Polisi kumng'ang'ania mtuhumiwa na hali ya kuwa walalamikaji hawana mpango na kesi tatizo ni nini?

Mwizukulu mgikuru

JF-Expert Member
Oct 21, 2021
4,737
11,095
Wakuu kuna jamaa yangu alipatwa na tatizo wakawa wamempeleka polisi, kule polisi akapata dhamana kwa sababu kosa lake lilikuwa lina dhamana, akaenda kuzungumza na wale waliokuwa wanamshitaki na wakawa wameelewana kuwa mambo yasiendelee mbele zaidi yaani kufika mahakamani.

Sasa changamoto iliyopo ni polisi kukomaa hasa yule mpelelezi aliyepewa jarada (file), kesi kaipeleka mahakamani na bado anamkomalia jamaa afike mahakamani, wanaomshitaki jamaa hawataki kesi wao wanapigiwa simu na polisi za vitisho ili wafike mahakamani, sielewi shida ni nini?🙃

Polisi wanaitafuta kwa nguvu zote aisee.
 
Ukitenda jinai umeikosea Jamhuri
Hapo lazima aende mahakamani atapata haki yake huko
Atashitakia na Jamhuri
 
Kama ni kesi ya jinai ikifika polisi mtu pekee anaeweza futa kesi ni DPP tu, ata wahusika wasipotaka iendelee.

Hao mashaidi wataenda tu mahakamani siku wakiitwa, ni kosa kisheria kuzuia ushahidi kwa kesi iliyofika mahakamani.

Option iliyobaki hapo ni ‘plea bargaining’ na prosecutor adhabu iwe ndogo maana wahusika hawana interest na case.
 
Wakuu kuna jamaa yangu alipatwa na tatizo wakawa wamempeleka polisi, kule polisi akapata dhamana kwa sababu kosa lake lilikuwa lina dhamana, akaenda kuzungumza na wale waliokuwa wanamshitaki na wakawa wameelewana kuwa mambo yasiendelee mbele zaidi yaani kufika mahakamani.

Sasa changamoto iliyopo ni polisi kukomaa hasa yule mpelelezi aliyepewa jarada (file), kesi kaipeleka mahakamani na bado anamkomalia jamaa afike mahakamani, wanaomshitaki jamaa hawataki kesi wao wanapigiwa simu na polisi za vitisho ili wafike mahakamani, sielewi shida ni nini?🙃

Polisi wanaitafuta kwa nguvu zote aisee.

Jinai ni mali ya Police, malizana nao tafadhali. Watawasumbueni na kuwapotezea mda.

Pia kesi haina nguvu kama kweli huyo mhusika hataki kesi, maana ushahidi wake ni lazima.

Inawezekana jamaa anawaimbisha ila anawaambia Police kabeni corner mpate hela, nchi ngumu hii, inaitaji watu jeuri.
 
Wakuu kuna jamaa yangu alipatwa na tatizo wakawa wamempeleka polisi, kule polisi akapata dhamana kwa sababu kosa lake lilikuwa lina dhamana, akaenda kuzungumza na wale waliokuwa wanamshitaki na wakawa wameelewana kuwa mambo yasiendelee mbele zaidi yaani kufika mahakamani.

Sasa changamoto iliyopo ni polisi kukomaa hasa yule mpelelezi aliyepewa jarada (file), kesi kaipeleka mahakamani na bado anamkomalia jamaa afike mahakamani, wanaomshitaki jamaa hawataki kesi wao wanapigiwa simu na polisi za vitisho ili wafike mahakamani, sielewi shida ni nini?🙃

Polisi wanaitafuta kwa nguvu zote aisee.
Ng'wizukulu Mgikoro...
Kabla ya kufunguliwa Jalada kesi mahakamani Walikuwa wana haki ya kuwithdraw case endapo ilikuwa haina viashria vya kuvunjwa kwa amani..
Kama kuna viashiria vya kuvunjika kwa amani endapo haki haikutendeka bhasi ni muhimu kesi kupelekwa mahakamani..
Kama kesi imeshafika mahakamani Then hapo huwa ni Jamhuri Against Huyo mtu na sio mshitaki tena ...
Lakini shahidi wa kwanza huwa ni mshtaki kama hatafika mahakamani..Kesi inaweza kuwa withdrew..

