Baadhi ya askari hawana nia njema, wanawatesa wananchi na kudhulumu mali zao

100 others

JF-Expert Member
Aug 5, 2017
3,626
12,057
Kuna kijana mtaani kwangu alikuwa anatoka kazini usiku, amepanda boda anaelekea nyumbani, ikatokea gari kwa nyuma na kuanza kumfuatilia, jamaa kafika nyumbani na kuingia ndani, sekunde chache tu akasikia mlango ukigongwa kwa nguvu na sauti za kibabe "fungua!!!, fungua!!!".

Jamaa akahoji nyie akina nani? Baada ya majibizano ya hapa na pale, jamaa wakavunja mlango, wakaingia ndani, wakamtandika jamaa haswa.

Wakamchukua jamaa mpaka kituoni, jamaa anawauliza askari mmenipiga hivi na mmenileta kituoni tatizo nini? Nina kesi gani? Polisi wakamwambia ana kesi ya wizi wa simu.

Jamaa kalala ndani hadi kesho, akaletwa dada mmoja anayedaiwa kaibiwa simu aje kuangalia mtuhumiwa na kuthibitisha, jamaa alipoletwa tu mbele ya yule dada, yule dada mpaka alikua analia huku akisema "ndio huyu!"

Jamaa alipigwa na mshangao, hofu na sintofahamu kwa wakati mmoja.

Jamaa akarudi selo, baada ya familia kufuatilia ili kumuokoa, familia ya jamaa ilibidi walipe laki nne, maskini ya Mungu kijana mwenyewe ndio kwao anategemewa.

Huyu kijana kwa kweli namfahamu, ana kibanda chake cha chips, hana hio michezo, lakini polisi walimkamata, wakampiga, wakachukua na pesa yake laki nne, hii ni dhuluma ya kiasi gani?

Kuna kijana mwingine tena ni boda, alikamatwa, akapelekwa kituoni akapewa kesi hio hio ya wizi wa simu, akaletwa mdada akathibitisha huyo boda ndio mwizi,lakini hawa vijana wote wamenihadithia mimi kwa nyakati tofauti na kiukweli hawana hizo tabia.

Baadhi ya askari hawana nia njema, wanawatesa wananchi na kudhulumu mali zao, hawa wanasababisha polisi wote waonekane ni wale wale.

Najua kuna wengi tu humu wana mikasa ambayo imewatokea au ndugu jamaa na marafiki wanaowafahamu.

Askari dumisheni ukaribu na wananchi, shirikianeni na wananchi, hata raisi kawaambieni... hakuna kitu kibaya kama wananchi kuwachukieni.

Huwa mkipanda kwenye hilo defender mnajiona kama dunia ni yenu, lakini kama hamna ushirikiano na wananchi ni kazi bure!
 
Kuna kijana mtaani kwangu alikua anatoka kazini usiku, amepanda boda anaelekea nyumbani, ikatokea gari kwa nyuma na kuanza kumfuatilia, jamaa kafika nyumbani na kuingia ndani, sekunde chache tu akasikia mlango ukigongwa kwa nguvu na sauti za kibabe "fungua!!!, fungua!!...
Lakini kaua usisahau hilo.
 
Whatever ila nyie magaidi mtapitia kwenye tanuru la moto hii ni Tanzania
Hauna kazi za kufanya, umejiunga Jul 2021 una message zaidi ya 300, mkuu tafuta kazi za kufanya... inaonesha ni jinsi gani unavyokurupuka kuandika upuuzi pasipo hata kutafakari.... ukipata kazi za kufanya utaacha huu utoto
 
Chanzo kimethibitishwa? au ndio mizuka na hisia ulizokuwa nazo? na hata kama chanzo kikiwa cha aina gani bado hakikupi mamlaka ya kutoa roho ya mwenzio kwani kosa kisheria.
Any way...
Kwani uchunguzi kuhusu Lissu kushambuliwa na Ben Saanane kupotea umefikia wapi?
We unazungumzia sheria ipi?
 
Mkuu kama ni kweli kisa cha kijana wa chips afanye kumshukuru Hamza tu hakuna namna usiombe ukutane na hawa polisi wetu ni watumishi wa hovyo sana baadhi yao na wanafanya matukio ya hatari kinoma nyuma ya pazia Mungu azidi kuwalaani polisi wote wanaodhulumu raia wema
 
Kuna askari mmoja aliniomba rushwa ya laki 1 kwa lazima nikagoma kumpatia akanilazimisha kwenda kituoni..
Kufika kituoni akanibanilishia case nakudai nimekamatwa kwa kosa la wizi wa kutumia siraha.
Shida yenyewe alinikamata naendesha gari kulitoa Geita kwenda Mwanza kwa ajili ya matengezo likiwa nimegongwa na hapo ndio alipodai trafic report nikamwambia sikupewa japo trafic wenyewe wa Geita ndio waliniruhusu kuchukua gari na bila ya kunipatia hiyo report.hapo ndipo mchezo ulipoanzia.
Mchezo ulikwisha saa 8 usiku baada ya jamaa yangu kuja na kubizana nao hapo ndipo waliponiachia lakini bado waliomba pesa ya soda 20,000
Police wetu wanamapungufu mengi sana hata kama ni ugumu wa maisha hata sisi raia huku mtaani nasi tunamagumu yetu sana.
Police wajifunze kutafuta pesa kwa jasho lao na wajue ajira walizonazo ni ajira kama ajira nyingine..ipo siku kazi itakwisha au kustaafu waishi na wafanye kazi zao kwa weredi na sio kukomoa au kuumiza raia.
 
Miaka 6 hakuna nyongeza ya mishahara huku viongozi na wabunge wakibadisha suti za kuvaa kila asubuhi , inauma sana.
 
Huyo mwizi kaamua kulipa simu aliyo iba we unajidai ndo unaujua undan wa mtu zaid
 
Any way...
Kwani uchunguzi kuhusu Lissu kushambuliwa na Ben Saanane kupotea umefikia wapi?
We unazungumzia sheria ipi?
Wenzako wanahesabu nazi ww una hesabu makuti,anyway Lisu na Saanane ndio akina na nani na wana umuhimu gani kwa taifa hili na walifanywa nini,unaweza nisaidia mimi si wafaham.
 
Wenzako wanahesabu nazi ww una hesabu makuti,anyway Lisu na Saanane ndio akina na nani na wana umuhimu gani kwa taifa hili na walifanywa nini,unaweza nisaidia mimi si wafaham.
Ni Lissu yupi ulikuwa ukimzungumzia kwenye hii comment? acha unafiki Mkuu!!!
Lissucmt.PNG
 
Ukiishafanyiwa tukio la uonevu, kinachotokea ni mtu kutumia akili za hisia, kufanya maamuzi tokana na hisia alizonazo kwa wakati huo, unakuta mwingine anakunywa sumu sababu ya mapenzi... anaamini hakufanyiwa haki... mwingine anaua kabisa...
 
Back
Top Bottom