Poleni wadau wa Emirates, huo ndio muziki wa Pep Guadiola

grafani11

JF-Expert Member
May 24, 2011
15,442
5,807
Poleni wadau na mashabiki wa Arsenal FC, nina imani hata nyinyi mlielewa nini kingetokea lakini baadhi yenu mliendelea kujipa moyo. Umiliki wa 70% kwa Bayern na 30% kwa Arsenal kwa kweli ilitusikitisha wengi hasa sisi wadau wa EPL.

Tujiulize ni kwanini Staa wetu OZIL anafichwa kwenye mechi kubwa kubwa na kuwika kwenye mechi ndogo ndogo??

Inabidi tujifunze kwa wazoefu wa ligi ile, kwanini mpaka sasa wao pekee ndiyo ambao hawajapoteza mchezo.
 
Ukweli ni kuwa Waingereza hupenda kusifia cha kwao na kukufanya wewe (mtumwa wao) udharau sio cha mtu mwingine bali chako mwenyewe, hili wamefaulu kwa baadhi yetu. Babu zetu walipinga kutawaliwa na wakaamua kupigana lakini leo vijana wetu wanapenda kutawaliwa hata kwenye fikra. Majanga.
 
Mkuu kwa hili tumetawaliwa. Maana vijana hata kazi hawataki kutwa kuongelea mechi za Ulaya tu.
 
Yaani mechi nilizotazama jana (Arsenal vs Bayern Munich) na ya juzi (Man City vs Barcelona), kiukweli nimeamini EPL bado kwenye pitch techinics, Germany na wenzetu wa La Liga wamekomaa na mpira wao upo juu sana, nilitegemea Man City afanye kitu kikubwa maana ni timu inayotisha England lakini hola....Tumewavulia kofia Germany na Spain aisee!
 
Refa alituua. Alipomtoa kipa basi mambo yakaharibika. Ile haikuwa fair penalt. Mbona yale aliyemkwatua Ozil hakutolewa wakati yake ilikuwa kali zaidi ya kipa wa Arsenal?. Tukienda kwao nao watachezea kichapo!
 
Tusubiri Manichester United ijipange upya kwa mwaka huu, kwani wao na Chelsea ndiyo pekee wazoefu wa Ligi ya Mabingwa Ulaya. Hawa wengine wanaishia kujigamba nyumbani tu.

Man United na Chelsea (The Blues) wanajua wanachokifanya hasa linapokuja suala la Mechi za nje ya England kama za UEFA.
 
Refa alituua. Alipomtoa kipa basi mambo yakaharibika. Ile haikuwa fair penalt. Mbona yale aliyemkwatua Ozil hakutolewa wakati yake ilikuwa kali zaidi ya kipa wa Arsenal?. Tukienda kwao nao watachezea kichapo!
Unaelewa nini kuhusu faulu iliyotendwa na mtu wa mwisho kwa minajili tu ya kuzuia goli lisifungwe na ile ya kawaida ndani ya mchezo???
 
Toni kroos jana alikuwa mwiba kwa Arsenal,jamaa yuko vizuri sana maana hata ukiangalia alipiga passes 117 na kapoteza 3 tu.
 
Toni kroos jana alikuwa mwiba kwa Arsenal,jamaa yuko vizuri sana maana hata ukiangalia alipiga passes 117 na kapoteza 3 tu.
Mimi alinifurahisha lile bomba lililompeleka kipa wa Arsenal Fabiansk kujigonga kwenye mwamba mpira ukijaa wavuni.
 
Huo ni mtazamo wako na si sheria na kanuni 17 za soka hasa linapokuja suala la "last man standing" ndani ya eneo lenu la hatari.
Sawa mkuu uamuzi wa refa ndio wa mwisho. Kichapo tumekipokea kwa mikono miwili.
 
Mimi alinifurahisha lile bomba lililompeleka kipa wa Arsenal Fabiansk kujigonga kwenye mwamba mpira ukijaa wavuni.
Lakini kuna lile alilopangua yule aliyetolewa lina fanana na lile ila jamaa alilifuata mzima mzima na ilikuwa upande ule ule. Ila yule dogo asingetolewa Gunners walikuwa wanashinda ile mechi.
 
Me nadhani Arsenal waliangushwa sana na Ozil kukosa penalty, red card ya golikipa wao ambayo kwa mtazamo wangu haikua fair, na maamuzi mabovu ya Wenger (sijui alipaniki?)

Bayern wanapewa sifa nyingi lakini tukumbuke walikua wanacheza na watu 10, wangekua wakali kama wanavyosifiwa walitakiwa washinde goli nyingi.

Ni mapema sana kuongea lakini Bayern hii itasumbuka sana ikikutana na team inayocheza good counter attacking football kama Chelsea au ATL

Manchester City sikuwapa nafasi ya kumfunga Barcelona, kwa sababu pamoja na sifa za kijinga wanazopewa na english media, tuliona jinsi walivyopata shida kwenye mechi za ligi dhidi ya Liverpool ambayo walishinda kutokana na maamuzi mabovu ya refa na ile waliyopotezwa na Chelsea.

Barcelona nayo haijakutana na watu wa mipango kama PSG, kwa kweli imekua team ya kawaida sana.
 
Basi mi nikajua anaongelea Emirates shirika la ndege maana kwenye front page penyewe title nzima haionekani kumbe Arsenal.. kwa heri
 
Back
Top Bottom