.

alisema RCO Nsimeki ambapo alitania kwa kusema: “Unajua mtu anaweza kukutwa na mke wa mtu akakatwa mapanga na kichwa kikaning’inia, sasa utasema huyo mtu si chanzo?”.

Duh kweli akili za polisi zetu zinatiashaka! Hivi lakini huku si ndio huwa wanakwenda wale walifeli f4!!!

Hebu tujiulize kamanda anamaanisha nini anaposema kuwa wabunge hawa wanaweza kuwa ndio chanzo. Je, kuna mtu yeyote alienda polisi kushitaki au kutoa taarifa yoyote ya kufanyiwa fujo na wabunge hawa!!!?

Ata kama imewatokea kama anavyoeleza kwenye mfano wake wa mke wa mtu! Je, na yeye anaona kitendo cha raia kujichukulia hatua mikononi ni sahihi!!? Tusubili tuone wakikamatwa watashitakiwa kwa makosa gani!
 
Haki inazd kuwa historia kwenye taifa hili! Hata vyombo vilivyopaswa kusimamia bila kuwa biased navyo vimekua vyaonyesha kushindwa.
 
police inanipa hedekiii kwakweli,how comes wanashindwa majukum yao,au wametoka syri???????????
 
Wathubutu waone,tayari tuko full,Mwanza si Tabora,tunajua yote waliyopanga ila watafanikiwa kwa 99.9% ila 0.1% itawashinda na ndio ina thamani.Pole yao mapongo magamba.

haijui mwanza huyu RPC. Tuna hasira sana, we ngoja
 
CHANZO: Polisi kuwakamata wabunge wa CDM waliokatwa mapanga | Fikra Pevu | Kisima cha busara!

"Kukatwa kwao mapanga isiwe sababu ya kutokamatwa na polisi, lazima tuwakamate tuwahoji. Inawezekana wabunge hawa ndiyo chanzo kikubwa katika kesi hii.

alisema RCO Nsimeki ambapo alitania kwa kusema: "Unajua mtu anaweza kukutwa na mke wa mtu akakatwa mapanga na kichwa kikaning'inia, sasa utasema huyo mtu,"
, kwani hata kama ikiwa ni chanzo kwani inamjustify huyo mtu kuuua? Na je anakua above the law jus because kaibiwa mke?
 
Back
Top Bottom