Polisi Congo wahukumiwa kifo

sulphadoxine

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
2,257
645
101206153420_floribert_chebeya_304x171_bbc.jpg
Floribert Chebeya


Mahakama ya kijeshi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imetoa hukumu ya kifo kwa polisi wanne kwa kuhusika na mauaji ya mwanaharakti maarufu wa kutetea haki za binadamu.
Floribert Chebeya, mkuu wa shirika la ihsani la Voice of the Voiceless, aliuawa Juni mwaka jana.
Mwili wake ulipatikana nyuma ya gari lake karibu na mji mkuu wa Congo, Kinshasa, baada ya kuitwa makao makuu ya jeshi.
Watatu waliohukumiwa kifo hawakuwepo mahakamani.
Kulingana na shirika la habari la AFP, mahakama ilielezwa watu hao watatu ndio hasa waliohusika na mauaji ya Bw Chebeya ambao bado wako mafichoni.
Mahakama hiyo imempa polisi mwengine kifungo cha maisha, huku watatu wakiachiwa huru.
Mwandishi wa mjini Kinshasa Jonny Hogg aliiambia BBC mamia ya watu walijitokeza katika magereza ya Makala mjini hapo kusikiliza hukumu, iliyochukua saa chungu nzima.
Kanali Daniel Mukalay, mkuu wa polisi wa masuala ya kijasusi wakati wa mauaji ya Bw Chebeya, alikuwa mwenye cheo kikuu miongoni mwa polisi hao watano.
Alipewa hukumu ya kifo kwa makosa ya kupanga na kuagiza mauaji hayo, kimesema chombo cha habari cha AFP.
Hukumu ya kifo hakikutekelezwa tangu Rais Joseph Kabila alipochukua madaraka mwaka 2001.

 
Back
Top Bottom