japo wanaweza kumtengenezea Kesinya kuzuia upelelezi na ushahidi (Kupitia sheria ya Ulinzi wa mashahidi..au ile sheria ya Whistleblower....
na pia anaweza kujikuta katika mikono ya TAKUKURU..
Cha msingi wanatakiwa kumfata mwwndesha mashtaka wakae chini kati ya Mwendesha mashtaka ,Mshitakiwa ,Mshtaki na Jaji ili swala linaisha kwa shauri la mwanzo kabisa ...
 
Hao wapumbavu kwa nini walimpeleka polisi kama hawakutaka kesi? Polisi wakiamua kuwashughulikia watakoma ubishi mpaka kamasi nyembamba ziwatoke!
 
Sasa kama kaongea na aliyewakosea wameelewana anaogopa nini. Huyo polisi anataka hela ya kufuta jalada kama anayo ampe kama hana anaogopa nini sasa, wacha kesi iende mahakamani mashahidi/mshtaki si ndio hao wameshaelewana. Hawatatokea tu mahakamani na kesi itafutwa
 
Wakuu kuna jamaa yangu alipatwa na tatizo wakawa wamempeleka polisi, kule polisi akapata dhamana kwa sababu kosa lake lilikuwa lina dhamana, akaenda kuzungumza na wale waliokuwa wanamshitaki na wakawa wameelewana kuwa mambo yasiendelee mbele zaidi yaani kufika mahakamani.

Sasa changamoto iliyopo ni polisi kukomaa hasa yule mpelelezi aliyepewa jarada (file), kesi kaipeleka mahakamani na bado anamkomalia jamaa afike mahakamani, wanaomshitaki jamaa hawataki kesi wao wanapigiwa simu na polisi za vitisho ili wafike mahakamani, sielewi shida ni nini?🙃

Polisi wanaitafuta kwa nguvu zote aisee.
Je, ni kesi ya jinai?
Kama kesi ni ya jinai, mshtaki ni Jamhuri ya muungano, aliyefungua kesi ni shahidi muhimu tu katika hiyo kesi na polisi ni chombo cha kukusanya ushahidi. Kwa hivyo mwenye jukumu la kufuta kesi ni ofisi ya mwendesha mashtaka wa serikali, sio mtuhumiwa wala polisi wenye mamlaka hayo.
 
Tofauti ya polisi na choo cha stendi ni kwamba choo cha stendi kiingilio pesa kutoka ni bure, ila polisi kiingilio bure kutoka ni pesa.
 
Wakuu kuna jamaa yangu alipatwa na tatizo wakawa wamempeleka polisi, kule polisi akapata dhamana kwa sababu kosa lake lilikuwa lina dhamana, akaenda kuzungumza na wale waliokuwa wanamshitaki na wakawa wameelewana kuwa mambo yasiendelee mbele zaidi yaani kufika mahakamani.

Sasa changamoto iliyopo ni polisi kukomaa hasa yule mpelelezi aliyepewa jarada (file), kesi kaipeleka mahakamani na bado anamkomalia jamaa afike mahakamani, wanaomshitaki jamaa hawataki kesi wao wanapigiwa simu na polisi za vitisho ili wafike mahakamani, sielewi shida ni nini?

Polisi wanaitafuta kwa nguvu zote aisee.
Kama alifanya jinai,mshtaki ni Jamuhuri.Hao walalamikaji ni mashahidi tu.Ongeeni na huyo mpelelezi mpatie pesa ili aende mahakamani atie Nolle au withdrawal as per CPA sect.91 au withdrawal sect.98.Usipofanya hivyo huyu nduguyo atahukumiwa.
 
Back
Top Bottom